Utabiri:Makato ya HESLB ya asilimia 15 kuongeza makosa ya mtandao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,062
144,497
Hivi sasa watu/watumishi wako aware kuwa wataanza kukatwa asilimia 15 ya mishahara yao badala ya asilimi 8 ya awali kwa ajili ya kulipia deni la Bodi ya Mikopo.

Kwa wale ambao walikuwa hawajaanza kukatwa nao wataanza kukatwa asilimia 15 ya basi salary.

Ukweli ni kwamba,japo hivi sasa watu wako aware ila bado hawajaanza ku-feel pain ya makato mapya ambayo yatakuwa ni almost mara mbili ya makato ya sasa kwa wale ambao walishaanza kukatwa na makato mapya ya asilimia 15 ya basic salary kwa wale ambao walikuwa hawajaanza kukatwa.

Sasa sipati picha mtu ana madeni kibao ya mabenki, kamshahara kenyewe kadogo alafu anakwenda benki mwisho wa mwezi anakuta amekatwa asilimia 15 ya mshara huku mtu huyo ana access na mitandao kama huu wa JamiiForums na mengineyo hiyo hasira yake sijui kama haitaishiai mitandaoni.

Ili kuepusha haya,ilibidi watu waandaliwe kisaikolojia kupokea mabadiliko haya vinginevyo hatua hii inaweza kuleta madhara makubwa sana kwa watu hasa pale maumivu yatakapoonza.

Tusubiri.
 
Back
Top Bottom