Utajuaje kama magumu unayopitia ni mpango wa Mungu upite au kuna sehemu umejikwaa unatakiwa kusafisha?

NEBASA

Member
Feb 17, 2024
15
17
Ndugu zangu?

Kuna wakati napitia mitihani mingi sana hadi naanza kujiuliza kuna sehemu nilikosea natakiwa kurekebisha au Mungu kaamua kunipa hiki kikombe nikinywe?

Swali gumu ni kwamba nitajuaje kama ni mitihani ya kawaida ya Mungu au ni mabalaa na mikosi imetengenezwa na wanadamu maana kuna wakati tunazungukwa na maadui ambao hata hatuwajui na je kama Mungu kaamua iwe hivo natakiwa kufanyaje na kama kuna vibweka nafanyiwa natakiwa kufanyaje?

Maana sio kawaida kila mchongo ukijaribu unapaa kila ukigusa hiki hakikai inafika wakati hata sh.100 ya kununulia maji ya kuoga inakosekana na upo aridhi ya ugenini ehee mora
 
Hakuna mipango ya Mungu mkuu, ni changamoto za maishani tu kila mtu anapitia kwa upande wake!
Hebu fikiria upate ajali uvunjike miguu yote halafu eti ni mipango ya Mungu, huyo Mungu mbona ni katili sana?
 
Hakuna mipango ya Mungu mkuu, ni changamoto za maishani tu kila mtu anapitia kwa upande wake!
Hebu fikiria upate ajali uvunjike miguu yote halafu eti ni mipango ya Mungu, huyo Mungu mbona ni katili sana?
Kwa mantiki hyo bac kuna vita zinapigwa muda mwingine bila hata sisi wenyewe kujua kama tunashiriki kwenye hizo vita maana unakuta hali unayopitia sio ya kawaida kabisa
 
Sio kila unachokikosa kilikuwa kizuri kwako mungu anakujua zaidi ya unavyojijua.
 
Hakuna mpango wa Mungu.

Imagine mtoto mchanga anazaliwa na virusi vya HIV na bado tuseme mpango wa Mungu?
 
Ulipata tabu,unapata tabu na utapata tabu
Mpaka pale kifo kitakapo kupumnzisha and the rest ni kijifariji tu
 
Mkuu, changamoto na yote unayopitia visikupotezee imani yako kwa Mungu. Yeye ndiye atakayekuvusha katika hayo.

Ukiamini na kumtumainia yeye, utashinda.
 
Back
Top Bottom