Utaratibu unaotumika kuanzisha huduma ya maabara na zahanati binafsi

Sina ujuzi wala utaalam,ila naitaji kufungua zahanati yangu binafsi na kuajiri watu, nianzie wapi ili niweze kutimiza masharti na matakwa yote ili nitimize lengo,au nianzie wapi. Msaada tafadhari
 
Wakuu naomba msaada kwa yoyote mwenye uzoefu na uendeshaji wa dispensary ama maabara.Ningependa kujua kila kitu kuhusu hii industry .
CHANGAMOTO ZAKE
UENDESHAJI WAKE
MAPATO YAKE
NA USAJILI.
 
Wakuu naomba msaada kwa yoyote mwenye uzoefu na uendeshaji wa dispensary ama maabara.Ningependa kujua kila kitu kuhusu hii industry .
CHANGAMOTO ZAKE
UENDESHAJI WAKE
MAPATO YAKE
NA USAJILI.
Mkuu kama utapata hii na mimi nipo interested pia
 
Sina ujuzi wala utaalam,ila naitaji kufungua zahanati yangu binafsi na kuajiri watu, nianzie wapi ili niweze kutimiza masharti na matakwa yote ili nitimize lengo,au nianzie wapi. Msaada tafadhari
Uko mkoa gani na wilaya gani?
1. Andaa jengo Kwa ajili ya huduma ya afya.
2. Maandalizi hayo, yaonyeshe, mapokezi, maabara na chumba cha sindano na chuma cha daktari, pia at least vyuma viwili vya kupumzikia Wagonjwa.
3. Nenda ofisi ya afya kwenye wilaya yako, wambie nataka kufungua zahanati. Watakwambia una jengo, wewe Sema ndiyo, watatumwa wakaguzi, kuliona jengo na ushauri watakupatia.
4. Watakwambia utoe vyeti vya wataamu wako photocopy 3 au 4 kila cheti. Daktari msimamizi, AMO au MD, clinical officer wawili, maabara wawili, nurse wa diploma mmoja, nurse assistance wawili,
5.Nimesikia siku hizi wanataka mkataba ya kazi baina ya hao niliowataja hapo juu na na wewe mwenye biashara.
6. Baada ya ukaguzi na nyaraka hizo kupitiwa ofisini ya DMO, watakupitishia nyaraka zako na utapatiwa copies tatu ya hizo nyaraka upeleke ofisi ya RMO copy moja na wizara ya afya copy moja, na copy nyingine utabaki nayo mwenyewe. Kumbuka ukirudishiwa nyaraka zako kwamba imepita ina maana wameridhika na jengo na pia wafanyakazi wako, kama kuna marekebisho utaambiwa Mapema kabla hazijapitishwa nyaraka.
7. Wizara ya afya watakaa kikao kupitia maombi yote walioomba, huwa wanakaa mara tatu au nne Kwa mwaka. Uzuri wake kule hakuna longo longo bodi ikikaa tu kibali unapewa tu. Hizo process Zote ni kama miezi 3-6. Certificate ikitoka utalipia wizarani.
8. Certificate ikitoka wizarani basi una process TIN na lesseni ya biashara.
9. Unaanza shughuli, ila hii shughuli ina changamoto nyingi na ukaguzi wa mara Kwa mara bila taarifa. Unatakiwa uwe smart katika utoaji huduma na kufuata miongozo ya nchi na wizara ya afya.
 
Ni DISPENSARY wala si DISPENCERY kama ulivoandika, andika collectly ili uonekane kuwa upo serious na kitu unachotarajia kufanya otherwise tutakuona na mzushi unayepima kina cha maji kwa kujifanya unataka kufungua DISPENSARY, makosa madogo kama hayo ndio ambayo yanaweza kukufanya ukampatia mtu dawa tofauti na ugonjwa anaoumwa, otherwise wish you all the best in your plans to open the DISPENCERY.
Mkuu umu kumbe kuna madokta
 
Habari wakuu,

Kuna swali limeulizwa Mara kadhaa na wadau katik huu uzi naomba mwenye uelewa atusaidie kujibu maana tupo wengi:

Kuanzisha Biashara ya Maabara ya Binadamu:

1. Mtaji wake kiasi gani?
2. Vifaa muhimu vinavyotakiwa na bei zake
3. Wafanyakazi wanaotakiwa na ujuzi wao
4. Muundo wa Jengo LA Maabara
5. Vibali na taratibu za kuanzisha
6. Changamoto na lolote muhimu la kujua juu ya hii biashara

Karibuni tusaidine, biashara hii bado ni fursa kubwa maeneo mengi sana kwani serikali pekee bado haijaweza.
Na je vp kuhusu laboratory ya kuanzia unatakiwa uwe na machine zipi?
 
Na je vp kuhusu laboratory ya kuanzia unatakiwa uwe na machine zipi?
Kwa zahanati, unatakiwa uwe na darubin (microscope) binocular ya umeme, centrifuge, slides kama50-100, hata oven ndogo, urine analysis machine, gluco plus, na mashine ya kupima Hb, PB machine at mbili, stretescope 2, Weighing scale.
 
Kwa zahanati, unatakiwa uwe na darubin (microscope) binocular ya umeme, centrifuge, slides kama50-100, hata oven ndogo, urine analysis machine, gluco plus, na mashine ya kupima Hb, PB machine at mbili, stretescope 2, Weighing scale.
naomba kama hutojali mawasiliano na wewe kwa msaada zaidi kama nitakwama sehemu na ushauri pia
 
Wadau nataka kuanzisha maabara ya kupima magonjwa huko bush, naomba kusaidiwa changamoto na faida katika hii biashara ya kutoa huduma kwa wananchi. Shukrani kwa msaada najua hapa JF hakuna lisilowezekana.
 
Kama uko eneo la Jiji nenda kwa Daktari wa Jiji, na kama uko eneo la Wilaya neda kwa ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya utapata maelezo ya mahitaji ya kufungua zahanati. Kadhalika kama unataka kufungua maabara, onana na msimamizi wa kitengo cha maabara katika hospitali ya Jiji au ya Wilaya utapewa maelekezo yote.
 
Naombeni ushauri ni jinsi gani ntamzuia ninayemwajiri asiniibie vifaa na fedha(kwa kutoandika vipimo vyote kwenye daftari)
 
Kuibiwa kupo tu, labda kupunguza asiibe parefu cha msingi kuwa karbu na mradi wako ikbid na ww uwe na ujuzi huo. Siku zote kumwachia mfanyakazi majukumu mazito ya mradi ni hatar sana.
 
Unaonekana mtu bahiri sana wewe aise, hakuna biashara ambayo unaweza ajiri mtu asikuibie, hata mlinzi mwenye lazima akuibie hata nguo iliyo chakaa.
 
Back
Top Bottom