Usimsifie mtoto wako wa kiume kuwa ni handsome boy akasikia, utamharibu

mtu mzuri ni mzuri tu hata asiwe na akili wala pesa.. kwa kuwa umevipa vipaumbele hizo sifa nyingine kwamba zinachukua precedence over u-handsome/ uzuri in general ibaki kuwa hulka yako..
 
Sie mwenye vipara matumbo makubwa wafupi na pua pana ,macho makubwa mekundu, weusi wa njaa, hatimae leo tumepata mkombozi.
1705924892905.jpg
 
Robert Heriel Mtibeli na wewe mada zako siku hizi mbili tatu unaandika kama sio yule tuliyekuzoea mwenye nondo za maana.

Sasa mzazi kumwita au kumwambia mtoto handsome kuna shida gani? Labda kama unataka kusema masingle mother kijanja wale wanao peti peti mtoto hadi anakuwa kama zezeta.

Hapana Mkuu sina ñia ovu ya kumsema yeyote isipokuwa tabia hatarishi inayoweza kumuathiri mtoto wa kiume.

Mzazi kumsifu mtoto wake sio tatizo. Inategemea anamsifu katika nini. Mtoto wa kiume ukimsifia mambo ya UHB lazima apuyange kitabia iwe kiutafutaji, au kuwa mlenda mlenda
 
USIMSIFIE MTOTO WAKO WAKIUME KUWA NI HANDSOME BOY AKASIKIA, UTAMHARIBU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wazazi wengi hasa kina mama wameharibu watoto wao wa kiume kwa kuwasifia sifa hii kuwa vijana wao ni Handsome boys, Yaani wavulana wazuri wa maumbile na wenye mvuto wa kimapenzi. Huenda ni kweli kijana wako ni mzuri wa sura na maumbile hasa kimvuto wa kimapenzi lakini huna sababu ya kumwambia akasikia.

Kumwambia kijana wako ni mzuri kutamuathiri kisaikolojia. Na atakosa kuwa mwanaume kamili. Elewa kuwa uanaume kamili unaanzia kichwani yaani mwanaume ni akili. Sifa ya uzuri ni sifa ya Kike au kitu kinachotumiwa.
Mwanaume hatumiwi bali yeye ndiye mtumiaji.

Sio rahisi kukuta kijana Handsome boy anaakili nyingi, sio rahisi. Sio rahisi kukuta kijana Handsome boy NI kichwa darasani. Ni ngumu sana. Sio rahisi kukuta kijana Handsome boy anapesa nyingi au ni tajiri. Sio rahisi.

Handsome boy wengi wameharibika au kuharibiwa akili na maneno ya kuitwa wazuri tangu wakiwa wadogo. Hii inawafanya wawe kama Wanawake tu.

Ni Handsome boy Wachache sana ambao wamebaki na sifa za kiume. Yaani ukute Handsome ambaye kichwani yupo vizuri ni sawa na ukute Mwanamke mwenye matamko makubwa alafu awe na akili. Ni nadra sana. Yaani kwenye Handsome boy 100 basi mmoja ndiye utakuta hajaridhika kiakili.

Wamama, msiwasemee watoto wenu wa kiume maneno ambayo hayawafanyi kuwa wanaume. Hakikisha mtoto wako unamwambia maneno kama; Wewe ni Mwanaume yakupasa uwe Hodari na shujaa" Unaakili sana mwanangu" unanguvu sana" wewe ni mjanja" Wewe ni mchapakazi". Sio mtoto unamsifia ujingaujinga.

Tatizo la kiumbe kikishaitwa kizuri kinaona kinathamani hivyo kinahitaji kuhudumiwa na kutunzwa.

Kijana Handsome anawaza kutafuta wanawake wenye vipato. Anawaza kulelewa. Yaani akili yake imelemaa kwa sababu tangu akiwa mdogo kalelewa kiuzuri uzuri kama Mwanamke. Akikosa vizuri ndio mwishowe anafirwa na kujiingiza kwenye mambo ya kushiba.

Sio ajabu kwa hapa Tanzania Mtu kuwa Handsome boy huonekana kama shoga kwa sababu ya tabia za Handsome boy kutopishana Sana na Mashoga.

Handsome hataki kazi ngumu na chafu. Handsome boy Kazi kujilamba lamba midomo na kurembaremba kama Mwanamke.

Handsome boy fikra na mitazamo yake ukimsikiliza akiongea hana tofauti na Mwanamke Slayqueen.
Yote ni wazazi kuwasemea watoto maneno yasiyoeleweka.

Ni vizuri uwe Handsome boy alafu uwe mwanaume halisi. Familia na jamii itakufurahia.

Sio Handsome boy kutwa kukimbizana na Wake za Watu kama kichaa. Au kuharibi watoto wa Watu.

Kazi hutaki kazi kujisifia ujingaujinga.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Dogo ndo basi tena. Siku hizi HUNA CONTENT KABISA. Umeishiwa sana. Unakuja na vitu vyepesi sana.. shida nini dogo? Sometimes unatakiwa unyamaze tu utulize kichwa. Ukitaka kila mara upost ndo matokeo yake ndo haya.
 
Dogo ndo basi tena. Siku hizi HUNA CONTENT KABISA. Umeishiwa sana. Unakuja na vitu vyepesi sana.. shida nini dogo? Sometimes unatakiwa unyamaze tu utulize kichwa. Ukitaka kila mara upost ndo matokeo yake ndo haya.

Huwezi nielewa. Wapo walioelewa nimeandika nini.
Hata hizo ulizokuwa unazielewa na kuziita contents wapo ambao hawakuzielewa na walizoona ni pumba.
Hivyo acha ubinafsi.
Kitu kama kioo chini ya uelewa wako au unakielewa au unakijua na hakitakusaidia usidhani hakitasaidia wengine
 
Huwezi nielewa. Wapo walioelewa nimeandika nini.
Hata hizo ulizokuwa unazielewa na kuziita contents wapo ambao hawakuzielewa na walizoona ni pumba.
Hivyo acha ubinafsi.
Kitu kama kioo chini ya uelewa wako au unakielewa au unakijua na hakitakusaidia usidhani hakitasaidia wengine
Usichukie au kuwa mbishi waliokuzidi umri wanapokushauri au kukupa maonyo.

"mwanangu sikiliza mausia ya baba yako na ushauri, akushauripo kuacha mabaya usishupaze shingo, la sivyo itavunjika"
mimi 20:24
 
Back
Top Bottom