Utafiti: Kahawa huongeza hamu ya wanawake kufanya mapenzi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,016
156,423
Imethibitika Kahawa huwaongezea wanawake ashki ya kujamiiana..!

Watafiti hivi sasa wanasema huenda wanaume wanaowategemea wanawake wanywe pombe kwanza ili iwe rahisi kwao kuwakubali, hawana haja ya kufanya hivyo. Hawana haja ya kufanya hivyo kwa sababu, imebainika kwamba, kahawa inafanya kazi bora zaidi kuliko pombe kwenye jambo hilo.

Imebainika kwamba, wanawake wanapokunywa kahawa wanapata ashki ya kufanya mapenzi kwa kiwango kikubwa. Kahawa na jamii nyingine zenye dawa ya caffeine, ikiwemo chai, cocoa, na vingine, vina athari hiyo.

Lakini kwa sasa kahawa ndiyo imefanyiwa majaribio. Ingawa utafiti huo haukufanywa kwa binadamu moja kwa moja, bali kwa panya, imeonesha kuwa, panya wa kike wanaathiriwa na kahawa kuhusiana na kujamiiana. Panya wa kike waliopewa kinywaji hicho, walionekana kufanya mapenzi na panya wa Kiume na kurejea tena kuomba kuendelea kwa kasi, ukilinganisha na wale ambao hawakuwa wamepewa kahawa.

Imeonesha kwamba, baada ya kunywa kahawa panya wa kike walikimbilia kwa panya wa kiume, siyo kutafuta ‘kampani,’ bali kutaka kujamiiana. Hata baada ya kujamiiana, waliendelea kukaa hapo na panya wa kiume, kama kwamba wakitaka tena. Wale ambao hawakupewa kahawa hawakuonesha kabisa haja hiyo.
F
Utafiti huo ambao umechapishwa kwenye jarida maarufu la pharmacology Biochemistry and Behavior, unaonesha kwamba, pamoja na kuwa panya hana mfumo wa moja kwa moja wa kujamiiana ambao unafanana na binadamu, lakini kuna kemikali za kujamiiana ambazo panya na binadamu wanashiriki sawa.

Fay Guarraci, kiongozi wa utafiti huo, alisema kuna uwezekano mkubwa, kahawa pia huwa inachochea hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.
Hata hivyo ametahadharishakwamba, wanawake na wanaume wasikurupuke kutumia kahawa kama ‘mkuyati,’ kwa sababu kiwango cha kahawa kina athari tofauti. Kwa mfano, kahawa ikiwa nyingi sana, haichochei hamu ya tendo la kujamiiana bali ikiwa ya wastani ndipo inapofanya kazi.

NB:-
Bandiko hili limekwapuliwa kutoka kwenye maktaba ya Mtambuzi.
 
mwaka? Maana akili yako asubuhi asubuhi inaelekezwa mikuyatini? Uko kwenye balahe?
Silly you... Unataka wote tuwaze sawa? Sisi sio hayawani ndio maana wewe hukugundua kila kitu. Gari unayotembelea hukuiunda wewe, nguo ulizovaa hukushona wewe. Chakula chako Cha asubuhi hukulima wewe, hata nywele hujinyoi wewe.
Grow up nigga, stop acting like a lunatic.
 
Umepanic nini sasa, mwanao barubaru naye awe anapost mautumbo kama yako humu, kwanza ataona hata aibu akigundua hii ID ni ya baba yake!

Nilikuwa nakutania tu bujibuji endeleza libeneke😁😁
Tuko pamoja sana!
 
Bujibuji hapanic, Wala sijawahi kupanic.
Tatizo lenu Watanzania mnadhani siasa ndio kila kitu.
Hata tukiwaulizeni maswali ya siasa hamna majibu yake.
Nilicho post Mimi is a scientific research, na kwa taarifa yako hii research imegharimu muda mrefu na fedha nyingi.
Tanzania hatuendelei kwasababu hatufanyi tafiti, hata tafiti zilizokwisha kufanyika tunazidharau
 
Na Wabongo kwa kupenda tafiti za kuhusu haya hatujambo,yaani katika tafiti zooote hii imeukuna mtima wangu.
Vipi hawakuzungumzia kwa wanaume kwamba caffeine iliyoko kwenye kahawa ni sawa na iliyoko kwenye tumbaku na inashusha zile maajabu za ile kitu kuumuka bila hamira?
 
Caffeine kwenye Kahawa inaenda kwenye digestion system na kufanya libido iwe aroused. Piga Kahawa uongeze blood flow kwenye mjeredi
 
Ngoja ninywe nikukimbilie

Back
Top Bottom