Usimuamini sana mtoto wa kike, kwenye mahusiano kuwa na kiasi

Heavy Weight

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
888
875
Habari zenu ndugu zangu wana JF, hivi karibuni kumekua na matukio kadhaa ya watu kujiua kutokana na mikasa ya kimapenzi, hali iliyopelekea hata juzi kati baadhi ya askari polisi kujitoa roho kisa mapenzi. Au kisa cha msanii Muna na wanaume zake na mgogoro wa nani baba wa mtoto.

Katika mambo ambayo hutakiwi kufanya ni kumuamini mwanamke kwa 100% kua ni wako pekeyako. Hawa watu akili zao wanazijua wenyewe. Bora uchelewe kuamini afu baadae ukaja kujua ni chaguo sahihi kuliko ukaweka uaminifu wako wote mwisho wa siku ukaja kujua hakua mtu sahihi. UTAPATA TABU SANA.

Mimi nilikua na demu wangu. Mwanzo tulikua hot mapenzi yenye shamra shamra kwa siku hata tukiwa bize vipi lazima tutafutane hata kwa dakika kadhaa kujuliana hali. Ikishindikana kuonana basi hata kwa simu.

Tulikua na uwezo wa kuchati mda mwingi kama tukiwa free, na usiku kwa maneno fulani fulani ili kupandishana genye. Ili tukikutana kila mtu awe na hamu na mwenzie. Kumwambia naitamani papuchi yako niichezee ilikua kawaida hata yeye akawa ananambia anaitamani duduwasha ikamkune panapomuwasha. Maneno hayo na mengine mengi tuliyatumia ili tu kunogesha manjonjo kwenye suala la mapenzi. Tuliendelea kwa muda ilifika kipindi wakati wote tunatamani tuwe pamoja.

Mambo yalikua ivyo hadi pale me nilipoenda mkoa mwingine kwa shughuli fulani fulani. Basi mawasiliano yakaendelea japo yalianza kupunguza kasi.
Kuna wakati nikawa nikipiga simu hapokei, nikituma ujumbe mfupi anajibu kwa kuchelewa au hajibu kabisa. Sikutilia maanani sana japo haikua kawaida yake nikahisi itakua anakua katingwa na kazi.

Japo nilijua hawezi kua bize kiasi icho cha kushindwa kujibu message au kupokea simu. Ila si unajua mapenzi upofu, ukipenda mda mwingine makosa au mambo ambayo yanaenda tofauti unayapotezea, Ili tu uendelee kuwa na unayempenda.

Mawasiliano ya kusuasua yakaendelea ikafikia hatua siku nyingine hanitafuti kabisa. Ila kwangu haikua kesi niliendelea kumtafuta kwa bidii ile ile. Nilivyoona respond yake ni ndogo nikaanza kukata tamaa nikijua labda huyu mtu kanichoka so inabidi na mimi nijiongeze.

Nikaanza kupunguza spidi ya kumtafuta, na hii ilichangiwa zaidi na yeye mwenyewe kwani hakutaka tena nimpigie simu usiku na hata nikipiga alikua anakata. Nilijaribu kumuuliza sababu akasema anawaogopa wazazi wake kwani hawapendi kumuona akiongea na simu usiku kwakua bado alikua anaishi kwao.

Nikajilazimisha kuamini japo nilikua na mashaka na sababu aliyonipa. Usiku ninao ongelea hapa sio usiku wa manane bali kuanzia saa mbili usiku sitakiwi kupiga simu. Nikamuuliza ivi huwezi hata kukaa chumbani kwako tukaongea, akaniamhia hawezi.

Kama upo kwenye mapenzi hii hali ya kutamani kuongea na mpenzi wako hata dakika kadhaa hua ni kawaida. Japo mimi sio muongeaji sana kwenye simu ila nilijitahidi niongee na mpenzi wangu kila nipatapo nafasi, hasa mida ya usiku kwani mchana shughuli nyingi labda text za kujuliana hali tu.

Kiukweli kwa mwanzo nilimuamini japo haikua kwa kiwango cha 100% ila ilikua asilimia nyingi.

Kuna siku mchana nilimpigia simu baada ya kua hajibu text zangu wala hanitafuti. Alipokea simu ila nilipata mshangao kwa jibu alilonipa, baada ya kupokea akanambia "nipo napiga story ntakutafuta baadae" Na hata iyo baadae hakunitafuta. Na hiyo ya kuniambia ntakutafuta baadae haikua mara ya kwanza ko nikawa najua kabisa akiniambia ivyo basi ndo imetoka. Hilo linaweza kua jibu la kawaida tu lakini inauma kama umeamua kumtafuta mtu afu kibaya zaidi mpenzi wako anakupa ilo jibu.

Nikawa namtumia meseji whatsapp anasoma lakini hajibu. Mda mwingine naona kabisa yupo online. Anasoma hajibu.

Ikabidi siku nyingine nimuulize ivi upo serious na mimi kweli au ndo tayari ushapata mwingine. Maana naona kabisa kama umenichoka. Yani kama hutaki kuendelea na mimi niambie tu kirahisi au tuma hata text moja tu kunijulisha kama hunitaki, kuliko kuniigizia kama unanipenda au kama bado tupo wote kumbe upo na mtu mwingine nikaja kudhalilika mchana kweupee.
Akanambia hamna me sina mtu mwingine ni wewe tu unanifikiria vibaya.
Binafsi nilikua natumia muda mwingi kwa huyu mtoto wa kike kwakua nilikua na yeye tu na sikutaka kua na branch nyingine.

Basi namimi nikazidi kupunguza kasi ya kumtafuta kwani nishaanza kujiandaa kisaikolojia kua huyu mtu hanitaki tena. Na kawaida ukiwa na mpenzi wako ghafla akapunguza speed ya kuwasiliana na wewe ujue tu kuna mwingine anamfanya awe bize.

Baada ya mimi kuwa kimya mda mrefu
{japo kuna kipindi nilimmiss mno kiasi cha kutamani kumtafuta, lakini nilijikaza kwani niliamini ningemtafuta majibu yake yangeniumiza zaidi kuliko nilivyoendelea kukaa kimya}
Alinitafuta na kunilalamikia mno kua nimebadilika sana skuizi simtafuti yani maneno kibao akaongea.

Nilishangaa kwakua yeye ndo alikua hanitafuti na nilishajaribu kumuuliza hapo nyuma tatizo ni nini hadi anakua kimya ivyo akawa ananijibu mambo mengi anatingwa na kazi.
Nikamjibu mbona wewe ndo upo kimya. Mara kibao me nakutafuta lakini wewe huoneshi response yoyote.

Ikabidi tuongee vizuri tuyamalize ili turudishe uhusiano wetu kama zamani
Japo tuliendelea lakini hatuakua kama mwanzo bado niliona kabisa huyu mtu hatupo sawa. Baada ya miezi kadhaa nilirudi alipokuepo japo saizi nilikua na mashaka kidogo sikumuamini asilimia nyingi sana naweza kusema nusu nusu.

Siku moja akaniachia simu yake ili niirekebishe kwani ilikua na shida moja ndogo tu ya setting.
Nikiwa naendelea kuirekebisha ye alikua ametoka kidogo. Ghafla ikaingia sms inauliza "uko wapi?" Kwenye simu yake. Sikuifungua kuisoma ila si unajua simu zetu izi message ikiingia kwanza inaonekana pale juu kwenye notification bar.
Iyo message haikunishtua ila kilichonishtua ni jina alilosave hiyo namba iliyotuma meseji. Jina alisave My Husband.

Nikauchuna kama sijaona kitu nikarekebisha tatizo lake afu nikailock, sababu ilikua na password na mimi nilikua siijui ila aliifungua alipotaka nimrekebishie.
Vile vile me sikua na tabia ya kukagua simu ya mtoto wa kike. Ko alipokuja akaniuliza tu ipo tayari nkamwambia ndiyo ipo tayari huku simu yake ikiwa mezani. Sikumuonesha kama nimeona chochote japo kichwani nikaanza kujiuliza vitu kibao.

Akili nyingine ikanijia kua nifanye mpango wa kuchukua simu yake ili niikague lakini nikaona isingekua uamuzi sahihi. Nikatuilia nitumie mbinu gani kujua mchezo wa huyu binti pendwa.

Nikapata wazo la kudukua (hack) whatsapp yake. Nikaona hii itakua njia sahihi kwakua kuna kipindi alikua anakua online lakini hajibu message zangu hivyo nikataka kujua hua anachati na nani na wanaongelea vitu gani kiasi kwamba anapuuzia txt zangu.

Kwa kutumia ujuzi mdogo tu wa kuchezea simu nikadownload application ya whats web kwenye simu yangu kisha nikaiacha isubiri siku nikikutana na mtoto wa kike nidukue simu yake. Nikaweka bando la data za kutosha kwenye simu ili mda wowote tukionana nitekeleze azma yangu.

Tukafanikiwa kuonana na mtoto wa kike safari hii tena akanambia simu yake imejaa nimsaidie kama naweza kuirekebisha. Nikamwambia usijali ngoja niirekebishe.

Mbuzi kafia kwa muuza supu. Hapo me nmefurahi kuwa ameniletea simu yake naidukua bila hata ye mwenyewe kujua. Nika connect wifi kutoka kwenye simu yangu kwakua ye hakua na bando la data (MBs)

Nikampa ela akachukue vocha ili aniachie space. Alipotoka tu me nika scan whatsapp code yake kutumia application ya whats web iliyokua kwenye simu yangu. Kiufupi nikafanikiwa kudukua whatsapp yake. Na message zake na taharifa zake zote za whatsapp nikawa naziona kwenye simu yangu.

Hapo ndipo nilipoyajua yote kumuhusu yeye na mwenendo wake wote.

NITAENDELEA........



MUENDELEZO.....

Muda mfupi baada ya kufanikiwa kudukua simu yake akawa amerejea na vocha. Nikarekebisha tatizo la simu yake na kuingiza ile vocha kisha nikamuungia data pekee bila dakika wala sms.

Nilifanya ivyo makusudi ili kama atakua na nia ya kuwasiliana na mtu ni lazima atumie whatsapp ambayo mimi nitakua naona kila kitu. Otherwise anunue vocha nyingine ajiunge kitu ambacho nilijua asingefanya kwa wakati ule.
Nilidisconnect wifi kisha nikampatia simu yake, huku data nikiiacha on.

Tuliendelea na maongezi meengi hadi baada ya muda fulani akaniambia "kuna sehemu nataka niende nimeagizwa ma mama ntakutafuta tena jioni" nikamwambia poa haina shida.

Baada ya yeye kuondoka pale huku nikiwa nimeacha data on kwenye simu yake, meseji zikaendelea kuingia. Nikaanza kufuatilia chati zake zote.
Kibaya zaidi alivyokua mjinga alikua hazifuti.

Nilishikwa na mshangao kidogo nilipokua nikiperuzi kwani kuna tetesi nilishawai kusikia kua kuna jamaa anatoka nae ila sikuwai kumuuliza. Na hata nilivyoona ile namba imeingia text imeseviwa my husband nikahisi labda ndo huyo jamaa ambae wanasema anatembea nae, na jamaa nilikua namjua kwa jina na sura na mda mwingine tulikua tunapiga nae story kimtindo japo hakua rafiki yangu. Nilivyokua nashuka na ile chati akili ikanijia kwamba niiangalie chati ya yule mtu aliyemsave my husband.

Nikasoma mwanzo hadi mwisho meseji zao, yes ni kweli alikua anatoka na huyu jamaa aliyemsave my husband na picha iliyokuwa display profile kwa jamaa ni nyingine yofauti na sura ya mtu ambae me namjua na nilikua nikiskia anatoka nae.

Nikaangalia chati za chini. Nikaona jina la yule jamaa ambaye ndio nilikua nasikia na nilihisi anatoka nae.
Meseji hazikudanganya ziliongea yote hadi siku ambayo demu anaenda geto kwa mchizi. Hadi alipofika anamuomba jamaa amfungulie ili aingie. Kilichoendelea humo jiongeze ukiwa kama mtu mzima.

Orodha ya wanaume kwa haraka haraka ni zaidi kama kumi ambao yupo nao kwenye uhusiano. Nisingeshangaa kama hao wanaume wangekua ndiyo wapo kwenye process za kumtongoza, ila ni kwamba hao wanaume tayari yupo nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Mwanzo nilipoona demu anaweza kua ananicheat kwa mtu mmoja niliumia. Nikahisi labda kuna vitu nilikua simridhishi hadi akaamua kutafta mtu mwingine.

Ila nilipojua tupo wengi kwenye foleni aisee sijui hata nilitoa wapi ile furaha hata yale maumivu ya kuumia roho yakapotea. Sikujua ni kwanini.

Ila nikawa naenjoy kuangalia anavyofanya na alivyokua akitupanga. Idadi ilikua ni kubwa mno.

Nikawa naangalia kila kitu anachofanya. Mwingine ambae hataki kuchati nae, anamwambia anaumwa huku anaendelea kuchat na mwanaume mwingine huyu anamwambia usiku mwema mwingine ndo anaanzisha nae story.

Hapo ndipo nilipojua kwanini meseji zangu za wasap zilikua zinasomwa lakini hazijibiwi.

Nilishangaa zaidi kuona akituma video za nusu uchi kwa mwanaume mwingine huku akikata viuno. Nilizidownload zile video kama ushahidi.

Nilishangaa kwakua hakuwahi kunitumia video kama zile wala picha za vile, na hata baada ya mambo kuanza kusuasua akawa hataki kabisa kusikia yale maneno ya kupandishana genye kama ilivyokua mwanzo kutoka kwangu.

Kuna rafiki zake wawili ndio walikia wanaiva sana sana nikaanza kusoma meseji za hao rafiki zake. Nikakuta rafiki yake mmoja alituma picha ya mwanaume kwa demu wangu. Iyo picha haikua mara ya kwanza kuiona.

First time iyo picha niliiona kwenye status ya demu wangu aliipost, nikamuuliza uyo nani akanambia "my bro mtoto wa mamkubwa" nikaguna akaniuliza "mbona unaguna?" sikujibu chochote.

Alivyotumiwa iyo picha demu wangu, akamwomba rafiki yake namba ya uyo mchizi, alafu akamtumia picha zake ili uyo rafiki yake amtumie mchizi na akamwambia "mtumie izo picha zangu kama na ye amenielewa tufanye mambo"

Yani kiufupi manzi alijirahisisha kwa jamaa na ndio huyo ambaye alimsave my husband.

Nikazirecord chati zote na namba zote ambazo alikua anawasiliana nazo, yani zile za wanaume ikiwa kama ushahidi.

Sasa nikaanza kufikiria niachane nae kwa style ipi. Je nimtumie huu ushahidi wote niliyouona? lakini nikajiuliza mara mbili mbili kwamba kudukua ni kosa kisheria vipi kama akiamua kunishtaki.

Nikaendelea nae bila kumwambia chochote wala kuonesha, dalili kwamba najua anayoyafanya.

Nilikua nikimtafutia sababu ya kuachana nae, ila asijue kwamba najua mambo yake yote hata yale ambayo hakutegemea kuwa ningeweza kuyajua.
Vile vile sijazoea kuacha na ma ex wangu kwa njia ya shari.

Yani me tukitibuana tu napiga, mute hadi tunapotezeana jumla.

Ila kwa huyu, ningetaka kusepa kimya kimya bado angeendelea kujua namtaka.

Nikawa namtafuta mda mwingi namjali, yani nikaanza kumuigizia kama ye ndo yeye kwangu. Kifupi tunasema unamtengeneza kisaikolojia au unamjaza ili ajue kweli umekufa.

Na me nilikua nachati nae kulingana na situation ninayoiona kwenye inbox yake.

Kuna siku jamaa mmoja nafahamiana nae akaniuliza "oya vipi uyo manzi naona upo nae karibu sana ni shemeji yetu nini"

Nilijua ananiuliza vile kwa kejeli, kwasababu alikua ni rafiki wa jamaa mmoja kati ya wanaotoka na yule demu.

Nikamjibu ndio. Jamaa akaguna mmh!! Afu akauliza oya ni kweli au unatania nkamwambia ni kweli. Akasema uyo demu mbona wa fulani kamtaja jamaa yake. Nikamwambia mbona nalijua ilo. Na sio uyo jamaa tu tupo wengine wengi nikamtajia orodha.

Ikabidi jamaa aniambie "oya mwanangu uyo demu kicheche achana nae, me nilikua najua kitambo ila sikutaka kukuambia mapema si unajua mapenzi"

Yani kiufupi washkaji walikua wanajua kuwa demu kiruka njia, ila walikua wanashindwa namna ya kuniface si unajua mapenzi. Unaweza kumwambia mtu hapo siyo afu nae akaenda kusemelea kwa baby wake mwisho wa siku unaonekana we mnafiki.

Jamaa akabaki ameduwaa tu kwamba nimewezaje kujua yote hayo afu still nipo kimya, yani kama sijui chochote. Nikamwambia tulia haya mambo hauhitaji kukurupuka.

Basi niliendelea na maigizo yangu ya kujidai sijui chochote.

Nikapata wazo la kumwambia face to face. Nikamtafuta kwenye simu nikamwambia kuna issue nataka niongee nae. Akashtuka ni issue gani iyo ambayo lazima tuonane ndio tuongee. Nikamwambia usijali ni yakawaida tu mpenzi wangu ila itapendeza kama tukionana ndio tuiongelee. Akaitikia poa.

Sasa ikawa kila tukipanga kuonana tunapishana mara sababu hii mara ile. Me nikaona uyu anazingua. Kuna siku tumepanga kuonana hakutokea. Nikampigia simu namwambia vipi mbona hujaja akanambia alikua na mambo mengi. Nikakata simu.

Niliona huyu tunapotezeana time tu hamna haja ya kuonana face to face. Nikamtumia sms fupi tu yenye ujumbe "its over between us"
Ilikua sio kawaida yake na wala hajawai kunipigia simu usiku alinipigia. Sikupokea, akaendelea tena na tena. Sikipokea.

Kesho yake asubuhi sana nayo haikua kawaida yake akapiga. Sikupokea. Akarudia na kurudia sikupokea nikaanza kukata.

Mida flani ya mchana akanitumia sms. "Sijakuelewa sababu gani imefanya umentumia meseji ya vile. Yani kunikosea ukosee wewe afu uwe wa kwanza kutaka tuachane. Kama hutaki kuwa na mimi si unifate uniambie kwa mdomo ntakuelewa"

Nikamjibu hamna sehemu ambayo me nimekosea. Na nilitafuta nafasi ya kukuambia kwa mdomo nikaikosa ndomana nimetuma meseji. Kiufupi mimi na wewe basi.
Akasema kwasababu ipi. Nikamwambia we jua tu ivyo me na wewe basi.

Akasema au nikufate ulipo uniambie sababu. Nikamjibu itakua vema. Akaniuliza nilipo nikamuelekeza akaja. Alikuja kwa ujasiri na kujiamini mno, hakujua kama me nipo serious akajua ni utani kwakua kuna wakati nilikua mtu wa utani sana.

Akanambia enhee sababu ni ipi mana hata salam hakutaka kuisikia. Nikamwangalia usoni nimemkazia macho afu nikamuuliza unataka kuijua sababu. Akasena ndio nikamjibu kwasababu wewe ni malaya. Na sio malaya tu yani we ni kahaba.

Punde ninavyomwambia hayo maneno hakuendelea tena kuniangalia usoni alikwepesha macho nikaona ujasiri aliokua nao umetoweka ghafla. Alikimbia na kuondoka pale nilipokuepo. Muda mfupi kidogo akanitumia meseji.
Unaweza kuniambia me malaya kivipi.
Nikamwambia njoo nikuambie kwa mdomo kama ulivyotaka. Akasema hawezi kuja. Akataka tuongee kwenye simu. Nikamwambia mauchafu yake anayoyafanya kwamba najua kila kitu kuhusu yeye.

Jambo lingine alilonishangaza ni jinsi alivyokua akibisha kua ye hayajui hayo mambo ninayoongelea. Akasema me namchekesha. Yani hadi nikashangaa anapata wapi ujasiri wa kubisha, nikataka kumtumia meseji zote za ushahidi ila nikaahirisha. Nikaamua kumpotezea kimya kimya.

Alinijibu kwa kejeli mno na akasema namfatilia kama nani kwani nimemlipia mali. Na akasema kwamba ndio umejua leo kua unatoka na kahaba. Nikasema ndio.

Maneno yake mengine akasema kua ye haumii hata kidogo yupo na amani tele. Nikamwambia sawa hata mimi lengo langu sio kukuumiza na ndio maana sikutaka kuyaongelea yote hayo.
Baada ya hapo akahamishia ligi kwenye status. Akaanza kunipiga madongo na vichambo. Nilichofanya nikafuta namba yake ili nisione chochote.

Baada ya wiki moja akaanza kunitumia meseji nikawa sijibu. Anatuma meseji eti hajaniona mda mrefu kanimiss na mengine kibao. Mara ananitumia meseji ananiambia ananipenda mara mimi ndo najua uhusiano umevunjika ila ye kwake halitambui hilo. Yani kiufupi ananisumbua.

Alivyoona kimya akaanza kumtumia mdogo wangu ili aniambie jinsi gani anaumia ila mimi siwezi kujirudi kwasababu nilishanawa mikono. Na nilishajiandaa kwamba huyu mtu mimi na yeye basi. Kwa ile team ya whatsapp angeweza hata kubeba world cup kwasababu ni kikosi kazi.

Tahadhari:

Kama unajua hauwezi kumuacha mpenzi wako usimchunguze.

Kudukua ni kosa kisheria.

Hata wanaume ni waongo ila dada zetu wamezidi.
 
Mwanamke muamini kwenye mambo mengine, sio mapenzi.

Kumuamini mwanamke kwenye mapenzi ni sawa na kucheza bahati nasibu. Unaweza kupata au ukakosa ila uwezekano wa kukosa ni mkubwa kuliko kupata.

Trust at your own peril.
Kweli mkuu kwenye mapenzi hawa watu hawaaminiki kabisa
 
dah, mkuu kumwamini mwanamke asiimia zote ni sawa na kujitengenezea kitanzi wewe mwnyewe, haya yote yanasababishwa na kua na mpenzi mmoja lazima utaumia tu
Mana mapenzi yote anayaweka kwenye ndoo moja ikipasuka ndo basi tena
 
Mwanamke muamini kwenye mambo mengine, sio mapenzi.

Kumuamini mwanamke kwenye mapenzi ni sawa na kucheza bahati nasibu. Unaweza kupata au ukakosa ila uwezekano wa kukosa ni mkubwa kuliko kupata.

Trust at your own peril.
dah, mkuu kumwamini mwanamke asiimia zote ni sawa na kujitengenezea kitanzi wewe mwnyewe, haya yote yanasababishwa na kua na mpenzi mmoja lazima utaumia tu
Kweli mkuu kwenye mapenzi hawa watu hawaaminiki kabisa
Hizi comments zitanifanya nisome huu uzi wote mpaka nukta,.sio kwa shambulizi hizi,.
 
Mwanamke muamini kwenye mambo mengine, sio mapenzi.

Kumuamini mwanamke kwenye mapenzi ni sawa na kucheza bahati nasibu. Unaweza kupata au ukakosa ila uwezekano wa kukosa ni mkubwa kuliko kupata.

Trust at your own peril.
Hata kwenye mambo mengine don't trust a woman
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom