UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 wa Aprili 2018 umebaini 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani 2015.

Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016 na 71% mwaka 2017

pic10.PNG

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Wazee (71%) kwa kiwango kikubwa wanaukubali utendaji wa Rais, huku wenye umri wa miaka 18-29 (46%) wakiukubali kiasi.

Wanawake (57%) wanaukubali utendaji wa Rasi kuliko wanaume (53%) na wasio na elimu (58%) wanaukubali zaidi kuliko wenye elimu ya juu (47%)

pic11.PNG

Kukubalika Vijijini

Mwaka 2017, wananchi wa vijijini (72%) waliukubali zaidi utendaji wa Rais kuliko wale wanmijini (70%)

Takwimu hizi zinaonesha kukubalika kwa utendaji wake kumeshuka zaidi vijijini kutoka 72% hadi 52% ukilinganisha na mijini 70% hadi 59%

Je, hii inaashiria nini kwa uongozi wa Rais Magufuli?





UPDATES:
Dkt. Vicencia Shule kutoka UDSM

Pamoja na kwamba watu wanaogopa vurugu, bado wanawake wameonesha kuwa na uelewa sawa na wanaume kuhusu malengo ya Maandamano; hili limenifurahisha

Pia kukubalika kwa Rais kumeshuka na sasa naona Wananchi wanajua kipi kinatekelezeka na kipi ni propaganda

Lakini ningependa kujua wanawake hawamkubali kiasi gani sababu Rais anadhalilisha na haheshimu wanawake kwa kutishia Mashangazi

>>>Anaongeza Vicencia
Nadhani twende mbela zaidi badala ya kuzungumzia maandamano tu tuzungumziae pia makongamano kwa kuwa tumekuwa na nyoka wengi sana kwamba kile unachozungumza tu kinafikisha usalama hapo hapo

Nadhani ni vizuri tafiti zikatupeleka kwenye kuelewa ni namna gani wanaume watapambana....hapa wanaume mnajinyima huru wenu wenyewe imekuwa tabu, mlipokuwa mnatunyima sisi uhuru kutoka hata kitandani sasa mnakuja kutuomba sisi msaada tuwasaidie kwa mwanaume mwenzenu anayewanyima uhuru

Tunaenda kwenye vyombp vya habari tunaambiwa msiongee kitu fulani maana chombo chetu kitakuwa na matatizo. na nadhani tunavyoenda kwenye kampen kutakuja sheria mpya nadhani hata ka kupiga marufuku kukohoa

Tafsiri ya mwenezi ni kwamba kwa sasa kinachofanywa ni vya CCM halisi hivyo Mwinyi, Mkapa, Kikwete wale hawakuwa CCM halisi na mimi nafurahi kwa kuwa sasa makucha ya CCM halisi tunayaona

Mwenyekiti wa Tanganyika Law Society(TLS), Fatma Karume

Nafurahi sana kuwa wananchi wameikita DemokrasiaYetu katika Uhuru na si kupiga kura kama Chama Tawala kinavyotuaminisha

Pia UhuruWaKujieleza si tu jambo la wasomi bali ni la Watanzania wote

Serikali ijue kuwa wananchi hawaogopi kuandamana sababu ya vitisho vya "Kupigwa kama mbwa koko" bali kwa sababu hawataki kufanya vurugu. Kadri haki zao zitakavyokuwa zinakiukwa, ndivyo tamaa ya kuandamana itaongezeka

>>>Anaongeza Fatma
Watanzania wengi wanadhani uchochozi ni umbea umbea tu. Sasa serikali ikitaka kuvidhibiti vyama vya siasa mbada(Sio Upinzani), vianapoanza kuwapeleka mahakamani mwananchi anadhani kuwa wamefanya fitna

lakini kwa mujibu wa sheria uchochozi sio fitna bali ni uhaini.... kwa mujibu wa sheria maana yake ni unataka kusababissha watu wasimame na waiondoe serikali nje ya mujibu wa sheria. hivyo wanatumia neno uchochezi kuwachanganya wananchi

Wanatumia neno hilo makusudi ili wananchi waseme "oooh! Mbowe anametaka kutufitnisha na serikali' Mbowe kwa mujibu wa sheria anatakiwa kukufitnisha na serikali ili yeye apate dola. Na CCM nayo ikitoka lazima itafanya fitna.

Hivyo uchochezi sio fitna na msikubai kuambiwa na serikali kuwa fitna ni uchochezi fitna ni siasa tu kwenye siasa

Kitu muhimu ni hivi, angalia ukurasa wa 3 wa Muhtasari No. 48 na ukurasa wa 5; Asilimi 84 ya wananchi wanaelewa wanataka demokrasia. Mkumbuke hilo....kurasa wa 7, asilimi 78 ya wananchi wanataka Rais aheshimu sheria na Mahakama, asilimia 59 wanataka Bunge lihakikishe kuwa Rais anatoa taarifa mara kwa mara naman anvyotumia fedha za umma

So, Humphrey msidhani mtabunguza umaarufu kwa vyama mbadala huku nyini mkidhani mtakuwa sawa...msidhani mkiwabana vyama mbadala ni sawa ila nyie wenyewe mnajipiga risasi kwenye vidole na ile rate yenu ya Vijijini ina shuka

Sasa kama hamheshimu Rule of law mtabaki kushuka tu

Maria Sarungi

Nimeona ongezeko la watu ambao hawajui watapigia chama gani kura kwenye uchaguzi(undecided) hadi 30%. Itafika mahala hawa ndio watakaofanya maamuzi katika chaguzi nchini

Kukubalika kwa Rais kumeshuka sana na hili ni jambo la kuangaliwa sana na Chama Tawala. Hapo Twaweza hawajaonesha wahojiwa walikuwa na uoga kiasi gani lakini labda ingekuwa chini zaidi

>>>Anaongeza maneno Maria
Chama cha mapinduzi kimeoeleka kama chama cha ukombozi. Sasa muundo wa Kitanzania unaonyesha kuna mabaki ya chama kushika hatamu, wananchi wanenda kulalamika kwa katibu mwenezi wa chama kwa sababu kuna taitizo la chama kushika hatamu. Na hiyo Status Chama cha mapinduzi kimerithi hiyo

Nafurahi sana kusikia kuwa kuna mambo yanendelea katika vyuo vikuu na CCM kijiimarisha. Vyama vya upinzani visijiite tena vyama vya upinzani maana na wao wanaweza kushika dola na inaweza kuwa 2020.

Wasijiite Upinzani maana upinzani ni kupinga maendeleo

Poromoko ambalo lipo chinin karibu kabisa na wananchi(Poromoko la madiwani) lipo sawa na poromoko la hadhi ya juu kwa rais. Tulimsikia Spika anasema eti bunge litavunjwa....backbencher wale kwa tafiti hizi hawawezi kutishika kwa sasa babu kwani ukivunja bunge kuna sehemu kutakuwa sawa

Hofu kwa asilimia kubwa ni ya kudhania lakini mbayo pia inatokea kutokana na kuna kitu halisi kimetokea. Mfano ni Bwana Melo alipokamatwa na kuweka Polisi kwa siku 8, hiyo ni kwake au Fatmu ofisi zao zilipovamiwa na kupigwa mabomu

Nadhani turuhusu uhuru wa kujieleaza, mwananchi anapisimama na kusema hatupo huru na tunapigwa( alisema mwanasiasa mwenzanko, akimuangalia Poleple) hii ni dhana iliyojengeka

Watu wanaosema kuhusu uhuru, kwamba sijui, sawa hawa ni watu wenye dhana ya hofu kichwani. Mtoto akikumbia sijui kama unanipenda hapo ni anakuogopa

Maxence Melo Kutoka JamiiForums

Wananchi wamepoteza imani na wabunge bila kujali chama; ni 44% tu wanaonesha kuwa na imani na Wabunge wao. Wabunge wawe makini sana kwa sasa na vyama viangalie machaguo yao ya wagombea

Kwa mujibu wa Utafiti, CCM imebakiza makundi mawili ambayo yanawakubali ambayo ni Wazee wa miaka zaidi ya 50 na wasio na elimu hata ya msingi. Hii ina maana kuwa makundi hayo yakiwa 'manipulated' watapoteza ufuasi mkubwa

>>>Anaongeza Maxence
Nimeangalia hizi tafiti na kikubwa kingine nilichokiona hapa ni kwamba wakati Rais Magufuli anaingia madarakani Watu waliokuwa na hofu ya uchumi ni asilimia 34 na sasa ni asilimia 72. Sasa nawaza sijui hili linaashiria nini? Sijui

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji

Hivi sasa Watanzania wamevurugwa sababu wanashindwa kuweka link ya hisia zao au hali zao na maamuzi wanayofanya. Sababu huwezi kutoridhika na kiongozi wako lakini ukaendelea kumchagua huyo huyo

Sheria zinazozungumzia Uchochezi ni za kikoloni sababu ni mambo ya 'perception' tu ya mtu. Ni aibu kwa taifa kushughulika na mambo ya uchochezi katika zama hizi

>>>Anaongezea Mashinji
Tuna wanachama wengi sana sema vitisho ni vingi sana na hivyo watu wameogopa na kijificha maana chama cha CCM hakijaonyesha mpaka wake unaishia wapi na wa serikali unaanzia wapi

Kuchimba visima watu wanaweza kufanya wenyewe hivyo sio vitu vya kuongelea hapa. Na niwasihii wabunge wangu tu wasifanye hivyo

Sasa approval rate ya rais imeshuka, wazee na wasomi wengi hawaakitaki chama cha mapinduzi. "It's not about reading number it's about understanding them"

Watu wengi wanaokukubali ni wepi na yule mama ambaye hana hata redio, anaamka naenda dukani na amelima mchicha wake pale sasa hapa nasema hiki ndicho anachokijua. Sasa hii nchi imekuwa kupuuzana puuzana tu sasa unapuuza viongozi wa vyana na sasa unapuuza wananchi hatuweza kuishi hivi

Tuliwapa dhamana ya kuongoza nchi lakina hawajafanya hicho kitu ila vitisho 'Intimadation' sasa ccm wakafanyie kazi hili kwamba tumeavcha kujenga madaraja sasa tunajenga visima vya kuzamisha watu

Kwenye hizi tafiti kuna hoja ya kushuka kwa umaarufu wa wabunge na madiwani, wakati tunaukumbusha umma kwamba kuna u-dictator watu waliona sisi ni wasanii fulani tunatafuta kiki za kisisa.

lakini najua kilichotokea, alienda kwenye taasisi za umma alienda kwenye halmashauri akihakikisha ananyang'anya vyanzo vya mapato akaenda kwenye vyombo vya habari. Maana yake hapa yeye anapaki yeye.....akaliingilia bunge na kuhakikisha kuwa wale wabunge wanajenga hoja lazima tuwa-downseize. Bunge halina meno tena hata mwananchi akiulizwa huyu mbunge mtampigia kura, lazima aulize kwa lipi maana wabunge hawana kazi pale wanaongea na kupokea posho tu

Nadhani kwa sasa Mahakama ndio imebaki sasa akisha malizana na Mahakama nadhani itakuwa ni yeye dhidi ya wananchi wote. Hilisuala ya elimu liakuja wananchi wakiwa huru kwenda shule... tuanze kwanza na suala la uhuru wa sheria(demokrasi) mebgine yatakuja baadae

Katibu Mwenezi na itikadi wa CCM, Humphrey Polepole
Tafiti zinapaswa kuakisi hali halisi ya Watanzania. Kuna mambo mengi ya kufanyia utafiti katika nchi kama rushwa, ukosefu wa ajira n.k. Tafiti hizi ni nzuri lakini hazileti mkate mezani kwa watu wetu

Mikutano ya hadhara haijapigwa marufuku bali imewekewa utaratibu maalum. Tunataka viongozi mf. Wabunge wasivurugwe katika maeneo yao ya Uongozi. Wanachama hawaongezwi kwa mikutano bali mbinu za nyumba kwa nyumba hata kitanda kwa kitanda

Nimekwenda majimbo kadhaa ya wapinzani kama kwa Mbowe, Mbatia, Zitto n.k na hawafanyi mikutano ya hadhara huko. Na hawa ndio wako mstari wa mbele kusema mikutano imekatazwa au inazuiwa. Lakini mikutano ya vyama Temeke, Ilala inafanyika

Mnawalazimisha watu kuongelea maandamano lakini watu hawataki hayo mambo. Kwenye utafiti kila mkiwatajia maandamano wanazungumzia kufanya maamuzi na wengi wamekataa kushiriki

Sishangai kukubalika kwa Rais kushuka kwani hata ndoani kuna "honeymoon phase". Maendeleo si kitu cha kimiujiza. Tunashughulikia maji, umeme, kilimo, miundimbinu n.k na mambo yako jikoni. Wasio na elimu ni wanyonge wanaziona juhudi zetu

>>>Anaongezea Humprey Polepole
Jambo la kwanza mimi naomba sisi wote ni wananchi na viongozi, tunapozungumza kuhusu uhuru naomba nisema kwa unyeyekevu sana Uhuru dunia kote mpaka mbinguni hakuna uhuru holela, uhuru una pande mbili; Ipo haki yako na upo wajibu

Uhuru pia umewekwa mipaka kuhusiana na sehemu husika na ndio maana hapa Tanzania tunasema ukitaka kuolewa uolewa na mtu wa jinsi tofauti na yko lakini nchi nyingine wanaruhusu jinsia sana. hakuna uhuru holela, uhuru unautaratibu

Mbowe ametoa tuhumu kwamba serikali inajinja na kuu watu naomba akatoe taarifa Polisi maana hapa wote ni mashahidi

Jambo la pili: Mimi kama msemaji wa chama cha mapinduzi, lengo letu ni kufika kwenye uchimi wa kati ambao umeongezewa maarifa kutoka kwa ngazi ya shule ya msingi mpaka chuo kikuu na ndicho tunachokifanya hapa

Hatuna vyanzo ambavyo ni sustanable, tunataka kutengeneza vyanzo hivyo Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na Kikwete hakuweza lakini Magufuli ameweza na ndio maana tumeleta Stiglers Gorge

Mimi nilishiriki kuandika Katiba na nakumbuka wananchi walisema wabunge lazima wakae majimboni na Madiwanai wake katani. Hakuna mbinu nyingine ya kuhudumia watu "Be there, live there". Fact ya tatu sasa Mbowe hakai Hai, Zitto hakai Kigoma, Mbatia hakai Vunjo

Kwa nini vijana wameonyesha Wanakubali chama cha mapinduzi, vijana wanatumia akili sana na wanaangalia hali ya kutabirika na wazee wanatumia hekima. Msingi wa akili ya uamuzi. Na katika chama ambacho kinatabirika mambo yake ni CCM.

Sisi tumekuwa wabunifu kwenye mbinu zetu, mikutano ninayofanya mimi ni mikutano ya ndani na si ya hadhara la pili mtu wa CCM akienda popote huko nchini Tanzania wananchini wanaona ameleta masuluhisho.....Watu wananisimamisha na kusema hapa kuna tatizo...Mimi kama kiongozi nwa chama naweza kumuita Waziri Jafo na kumpa maelekezo.

Tumeenda Kigoma watu analalamika nikasuluhisha. Na yule bwana atafute kazi nyingie

Jenerali Ulimwengu

Humphrey Polepole amezungumzia kuwa kitu cha muhimu ni mkate mezani lakini Binadamu hataishi kwa mkate tu. Bila matumaini ya kiroho mtu bado hajaendelea; "development cannot be inflicted". Usiseme tunajenga barabara. Barabara za kwenda wapi?

Ifike wakati mtu awe na amani kuwa hata akiwa anafurahia mkate wake hakupewa tu kama sadaka au msaada bali amepewa Uhuru kujitafutia kipato chake kwa jasho lake. Maswali ya amani na uhuru wa wananchi hayapaswi kujibiwa kwa hoja za mkate

Karibu theluthi ya watu wa Tanzania wame-disengage kwenye siasa; yaani hawataki kuwa upande wowote na wanaongezeka. Unapozuia siasa za wazi unakaribisha siasa za kificho na makundi ya kigaidi kama Alqaeda

>>>Anaongeza Ulimwengu
Kwa kuwa Polepole ameshaonyesha kuwa anaushawishi mkubwa sana kwenye chama na serikali kama alivyosema hapa(sijui imekutokeaje hiyo) atusaidie kueleza wenzake kwenye chama kuwa kuna perception ya uoga huku

Hivyo tuchukulie hali ya hofu ni ya kweli, Ben Sanane hajulikana yupo wapi, Azory Gwada hajulikani alipo...sio kwamba wamechukuliwa na serikali hatujasema ni nani. Isije kuwa kama ile CAG anasimamishwa na kusema eti kuna Trilioni 1.5 zimepotea? "Aaaha hatujasema imepotea ila hazijulikani zilipo"

Mimi juzi nilipooona maaskofu aliposiamama juzi na kuongea na si maaskofu uchwara ila maaskofu kabisa mimi niidhani viongozi wenye akili timamu walitakiwa wajiulize haya yanatoka wapi?

Wale hamuwezi kuwatisha wale, wale sio CHADEMA wala ACT hawatishiki hawa mimi nilidhani mngekaa nao chini na kuhoji haya yanatoka wapi. Ili mafanyie kazi

Maendeleo yote ni sisi bila siasa jamii inakuwa jamii mfu, wakati wa uchaguzi lazima kuwe na siasa baada ya uchaguzi lazima kuwe na siasa. Sio kufanya kama vile eti Mkulima amevuna unamwambia asilime tena...mwache alime aasipopata matunda ataacha mwenyewe

Siwezi kumpinga rais Magufuli kwa kupinga unyonyaji unaoendelea ila tusisahau uongzi uliopita lzimauulizwe waliachaje unyonyaji ule uundelee kwa kwenye madini na sehemu nyingine....wakubalini na wale wanaosema na kuonyesha kuwa tunaibiwa kama akina LIssu walivyosema kwa Mkapa. Kwa nini leo hamwaoni kama ni watetezi wa nchi lakini leo wanapigwa risasi(sijui nani kampiga risasi) wanaonewa

Yeyote anayeweka mazuio kwa wananchi kutoa maoni yao kwa mambo mema anayowatenda basi hatendi mambo mema...turuhusu kukosolewa tujenge haki ya kukosoana. Kama mmezoea kuziba midomo ya watu hapa nyumbani huko nje mnaenda kubishana na ku-negotiate vipi ikiwa hamna uwezo toka nyumbani?

Ado Shaibu kutoka ACT Wazalendo

Napenda kwanza kusema tu Magufuli ndio rais ambaye ni 'Unpopular' kuliko Marais wote, kwa mujibu wa tafiti hizi za Twaweza Mkapa alianza na asilimia 93 na akaondoka na 90, Kikwete asilimia zilipungua kidogo sana ila sasa Magufuli ameanza na 96% kwa sasa yupo 55%

Sasa hili linatokana na Magufuli kutengeneza ugomvi na Wakulima, Wavuvi, Mashangazi, Wafanyakazi na wananchi wote kwa ujumla

Anachokifanya Magufuli ni sawa na kucheza mpira halafu umewafunga kamba wapinzani sasa anacheza mwenyewe maana hakuna uhuru wa vyombo ya habari, vyama vya siasa havipo huru. Je, angeachia huru vitu hivi ingekuwaje?

Mimi nasema Rais Magufuli hizo asilimia zilitakiwa zifike 20
 
Bawacha hawataki kabisa kusikia....hiii hahahaha
 
Utafiti wa Sauti za Wananchi, Awamu ya 27 wa Aprili 2018 umebaini 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani 2015.

Kukubalika huku kumepungua kutoka 96% mwaka 2016 na 71% mwaka 2017

View attachment 802964

Kiwango cha kukubalika kwa Rais kimeshuka kutoka kwenye rekodi ya juu kuwahi kuwekwa na Rais wa Tanzania mpaka rekodi ya chini tangu takwimu hizi zianze kukusanywa mwaka 2001.

Wazee (71%) kwa kiwango kikubwa wanaukubali utendaji wa Rais, huku wenye umri wa miaka 18-29 (46%) wakiukubali kiasi.

Wanawake (57%) wanaukubali utendaji wa Rasi kuliko wanaume (53%) na wasio na elimu (58%) wanaukubali zaidi kuliko wenye elimu ya juu (47%)

View attachment 802965

Kukubalika Vijijini

Mwaka 2017, wananchi wa vijijini (72%) waliukubali zaidi utendaji wa Rais kuliko wale wanmijini (70%)

Takwimu hizi zinaonesha kukubalika kwa utendaji wake kumeshuka zaidi vijijini kutoka 72% hadi 52% ukilinganisha na mijini 70% hadi 59%

Je, hii inaashiria nini kwa uongozi wa Rais Magufuli?


Mod One Mod Two Moderator futeni huu uzi maana hauna ukweli wowote. Ni kipande tu mtu kakaa na kukitengeneza maana hakuna pahala huu utafiti ulipofafanua njia waliyotumia kufanya utafiti, hakuna validity wala reliability ya variable/data zao. Huu ni upotoshaji mkubwa sana, futeni haraka sana!
 
Back
Top Bottom