Utata wa kifo cha Mwanamke wa Isdal

Apr 25, 2020
29
56
images (16).jpeg


Ilikuwa mchana wa Novemba 29,1970 ambapo familia moja ambayo ilikuwa na Baba na Binti wawili wenye asili ya Norway walikuwa wakienda kutalii katika Mlima Ulriken upatikanao katika Jiji la Bergen, Watalii wengi hupenda kupanda Mlima huo uliojaa barafu na nchi ya Norway ni nchi ya baridi kali na barafu. Kabla ya kuanza kupanda mlima huu kuna bonde kubwa ambalo upande mmoja una barafu na upande mwingine hauna barafu nalo ni kivutio cha utalii.

Familia hii ilipita upande wa bonde usiokuwa na barafu ambapo kumejaa mawe makubwa na miamba na wakiwa wakimalizia bonde hili, mmoja wa watoto wa mzee huyu akaona saa kwenye moja ya jiwe kubwa. Yule mtoto akakimbilia kwenye lile jiwe aliloona saa huku familia yake ikimshangaa anaelekea wapi na kuanza kumuita kwasababu huko alikokuwa anaelekea kulikuwa na mawe ambayo yametengeneza maficho ya kutisha ambayo ni hatari pia.

Mtoto huyo alipokaribia saa, akaona kitu kilichomshtua na kumfanya apige ukelele na kuifanya familia yake kushtuka na kumkimbilia kule alikokuwa kujua sababu ya ukelele huo ni nini, na kama nilivyoelezea hapo alikuwa eneo hatarishi. Wakakutana na mwili wa mwanamke ambao umeungua na kuharibika sana hata kutambulika ni vigumu, hapo hapo baba wa familia hiyo akatoa taarifa polisi. Mtaa karibia na bonde hilo kulikuwa na polisi mwanasheria ambae ndiye wa kwanza taarifa hizi kumfikia ambaye aliitwa Carl Halvor Aas, ambapo aliuona mwili wa mwanamke huyu ukiwa umeungua sana huku amelala chali huku mikono yake ikiwa imeelekea juu na kutengeneza utata flani kuwa labda alikuwa anajitetea au ndio pozi la kukata roho.

Afande huyu hisia zake za haraka zikamuongoza kuwa ni tukio la kujitoa roho na ukizingazia historia ya bonde hili "death valley"....maiti ya mwanamke huyu ilikuwa imezungukwa na vitu vinavyoaminika ni vya kwake, hata walipoenda kupima DNA walikuta ni vya kwake. Juu ya jiwe mojawapo kulikuwa na saa ya kike nzuri, bangili na hereni za kuvutia.

Chini pembeni ya mwanamke huyu kulikuwa na mwavuli uliovunjika, galoni la mafuta, chupa mbili za vinywaji zilizotupu, nguo nzito na hapa ni kwasababu ni nchi ya baridi na kingine kilichokutwa na viatu.

Wapelelezi wakaanza kuvikagua hivi vitu, huku wakivikusanya kwa ajili ya ushahidi na uchnguzi zaidi na kilichowashangaza zaidi nguo na chupa zimeondolewa label zake za utambuzi na kuzidi kuwachanganya wapelelzi hao na jinsi vitu hivyo vilivyosambazwa kama alivivua na kuviweka hapo. Wakaendelea na kuchunguza mwili ukiwa hapo eneo la tukio na wakiwa na mfuko wa kubebea maiti.

Lakini ghafla wakiwa kwenye harakati za kuubeba mwili huo, walishtushwa walipokuwa wanataka kuubeba na kukuta hajaungua sehemu ya nyuma kabisa kwani ni hali isiyo ya kawaida mwili uungue sana eneo la mbele tu. Shingoni pia walikuta mikwaruzo/michubuko na maswali mengi yakazuka na kuzidi kuchachua hisia zao za awali kuwa kama alijichoma moto mwenyewe iweje asiungue sehemu ya nyuma?

Wapelelezi wakaondoka na mwili na vitu vyote walivyovikuta eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu na baadhi ya wapelelezi wakabakia eneo la tukio kuchunguza kama wataona kiashiria kingine chochote. Wakati wakiendelea kuangalia huku na huko wakagundua sehemu familia ile ilipougundua mwili huo si njia ya kupanda mlimani na familia ile ilijieleza kuwa ilikuwa na safari ya kupanda mlima hata afande Carl alithibitisha kwa mizigo na mavazi yao yalikuwa yanadhihirisha walikuwa wanapanda mlima. Wapelelezi wakaamua kuwaweka kiporo maana hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhusika na tukio hili, na si kuwa njia hii haifikishi watu mlimani bali si njia rasmi maana ilifungwa baada ya kusababisha maafa kwa watu waliokuwa wanapanda mlimani ambapo miaka ya 1960 kundi flani lilianguka na kupoteza maisha lote, hivyo serikali ya Norway ikafunga njia hiyo.

Hospitalini madaktari wakafanya uchunguzi na majibu yakatoka na yakazidi kuwavuruga wapelelezi hao, kwani tumboni walikuta takribani vidonge 70 vya usingizi ambavyo havijayeyuka na kuingia kwenye mishipa ya damu ili viweze kuleta matokeo pia mapafu yake yalikuwa na moshi na hitimisho likawa mwanamke huyo alichomwa/alijichoma moto mwenyewe.

Vichwa vikazidi kupata moto, kwamba ni nini kilichotokea kwa huyu mwanamke maana dawa ukishameza zinayeyuka mwilini na kwa ripoti hii inamaana alikata roho kabla dawa hazijaanza kufanya kazi na ukichanganya upatikanaji wa moshi kwenye mapafu inahitimisha kuwa kilichomuua ni moto huo. Wapelelezi wakapata picha kuwa mwanamke huyu alikufa kifo cha mateso na kikatili sana cha kuchomwa moto akiwa hai. Swali la kwanini hakuungua maeneo ya mgongoni, wapelelezi na madaktari kwa muda huo wakashindwa kung'amua kwani mtu akichomwa moto akiwa hai maanake angejiviringisha na hata moto kusambaa maeneo mengine mwilini ikiwamo mgongoni.

Taarifa za mwanamke huyu zilisambaa kote Norway ili kama kuna ndugu, jamaa au rafiki aliepotelewa na mtu wake aweze kuripoti polisi, hakuna yeyote aliejitokeza na hakuna taarifa yoyote polisi kuhusiana na mwanamke mwenye sifa hizo.

Siku ya nne wapelelezi wakiendelea kukuna vichwa vyao, akajitokeza jamaa mmoja na kuanza kuongea na wapelelezi kuhusu mwanamke huyo ambae bado hajajulikana.
Huyu mtu alikuwa muuzaji wa duka kubwa la nguo na viatu jijini Bergen na alikuwa shahidi wa kwanza kusema anamfahamu huyo mwanamke kwani alishakuja dukani kwake kununua viatu hivyo ambavyo vilitangazwa kwenye vyombo vya habari.

Viatu alivyokutwa navyo mwanamke huyu kwa wakati huo vilijukikana kama "Celebrity boots", ambavyo bei yake ilikuwa juu sana kipindi hicho, hivyo vilivaliwa na wachache sana.

Wapelelezi wakataka picha ya mwanamke huyo inafananaje maana uso na nyweke zake zilikuwa zimeungua kiasi cha kutofahamika na ndipo muuza duka huyo akaanza kuwaelezea anavyofanana na ndipo sasa wapelelezi wakafanikiwa kuchora taswira yake kwa maelezo ya muuza duka huyo.

Kwa picha hiyo, bado hakuna aliejitokeza kuwa anamfahamu na ndipo wapelelezi wakambatiza jina la Isdal huku wakiendelea na uchunguzi wao, wakati mambo haya yakiendelea polisi jijini Bergen wakapata taarifa kutoka kwenye station ya treni jijini apo kuwa kuna mizigo iliachwa hapo kwa muda mrefu na haijulikani ni ya nani! Polisi wakaelekeza ipelekwe kituoni kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Mizigo yenyewe ilikuwa masanduku na briefcase kubwa mbili, moja ya rangi nyeusi na nyingine rangi ya fedha.

Baada ya kufikishwa kituoni, mizigo ikakaguliwa na kifaa maalumu cha kukagulia mabomu na vilipukizi ili isije kuwa ni mtego wa bomu maana miaka hiyo ilikuwa ndio kipindi cha vita baridi na Norway ilikuwa imetoka kujaribisha kombora lake la masafa marefu, hivyo kuwa tishio kwa nchi nyingine. Kifaa kikaonesha kuwa masanduku hayo hayana shida yoyote, ikabidi sasa kuyafungua na kuanza kutoa vilivyomo, katika masunduku hayo kulikutwa na vitu kama nguo za ndani za kike, mawigi, fedha za kigeni za Ujerumani, Norway na sarafu za kigeni za Uingereza na Uswizi, chanuo na brush, manukato, vijiko vya chai, cream, mfuko wa Oscar Rortvedt's Foot wear store ambapo ni duka la viatu huko Stavanger, miwani, paspoti za nchi 8,diary na business cards.

Polisi wakaingiwa na wasiwasi baada ya kukuta vitu hivyo na kilichowapa waswasi sana ni mfuko huo wa Oscar Rortvedt's na kuamua kuyapeleka mbele masanduko hayo kwa wapelelezi maana huo mfuko ni wa lile duka kubwa la nguo na viatu la yule jamaa ambae alisaidia kupatikana kwa taswira ya mwanamke huyu wa Isdal...

Wapelelezi baada ya kufikishiwa masanduku hayo wakaanza kuvichunguza vitu vya ndani ya masanduku hayo, waliingiwa na wasiwasi zaidi pale walipogundua nguo zote zimeondolewa label zake na cream zote zimeondolewa label zake, wapelelezi wakamkumbuka mwanamke wa Isdal ambae tuliona mwanzoni kabisa nguo zake zilikuwa zimeondolwa label za utambuzi na walipouona tena mfuko wa duka la yule jamaa wakaanza kuunganisha dots kuwa hayo masanduku yanahusiana na mwanamke wa Isdal.

Kwa picha hiyo, bado hakuna aliejitokeza kuwa anamfahamu na ndipo wapelelezi wakambatiza jina la Isdal huku wakiendelea na uchunguzi wao, wakati mambo haya yakiend

Vile vitu vilivyokutwa kwenye begi vilikuwa havina alama zozote za vidole, isipokuwa miwani kwenye lens zake wakashukuru sana maana isingekuwa hivyo kizaazaa kingetanda zaidi. Baada ya vipimo vya alama za vidole vya miwani wakakuta alama za vidole zinaendana na mwanamke wa Isdal na ndipo wakajidhihirisha ya kuwa hivyo vitu ni vya kwake.

Na ndio joto la kesi likaongezeka ara dufu maana haiwapi tena mwanga zaidi ya kuongeza giza totoro mbele yao, maswali yakawa mengi zaidi kuwa huyu mwanamke ni nani? Utaifa wake ni upi? Na ile fedha za nchi mbalimbali zilikuwa za nini? Mizigo yake iliachwaje station?

Wapelelezi wakazicukua zile business card wakaanza kutafuta jina na namba walau waweze kupata msaada juu ya mwanamke huyu maana utata ni jinsi ambavyo mpaka wakati huo wameshindwa kuutambua uhusika wa mwanamke huyo. Wakafanikiwa kumpata mwenye hiyo business card, alikuwa ni mpiga picha wa kiitaliano na mahojiano yakaanza mara moja dhidi yake. Mpiga picha huyu akaanza kujieleza kuwa kweli alikutana na mwanmke huyo siku za nyuma kidogo baada ya kumpa lift na alipomshusha mwanamke huyo ndio akampa business card yake na ambapo alikuja kumtafuta kupitia simu za jiji na wakafanikiwa kukutana na kupata chakula cha jioni na kupiga story kadhaa na nia ya mwanamke huyo ni kuwa siku moja aje ampige picha. Ila toka walipoachana siku hiyo hawakuweza kukutana tena, na hakujua kama alikutana na mkasa huo wa moto. Wakaamuliza mpiga picha huyo kama alitajiwa uraia wa mwanamke huyo, akamjibu kuwa ni raia wa Afrika Kusini, wakamuuliza swali la pili kuwa walikuwa wanatumia lugha gani kwenye maongezi yao? Jamaa huyo akamjibu kuwa ni kiingereza ila chenye lafudhi ya lugha mama yake, hapa akimaanisha mwanamke huyo si wa taifa la wazungumzaji wa kiingereza, wapelelezi walimuuliza maswali mengine ambayo hayakuwa na msaada wowote ule.

Sasa ikabidi wapelelezi hao wawasiliane na mamlaka za Afrika Kusini ambapo kwa wakati huo walikuwa makaburu, mamlaka za upelelezi za Afrika Kusini zikasema hazina mtu wao aliepotea mwenye sifa za kama huyo mwanamke na kwa namna watu weupe walivyokuwa wachache ilikuwa raisi kugundua kuwa mtu flani amepotea. Hivyo business card haikuweza kuzaa matunda zaidi tu ya kuwafahamisha kuwa mwanamke huyo si raia wao ukikumbuka kuwa mpiga picha alisema lafudhi ya mwanamke huyo ni tofauti hivyo kitendawili kikazidi kuwa kikubwa

Kitu cha mwisho kwenye yale masandunduku kilikuwa ni diary, ambayo ilipofunguliwa kwa ndani ilikutwa na maandishi flani ambayo yalizidi kuwaongezea utata (codes), sifa yake ni usiri maana yake mwenye nacho ndio pekee mwenye uwezo wa kutambua ni nini kipo kwenye huo ujumbe na wapelelezi walipata ugumu sana kutambua ni nini kilichokuwamo kwenye hiyo code.

Wakaamua kushirikisha shirika lao la ujasusi, ili waweze kuwasaidia kung’amua codes hizo na baadae wakaamua kuyashirikisha mataifa mengine ya kijasusi duniani ili kuwasaidia kung’amua codes hizo, mashirika hayo nayo yalichemka kung’amua chochote na kuomba kupewa muda zaidi. Na shirika la ujasusi nchini Norway lilivyoshindwa kung’amua codes hizo, likaamua kufanya uchunguzi wa peke yake kuhusu mwanamke huyo (individual investigation), kwani shirika hilo liliona kesi hiyo inaweza kuwa pana zaidi kutokana na mazingira yake na ikahusisha maswala ya kiintelejensia zaidi. Hivyo likaamua kulivalia njuga swala hilo bila kushirikisha taasisi yoyote ile ya kijasusi.

Wapelelezi wakaamua kuziweka kiporo zile codes na kuendelea na vipengele vingine huku magazeti ya nchini humo kwenye kurasa zake za mbele zikitanda habari za mwanamke huyo na jinsi ambavyo mamlaka hazijaweza kung’amua chochote na suala kubaki kuwa kitendawili. Siku zinazidi kuyoyoma na wapelelezi wakaamua sasa kuzunguka hoteli mbalimbali kuona labda amepita/kulala huko maana wameshagundua kuwa ni mgeni na wapelelezi wengine wakaamua kuzunguka kwenye nyumba za kukodi kwani inaweza kuwa amefikia huko pia. Baada ya kuzunguka hoteli kadhaa wakafikia hoteli moja jijini Bergen inaitwa Neptun, wakakutana na mhudumu wake ambae alikuwa mwanamke aliitwa Alvhild Rangnes ambae alikuwa na miaka 21 kwa kipindi hicho, na baada ya mahojiano nayo kidogo mhudumu huyu aliweza kumkumbuka huyu mwanamke afananae na maelezo ya polisi.

Wapelelezi wakaomba awaelezee afananvyo huyo mwanamke na akawa anataja sifa zile zile ambazo alizitaja muuza duka awali. Basi wapelelezi wakaomba kitabu cha wageni ili waweze kujua alitumia jina gani, wapelelezi wakaona alitumia jina Alexia Zarne-Merchez kutoka Ljubljana na amekaa tokea tarehe 30 Octoba mpaka 5 Novemba na kwenye fomu alijaza ni mkazi wa Uingereza (London)-tizama picha chini, basi wakafananisha miandiko na kwenye ile diary na kukuta miandiko inafanana vile vile basi wapelelezi wakakenua meno bila kujua ugumu ndio unazidi kuongezeka kwenye hii kesi, wakaanza kumhoji vizuri huyu mhudumu na kuwaambia kuwa alikuwa mtu wa fashion kwa namna alivyokuwa amevaa mwenye machejo na kuna wakati alimkonyeza kidogo, aksema pia anaongea lugha ya kijerumani wakamuuliza tena vipi kuhusu lugha ya nyumbani kinorway akawajibu nayo anazungumza vizuri tu sema alikuwa hapendelei sana kukiongea.

Wakammuliza ulijuaje kuwa anazungumza kijerumani, akasema kuwa kuna siku alikuwa anamuhudumumia sehemu ya kula chakula hapo alikuwa ameketi mwanamke huyo pembeni kulikuwa na wageni wengine ambao walikuwa maafisa wa jeshi la maji wa Ujerumani ndipo mwanamke huyu akakuta anawasalimia maafisa hao kwa lugha ya kijerumani na kuongea maneno mawili matatu ila hakutulia maanani na kuendellea na mabo yake.

Ingawa hakukuwa na mahusiano yoyote zaidi ya kukatana hapo kwenye hoteli yao na maafisa hao wa kijeshi waliondoka zao eneo hilo na hakuona akijihusisha nao mpaka siku mwanamke huyo alipomaliza muda wake wa kuishi hapo hotelini. Cha mwisho wapelelezi walichopata kutoka kwa mhudumu huyo ni kuwa muda mfupi ambao mwanamke huyo aliokaa hapo alikuwa akibadilisha vyumba na alifanya hivyo mara tatu ila hajui kwanini mwanamke huyo alipenda kufanya hivyo. Wapelelezi wakaondoka na maswali mengi sana vichwani mwao na kuamua kuzunguka hoteli zote jijini Bergen kuona kama alifikia hoteli nyingine na hapo ndipo walipogundua kuwa alifika kwenye hoteli takribani tisa! Na alitumia majina tofauti na paspoti tofauti pia, unapochukua chumba kwenye hoteli kubwa unatakiwa kuonesha paspoti yako na kujaza majina kama yanavyoonekana kwasababu za kiusalama zaidi na mwanamke huyu alikuwa akifanya hivyo ila kwa kutumia passports tofauti tofauti kutokana na kuwa na paspoti kadhaa za majina tofauti kama tulivyoona kwenye uchuguzi wa masanduku.

Njia walizokuwa wakitumia kujua kama ni yeye walikuwa wakifananisha miandiko ikitumiwa katika kujaza kitabu

Hoteli alizopitia, mjina yake bandia na muda aliokaa ni kama ifuatavyo:
1. Genevieve Lancier, kutokea Louvain, alikaa Hoteli ya Viking, Oslo kuanzia 21-24 Machi 1970

2. Claudia Tielt, kutokea Brussels, alikaa Hoteli ya Bristol, Bergen kuanzia 24-25 Machi

3. Claudia Tielt, kutokea Brussels, alikaa Hoteli ya Skandia, Bergen kuanzia 25 Machi mpaka 1 Aprili

4. Claudia Nielsen, kutokea Ghent, alikaa Hoteli ya KNA, Stavanger kuanzia 29 -30 Oktoba

5. Alexia Zarne-Merchez, kutokea Ljubljana, alikaa Hoteli ya Neptun, Bergen kuanzia 30 Oktoba mpaka 5 Novemba

6. Vera Jarle, kutokea Antwerp, alikaa Hoteli ya Bristol, Trondheim, kuanzia 6-8 Novemba

7. Fenella Lorch, alikaa Hoteli ya St Svithun, Stavanger kuanzia 9 mpaka 18 Novemba

8. Ms Leenhouwfr, alikaa Hoteli ya Rosenkrantz, Bergen kuanzia 18 - 19 Novemba

9. Elisabeth Leenhouwfr, kutokea Ostend, alikaa Hoteli ya Hordaheimen, Bergen kuanzia 19-23 Novemba

Hizo ndizo hoteli alizoweza kufikia kwa kipindi cha kutokea Machi mpaka Novemba, ingawa ilipofika aprili alirudi tena Octoba na akazidi kuwachanganya wapelelezi kuwa kipindi cha hapo kati yaani Mei mpaka Septemba alikuwa wapi? au alirudi nyumbani kwao? maswali yalizidi kuzaliwa vichwani mwao, wapelelezi wakakubaliana kuwa majina yote yanayoonekana si yak wake nan chi ya Ubelgiji ndio imeonekana sana ndiko alikotekea! Hivyo wakaamua kuwailiana na idara za usalama za nchini Ubelgiji kuwa kama mtu huyo ni wa kwao. Ubelgiji wakasema hawana upotevu wa mtu yeyote mwenye sifa kama hizo, sasa kesi ikazidi kuwa nzito kwa wapelelezi maana kiza kilitanda kila wanapojaribu kupeleleza.

Basi wakakubaliana kurudi kwa tabibu mchunguzi na kufanya kufanya uchunguzi zaidi wa kimaabara (autopsy/postmortem) ya kinywa cha mwanamke huyo, ambapo iliwabidi kung’oa mfumo wao wa meno ili kuchunguza na kujaribu kupata angalau ishara kuwa inaasili gani au ametokea wapi (hapa nifafanue kidogo, huu uchunguzi kwa kitaalamu unaitwa Isotope Analysis ambapo huchunguza elements mbalimbali zinazounda kinywa/meno ambapo ni Oxygen Isotope Analysis (uchunguzi wa maji na maeneo yanakotokea) na Strontium Isotope Analysis (aina ya chakula, udongo wa eneo alilokulia)), na unaambiwa ndio mara ya kwanza Norway kufanya uchunguzi huu maanake maji yaliwafikia hingoni na uliratibiwa na Norwegian Criminal Investigation Service (Kripos) na Chuo Kikuu cha Bergen. Mwanamke huyo alikuwa na meno ya kipekee-14 yalikuwa yamejazwa (root canal), na yalijazwa kwa vikofia vya dhahabu na ni nadra kwa range ya umri wake (25-40) na sio aina ya dental works zinazofanyika Norway.

Pia wapelelezi waliwaita wataalamu wa miandiko kuchunguza miandiko yake ili kuweza kung’amua ametokea sehemu gani duniani, basi tatibibu na wataalamu wa miandiko wakaja na majibu yanayotofautiana kidogo.

Mtabibu alisema kwa asili ya meno yake ambayo mengine yalikuwa na rangi ya dhahabu ni watu wa asili ambao hupatikana mpakani mwa Ufaransa na Ujerumani, ila wale wa mwandiko wakasema mwanamke huyu anaweza kuwa wa asili ya bara la Amerika ya Kaskazini au mataifa yay a katikati mwa bara la Asia. Wakawasiliana na mataifa husika kuhusu mwanamke huyu kama walivyokuwa wakifanya awali nao wakasema hawana rekodi za mwanamke kama huyo na kuwataka Norway kuendelea kupambana na hali yao.

Wakati wapelelezi wakinyukwa vikali, basi majasusi wa Norway na sehemu mablimbali duniani walikuwa wanalala na kuamka na karatasi yenye zile codes. Basi jopo la wataalamu hao wakaja na majibu ya hizo codes na si codes ziling’amuliwa na ambazo walipata maana yake zilihusu muda na tarehe ya maeneo ambayo alikuwepo kama ilivyoelezwa hapo juu.

Codes hizo zilitafsiriwa kama hivi (O=Octoba, P=Paris ambapo alikaa 22-28 Octoba, B=Bergen ambapo alikaa 30 Octoba mpaka Novemba 5). Kesi hii ikazidi kuwa ngumu kwa wapelelezi kwani wakimaliza hili linakuja jingine gumu zaidi,maana hawaelewi kwanini mwanamke huyu aliweka siri sana kwenye mapito yake! Na kilichowanyima raha zaidi ni juu ya codes nyingine ambazo walishindwa kung’amua. Mpaka hapo wapelelezi wakanyoosha mikono juu maana mambo mengi ila muda mchache na walichokifanya ni kuhitimisha story hii kwa kutoa summary ya upelelezi wao na mabyo ndio ilifunga kesi hii kwa wao kama idara ya upelelezi.

Ripoti y auchunguzi ilisema kutokana na kukutwa na vidongo vya usingizi mwilini mwake vipatavyo 70 inamaanisha kuwa mwanamke huyu alijiua mwenyewe, wakafunga hivyo wapelelezi wa Norway maana kiza kilizidi kutanda kwenye hiyo kesi ilahali na wao wanahisi haiwezekani mwanamke huyoakawa amejiua mwenyewe. Mara zote kesi inapofika hapo kwa wapelelezi na kinachofuata ni nadharia kuwa labda ilikuwa hivi ama vile. Kabla hatujaelekea kwenye nadharia hizo mnamo mwaka 1971 baada ya kesi hiyo kufungwa na mamalaka nchini Norway wakaamua kumtoa viungo muhimu kama figo na maini wakiamini zitasaidia huko mbeleni pale teknolojia itakapokuwa imekua zaidi.

Baada ya hapo wakampa heshima ya maziko kama mkatoliki maana raia wengi waishio kati ya Ufaransa na Ujerumani wengi wao ni wakatoliki na wakamzika kwenye jeneza lilopambwa na lilacs na tulips huku likiwa na zinc ili asioze, shabaha yao ili asioze ni kuwa ipo siku ndugu zake watajitokeza na watachimbua kaburi hilo ili kufanyanya maziko upya kwenye heshima zao maana hapo kazikwa ugenini na maafisa wa polisi tu.

Kaburi lake , halina maandishi yoyote, msumaa na shada la maua.

Sasa tufuatilie nadharia kadhaa:
1. Alijiua mwenyewe, hii ndio nadharia kuu kuliko zote ambayo ndio iliyofunga kesi hii, ila mapungufu yake haijaweza kung’amua mwanamke hyo ni nani nap pia swala la moto halijazungumziwa ila tu umezaji wa vidonge ndio ulionekana kama suicide! Maana kama ni kujiua tu angekunywa tu vidonge, kwanini ajichome tena moto? What if alilazimishwa kunywa vidonge kisha kuchomwa moto? Na vipi suala ya kutoungua kabisa mgongoni?

2. Mwanamke huyu alipata ajali ya moto na kuungulia hapo chini! Nadharia hii ni dhaifu kabisa, nani aliuwasha moto, kwanini asiuungue mgongoni, vipi kuhusu nguo na vitu vingine vilivyopatikana pemebni yake, kulikuwa na dumu la petrol pembeni na mwili pia ulikuwa umemwagiwa mafuta hayo kabla ya kuunguzwa,vipi vidonge vilifakaje tumboni, kama alikuwa anapanda mlimani mbona hakukuwa na vifaa vya kupandia mlima?

3. Kuhusu mwanamke huyo kuwa shushu, ikumbukwe kilikiwa kipindi cha vita baridi, kulikuwa na watalii wengi Bergen kwa kipindi hicho n mwanamke huyo alionekana kuwa alikuwa anajiweza kifedha. Hivyo basi kutakuwa kulikuwa na mashushu wengi wa krusi anasema Gunnar Staalesen ambae ni mwandishi wa Makala za kesi mbalimbali hapo Bergen ambapo kwa kipindi hicho alikuwa mwanafunzi. Anasema kuna kipindi Mossad agent aliua mtu huko Lilehammer wakimdhania ni mtalii shushu, walihisi pia kulikuwa na uchunguzi wa roketi za kijeshi za Norway lakini bado hakuna ushahidi wenye mashiko juu ya hili.

4. Mwaka 2016 wachunguzi waliyachunguza tena meno yake na kuhitimisha kuwa anatokea kusini mwa Ujerumani na alikulia Ubelgji na ana umriwa miaka 40! Swali ni je, alikuwa nani na laikufaje? Ilifika mahali wakahisi walichora vibaya maana picha zilisambaa duniani kote na hakutambulika kabisa. Pia taarifa za awali zilionesha kuwa mwanamke huyo hakuwahi kuwa mgonjwa na hakuwahi kuzaa au hata kupata mimba tu!
Usisahau kulike page
#Abnockfacts

Kwa mavitu mengine kama haya nende FB halafu search ABNOCK MEDIA
Logopit_1618574214882.jpg
 
Watu wengine bana wagonjwa sijui??/ sasa theme ya huu utoporo ni nini?? na akili zako kabisaa, unajifunza kuandika au!!
 
Back
Top Bottom