Usomi wako usitutese bali utusaidie kutatua changamoto zetu

Guluma

Member
Jan 7, 2022
98
150
Nimemsikiliza vizuri Katibu mwenezi wetu wa CCM. Comred Paul Makonda akiwajibu washambulizi wake kuwa usomi wao usitumike kututesa bali utusaidie kutatua changamoto zetu za kila siku. Kauli hii imenifanya kujua kwamba kweli Makonda anajitambua.

Kwanini wasomi wetu wanajiona wao ni Watanzania wa daraja la kwanza? Kwamba wanastahili kupata unafuu kuliko Watanzania wengine kwa kila kitu? Kwanini hawafikirii kwamba elimu walizo nazo ni kwa ajili ya kutatua changamoto za Watanzania?

Najiuliza sana wanaomsema makonda kwamba anakosea kuwasikiliza wananchi, sijui wao ni Watanzania wa wapi? Sidhani kama kweli nia yao ni kulisaidia hili taifa.

Namtia moyo makonda, endelea na clinic zako kwa wananchi, usiache. Msaidie Mh Rais wetu kutatua kero za wananchi. Hata ningepewa mimi fursa kama yako. Ningefanya zaidi ya wewe. Kupendwa na wananchi ndio mtaji mkubwa kwenye siasa. Nakwambia mimi nikipewa fursa, hakika nitafanya zaidi ya wewe. Bila kupepesa macho, wafanyie kazi wananchi ipo siku watakulipa.

Ni mimi. Comredi M. Baraka. 0685292038. Ifakara mji. Morogoro.
 
Nimemsikiliza vizuri Katibu mwenezi wetu wa CCM. Comred paul makonda..akiwajibu washambulizi wake kuwa..Usomi wao usitumike kututesa bali utusaidie kutatua changamoto zetu za kila siku....kauli hii imenifanya kujua kwamba kweli makonda anajitambua.

Kwanini wasomi wetu wanajiona wao ni watanzania wa daraja la kwanza? Kwamba wanastahili kupata unafuu kuliko watanzania wengine kwa kila kitu?... kwanini hawafikirii kwamba Elimu walizo nazo ni kwaajili ya kutatua changamoto za watanzania?....

Najiuliza sana wanaomsema makonda kwamba anakosea kuwasikiliza wananchi, sijui wao ni watanzania wa wapi ?,, sidhani kama kweli nia yao ni kulisaidia hili taifa.

Namtia moyo makonda, endelea na clinic zako kwa wananchi...usiache. Msaidie mh Rais wetu kutatua kero za wananchi. Hata ningepewa mimi Fursa kama yako...ningefanya zaidi ya wewe...kupendwa na wananchi ndio mtaji mkubwa kwenye siasa...nakwambia mimi nikipewa fursa...hakika nitafanya zaidi ya wewe...bila kupepesa macho, wafanyie kazi wananchi ipo siku watakulipa

Hakika
 
naunga mkono hoja 100%
 
Na wanaojiita ni wasomi ndio wametufikisha hapa!

Usomi usiozingatia kutatua kero zetu ni upumbufu
 
Nimemsikiliza vizuri Katibu mwenezi wetu wa CCM. Comred Paul Makonda akiwajibu washambulizi wake kuwa usomi wao usitumike kututesa bali utusaidie kutatua changamoto zetu za kila siku. Kauli hii imenifanya kujua kwamba kweli Makonda anajitambua.

Kwanini wasomi wetu wanajiona wao ni Watanzania wa daraja la kwanza? Kwamba wanastahili kupata unafuu kuliko Watanzania wengine kwa kila kitu? Kwanini hawafikirii kwamba elimu walizo nazo ni kwa ajili ya kutatua changamoto za Watanzania?

Najiuliza sana wanaomsema makonda kwamba anakosea kuwasikiliza wananchi, sijui wao ni Watanzania wa wapi? Sidhani kama kweli nia yao ni kulisaidia hili taifa.

Namtia moyo makonda, endelea na clinic zako kwa wananchi, usiache. Msaidie Mh Rais wetu kutatua kero za wananchi. Hata ningepewa mimi fursa kama yako. Ningefanya zaidi ya wewe. Kupendwa na wananchi ndio mtaji mkubwa kwenye siasa. Nakwambia mimi nikipewa fursa, hakika nitafanya zaidi ya wewe. Bila kupepesa macho, wafanyie kazi wananchi ipo siku watakulipa.

Ni mimi. Comredi M. Baraka. 0685292038. Ifakara mji. Morogoro.

Kusikiliza bila ya kuwa ni mifumo ya utatuzi, inakusaidia nini, zaidi ya kujifariji umepata mahali pa kupigia kelele?

Kuna mdau humu aliuliza, tangu watu waanze usaa wa kupiga kelele kwenye mikutano ya huyu msanii mwovu, ni matatizo gani yametatuliwa? Mpaka sasa hakuna hata 1, bado kuna mwenye akili atakwenda kueleza matatizo yake kwa huyu mwovu asiye na uwezo wa kutatua tatizo lolote?

Huyu bwana ni muuaji, jambazi wa kuteka watu na kuwapoteza, usanii wake kupitia mikutano hautamwondolea uovu wake mpaka siku ile atakapohukumiwa sawa na uovu wake.
 
Na wanaojiita ni wasomi ndio wametufikisha hapa!

Usomi usiozingatia kutatua kero zetu ni upumbufu

Kuna uwongo na ukweli pia.

Jiulize, kwa nini msomi wa Tanzania aende akafanye kazi Australia, UK, US, Ghana, UN apate sifa tele kwa utaalam na utendaji mzuri wa kazi, lakini alipokuwa Tanzania hakuwa na mchango wowote wa maana?

Tatizo kubwa lipo kwenye mifumo ya utawala. Watawala ndiyo hovyo kabisa. Ndio wanaofanya michango ya watanzania wote kwenye uchumi wa nchi isionekane. Kipimo kidogo kipo kwente taasisi zinazosimamiwa na Setikali. Utalinganisha TTCL na Vodacom, Tigo, Airtel au Halotel? Kwa nini TBL chini ya Serikali, wateja ilikuwa mpaka wanaohonga ili wapate crate ya bia, lakini leo wateja wanabembelezwa?

Hata huu upumbavu unaoendelea kwenye umeme, ingekuwa ni sekta binafsi, watu wangekuwa wanabembelezwa kutumia umeme mwingi, lakini chini ya hawa wasiojitambua, mambo yapo kama yalivyo, na yataendelea kuwa kama yalivyo. Ni nini chema Serikali iliwahi kukisimamia kikawa na ufanisi? Msomi anayefanye kazi chini ya mifumo ya watawala wasiojua kitu, unadhani ataweza kutatua changamoto za jamii?

Fikiria wakati wa Fastjet, hata maskini wa kawaida aliweza kusafiri kwa ndege, leo ATCL chini ya Serikali, maskini anaweza kupanda ndege? Serikali ndiyo leading failure institution leading every entity to failure.
 
Back
Top Bottom