Usingizi

Richbest

Senior Member
May 23, 2011
101
24
Habar za jioni wapendwa! Naomba ushaur wenu ninasinzia mchana darasani sana alafu usiku saa 4 nikipanda kitandan sipati usingizi hadi saa sita.je nifanye nini ili niwahi kupata usingizi usiku na mchana nisisinzie? Nawasilisha!
 
"Akili nzuri hupatikana kwa siha nzuri". Usingizi ni moja katika jambo la ibada, na kila ibada ina muda wake maalum kwa vile usingizi ni ibada bila shaka una muda wake maalum wa kuitekeleza ibada hii. Wanasayansi wamependezesha kuwa mtu alale masaa 8. Pia ni uzuri kulala mwanzo wa usiku (yaani baada ya isha) na ukaamka nusu ya usiku na kufanya ibada.

Kutopata usingizi husababisha wazimu (sio kukesha siku moja kwa wale wenye tabia ya kukosa usingizi siku zote). Kukesha kunaweza kumkondesha mtu na hudhurika ubongo.

YENYE KULETA USINGIZI:

1. Miongoni mwa vinvyosababisha usingizi ni mafuta ya tango, hufaa sana kwa wale wenye usingizi mchache wajipake mafuta hayo.

2. Vilevile mafuta ya busanji yanasaidia kuleta usingizi, pia ukitia miguu katika maji ya dafidafi (warm water).

3. Pia kunusa manemane na kunywa maji yaliorowekwa manemane.

4. Kunusa zafarani na tufaha (apple) na pia maji ya zafarani ukayatia kichwani husaidia kuleta usingizi.

5. Kunya maziwa huleta usingizi

6. Asali safi ya nyuki kunywa kabla kulala kwa saa huleta usingizi.
 
Back
Top Bottom