Utajili! Utajili! Huo maradufu

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Habari wanajamii!

Nawatafuta watu wenye mitaji ya kuanzia kama milioni 3 hivi tufanye nao biashara.

Biashara yenyewe iko namna hii ni kuzalisha umeme kwa kutumia machine ya kusaga itakayobadilishwa na kuwa ya kufua umeme kwa kufungiwa moter, nipo eneo moja Mkoani mwanza pembezoni mwa mji ni sehemu iliyo na watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa wamekuja kutafuta eneo hili, kwa bahati mbaya eneo hili hakuna umeme usambazwao na shirika letu la umeme la Tanesco bado haujafika, ingawa kuna mtu mmoja yupo sehemu hii ikijaribu kutoa huduma hii maeneo haya kwa kutumia machine ya kusaga yenye piston moja ambayo imeelemewa mzigo kwa mahitaji ya wateja kuwa makubwa hivyo kufanya watu kuendelea kukaa gizani

hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku

2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku

3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku

3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu

4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo

kwa kifupi mahitaji bado ni mengi mno na hudumu iliyopo sasa inalegalega sana kama utalizika na maono yangu ya kufanya nawe mfanyabiasha biashara hii katika eneo ili tafadhari tuwasiliane kwa kuniPM
 
Mchanganuo gani huonyeshi gharama za uendeshaji?

Vipi kuhusu idadi ya watu kwa wastani au idadi ya households.

Unatafuta watu wenye 3m wangapi?

Ngosha jipange uzuri halafu urejee
 
Idea nzuri Mwea. Nina ushauri kidogo na kwakuwa nimekaa vijijini kwa muda na gharama unazosema kidogo na mashaka nazo ingawa sitaki kukukatisha tamaa. Bulb moja kwa sh. 500 ni bei juu kidogo na wastani wa matumizi ya umeme vijijini ni kama sh. 15,000 kwa bulb, TV, kucharge simu. Angalia hili kwanza, pili monitoring ya matumizi ni ngumu sana na wateja si waaminifu hivyo utakuta unaungaza motor kila week na tracing nani anatumia umeme zaidi ni ngumu. Ninachokushauri, kuingia risk ya kuchukua 3m mfanye biashara inaweza kuwa na return nzuri lakini wakati mmepata wateja challenges zitaanza TRA na pili TANESCO watakuwa mgongoni. Nenda REA - Rural Electrification Agency, http://www.rea.go.tz utapata ideas nzuri za nishati mbadala na kutoa risk kwako na share holders; wewe ni mdau mzuri unaisaidia serikali kupeleka nishati vijijini au sehemu ambazo TANESCO hawajafika, na kwa sababu hiyo kuna mfuko wa fedha kwa ajili hiyo lakini kama unavyojua mambo ya serikali yetu lakini jaribu kwanza ikishindikana then endelea na plan yako ila uwe tayari na ku deal na madenni ya shareholders na kodi za nchi hii..unazalisha umeme vijijini unapigwa kodi juu..mtu anachukua Kilimanjaro Hotel halipi kodi 5 years...upo hapo
 
Wazo zuri sana, kwa kuwaongezea siku hizi pana meter za kupimia matumizi ya umeme madukani analogy sh 15000,digital shs 15000-45000 tegemea na size,

Pili nadhani hiyo yaweza kuwa viable idea tafuta mshauri mtaalamu akuandikie Business Plan ya kawaida sana isiyo na gharama kubwa hata kwa kiswahili, itakayoonyesha ukubwa, uwezo na mwenendo tarajiwa wa 1) soko 2)mapato/mauzo, 3) Gharama za uwekezaji 4) Gharama za uendeshaji 5)watu husika watumishi 6)Mtaji na upatikanaji wake 7) Changamoto na tishio RISKS n.k.

Tatu fikiria na vyanzo vingine visivyo tumia gharama kubwa kama mafuta diesel mfano zipo generator ndogo za kufua umeme kwa upepo, na pia solar panel vyote vinaweza kuchanganywa pamoja vikasaidiana bila shida kabisa, mfano siku upepo ni mwingi unazima ya mafuta, unatumia solar na windgenerator.

Naamini kwa namna hiyo na ukatangaza ni rahisi sana kumpata partiner au mkopo wa benk ukafanya mwenyewe.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri.
 
Idea nzuri Mwea. Nina ushauri kidogo na kwakuwa nimekaa vijijini kwa muda na gharama unazosema kidogo na mashaka nazo ingawa sitaki kukukatisha tamaa. Bulb moja kwa sh. 500 ni bei juu kidogo na wastani wa matumizi ya umeme vijijini ni kama sh. 15,000 kwa bulb, TV, kucharge simu. Angalia hili kwanza, pili monitoring ya matumizi ni ngumu sana na wateja si waaminifu hivyo utakuta unaungaza motor kila week na tracing nani anatumia umeme zaidi ni ngumu. Ninachokushauri, kuingia risk ya kuchukua 3m mfanye biashara inaweza kuwa na return nzuri lakini wakati mmepata wateja challenges zitaanza TRA na pili TANESCO watakuwa mgongoni. Nenda REA - Rural Electrification Agency, http://www.rea.go.tz utapata ideas nzuri za nishati mbadala na kutoa risk kwako na share holders; wewe ni mdau mzuri unaisaidia serikali kupeleka nishati vijijini au sehemu ambazo TANESCO hawajafika, na kwa sababu hiyo kuna mfuko wa fedha kwa ajili hiyo lakini kama unavyojua mambo ya serikali yetu lakini jaribu kwanza ikishindikana then endelea na plan yako ila uwe tayari na ku deal na madenni ya shareholders na kodi za nchi hii..unazalisha umeme vijijini unapigwa kodi juu..mtu anachukua Kilimanjaro Hotel halipi kodi 5 years...upo hapo

Huu ndio uzuri na mawazo tofauti ahsante.
 
Back
Top Bottom