Thomas Juma
Member
- Nov 9, 2010
- 88
- 17
Jana nikiwa katika ofisi yangu kama wakala wa vodacom m-pesa wilaya ya Kahama nimekumbwa na utapeli ambao mpaka sasa sijaelewa huu utapeli umekaa vipi.
Kuna bwana mmoja amefika kwa ajili ya kutoa pesa kwa kuwa cash ilikuwepo nikamruhusu atoe baada ya hapo nikasubiri voda wahakiki kuingia kwa pesa hiyo baada ya muda kweli msg ikaingia kwenye Simu yangu kuwa wamehakiki na float yangu imeongezeka na kuwa kiasi flani ambacho ni kweli kulingana na salio alilotoa huyo bwana + salio lililokuwepo kwenye float pia hata muda ambao huyo bwana ametoa hiyo pesa ni sawasawa kabisa.
Cha kushangaza baada ya muda kidogo mtu mwingine amekuja kuweka pesa nilipokuwa namuwekea pesa kwenye account yake ndipo nikaambiwa salio langu halitoshi, ikabidi nihakikishe kwa kuangalia salio maana uhakika wa kuwa salio lipo nilikuwanao kwa kuwa yule mtu alitoa na nikampatia cash,katika kuangalia salio nikakuta kweli halitoshi.
Nikawapigia vodacom kwa taarifa nilichoambiwa ni kwamba hiyo pesa hawaioni kwenye transaction nilizofanya na kwamba hapo tayar nimeshatapeliwa.
Sawa sasa kuna maswali kadhaa najiuliza;
1/ Hiyo msg ya kuhakiki mbona vodacom ndio waliotuma kuingia kwenye Simu yangu?
2/ kwanini salio langu limewiana ukiongeza na salio la huyu wanaedai kuwa ni tapeli?
3/ Hata muda aliotoa pesa mbona unaendana na muda halisi?
Sasa basi Kama ni utapeli nani kafanya ni vodacom wenyewe au ni mteja?
Na je nitawezaje kutambua tapeli kati ya mteja na vodacom ikiwa msg za uhakiki wanatuma vodacom wenyewe na mwisho wanadai hazionekani kwenye computer zao ili kuweza kumsaidia wakala.
Ndugu zangu naomba kujua nani kanitapeli na je nifanye?
Msaada plz.