Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,921
- 36,784
Mambo vipi wazee!
Aisee duniani kuna mambo sana.
Ukienda gende yenyewe original kutafuta utajiri hakika utaupata endapo tu utazingatia masharti yao.
Sharti lao kuu uwe na biashara, hili sharti halihitaji biashara kubwa. Hata biashara ya kuuza nyanya chungu poa tu, hata kuuza mishikaki ya mia mia poa tu.
Jamaa watakupa pesa either ya noti au sarafu ingawa sarafu ndio kipaumbele chao zaidi. Ile pesa utaambiwa kaiweke kwenye mkoba au chombo unachotunzia fedha za mauzo.
Jioni ukipega hesabu utakuta imeji double mara kadhaa.
Kuhusu gharama ya ndagu jamaa kwa ufupi ni Kama wanatoa bure vile maana mara nyingi wanasema utarudi kushukuru wazee ukifanikiwa.
Hapo ndipo utajiri unakujia.
Nitatoa mifano ya watu 4 ninaowafahamu walioshindwa masharti kabla au baada ya utajiri:
1. Huyu jamaa alipewa sharti la kupeleka sh. Mia moja ya sarafu kila mwaka wakati wa kiangazi. Aliweza kupeleka misimu miwili tu akadharau. Aliishia kuwa fukara.
2. Huyu jamaa alipewa sharti la kupeleka sindano ya mkono moja kila mwaka wakati wa kiangazi alipekeka mara moja tu akaona ni ujinga, atoke na gari Iringa mpaka Liwale ngende kupeleka sindano ya sh. Hamsini huku anatumia mafuta ya laki 3 . Sasa ni fukara anaomba mpaka sigara.
3. Alipewa sharti la kutokusalimiana au kupeana mkono na mtu yeyote kutoka Liwale Lindi mpaka Dar. Akaona simple. Nakuambia huyu alichemka vibaya. Akarudi kwa bibi akabadilishiwa sharti. Akatajirika ila mwishowe alichemka sharti la pili la kutokuchepuka. Unaambiwa baada ya kuwa na mipesa mastaa wa Bongo warembo unaowafahamu walimzonga kila kona akachepuka nao wawili watatu akafilisika.
4. Huyu alipewa sharti la kusafiri kwa mguu au baiskeli tu. Akafanikiwa sana mpaka alijenga hoteli za kisasa. Akiangalia meneja wa hotel zake zote mbili wana magari yeye ni mwendo wa baiskeli tu. Akanunua magari ya kutembelea. Akafulia.
Visa ni vingi takuja kusimulia vingine.