SoC03 Usimamizi wa taka ngumu

Stories of Change - 2023 Competition

Pso

New Member
Jun 28, 2023
1
0
Neno "usimamizi wa taka ngumu" linamaanisha ukusanyaji, matibabu na utaratibu wa utupaji wa taka ngumu. Taka ngumu ni nyenzo isiyo ya kioevu, isiyo na mumunyifu kuanzia taka ya manispaa hadi taka ya viwandani ambayo wakati mwingine huwa na vitu changamano na hatari. Inajumuisha taka za nyumbani, taka za usafi, taka za biashara, taka za taasisi, upishi na taka za soko, taka za matibabu, na taka za kielektroniki.

Taka hukusanywa kutoka kwa vyanzo mbalimbali na hutupwa kupitia mchakato wa usimamizi wa taka, ambao unahusisha ukusanyaji, usafirishaji, matibabu, uchambuzi na utupaji. Tani kadhaa za takataka huachwa bila kukusanywa katika mitaa ya miji mingi inayoendelea kila siku, hii unaopelekea kuwa eneo la kuzaliana kwa wadudu wanaoeneza magonjwa, kuzuia mifereji ya maji machafu, na kusababisha maswala mengine ya miundombinu. Kutokana na ufanisi mdogo wa ukusanyaji wa taka hizi katika miji na majiji mbalimbali hapa nchini, napendekeza ungetumika mfumo ufuatao;

Serikali kutoa kibali kwa sekta binafsi zenye uwezo wa kukusanya taka kwa kutoa bei elekezi ya gharama nafuu inayopaswa kutoletwa na kila mwananchi atakayehitaji huduma hii kutokana na kiasi Cha taka alichonacho. serikali inapaswa kutoa bei elekezi kwa kika kiasi Cha taka ambayo ni nafuu na kila mwananchi anaweza kuimudu. Hivyo kampuni nyingi zinajitokeza kwa akili ya kutoa huduma hii huku zikiwa na vifaa bora vya kukusanyia taka kutokana na muongozo wa serikali.

Mamlaka husika kutoa elimu katika jamii juu ya athari zinazotokana na mrundikano wa taka ngumu katika makazi ya watu, jamii inapaswa kufahamu athari za milipuko ya magojwa yanayosababishwa na kutelekezwa kwa taka ngumu katika makazi pia uharibifu wa miundombinu kama mitaro na barabara. Endapo jamii itakua na uelewa kutakua na muitikio chanya na ushirikiano thabiti juu ya uthibiti wa taka ngumu. Jamii inakua mdau namba moja katika kutekeleza sera ya usafi huu katika maeneo yote nchi; hivyo tutakua na jamii yenye uelevu juu ya athari zinazotokana na kutelekezwa kwa taka ngumu katika makazi ya watu.

Kazi kubwa ya manispaa za miji na majiji iwe ni kutoa muongozo na kushughulikia changamoto zinazojitokeza kuliko wao kuhusika na ukusanyaji wa taka hizi ambao umepelekea taka nyingi kubaki mtaani. mfano kutenga maeneo maalumu ya kuziweka taka hizi baada ya kukusanywa, serikali kushirikia na kampuni binafsi zitakazopewa kibali kushauriana njia rafiki ya kuyafikia maeneo yote ya miji kutokana na changamoto za kiusalama, kijiographia na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza.

Serikali za mitaa kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba na kutoza faini kwa wale wanaolimbikiza taka majumbani; hii inatokana na watu wengi kutopenda kushiriki kikamilifu katika zoezi la kudhibiti taka, kupitia adhabu zitakazotolewa kila mtu atakuwa na utayari wa kushiriki zoezi hili kikamilifu. Hivyo kungua kwa kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayosababishwa na mrundikano wa taka hizi. mfano, ugonjwa wa kipindupindu ambao hnasababishwa na usimamizi mbovu wa taka.

Zifuatazo ni faida za mfumo huu katika ukusanyaji wa taka ngumu katika miji na mjini mbalimbali hapa Tanzania;-
Kuongeza ushindani unaopelekea ufanisi; endapo sekta binafsi zitapewa kibali cha kudhibiti taka ngumu katika miji na majiji hapa nchini, kutakuwa na usimamizi imara na kufanya kazi kwa kujituma, taka ngumu zitakusanywa kwa wakati na kwa ushindani ili kuongeza mapato katika taasisi husika. Hivyo changamoto ya kuwa na taka ngumu zinazotelekezwa mtaani litakua limepata suluhu.

Kuongeza ubunifu na ajira binafsi; endapo kutakua na taasisi nyingi zinazojishughulisha na ukusanyaji wa taka ngumu, ubunifu utaongezeka katika zoezi la ukusanyaji taka ili kuvutia wateja wenye taka hizi. Pia sekta hizi zitaajiri vijana wasio na ajira, hivyo itasaidia kupunguza tatizo la ajira katika nchi yetu.

Serikali kuongeza mapato yanayotoka na kodi; hii ni kutokana na taasisi binafsi zitakazopewa kibali cha kuthibiti taka zitahusika katika ulipaji wa kodi hivyo serikali kujipatia mapato yatakayosaidia kutatua changamoto mbalimbali katika zoezi la usimamizi taka ngumu pia mapato ya kodi hizi yatatumika katika ujenzi wa nchi yetu.

Kupungua kwa uharibifu wa miundombinu ya barabara na mitaro; imeshuhudiwa katika miji na majiji mengi yanatokea mafuriko kutokana na mitaro ambayo inahusika kupitisha maji machafu na ya mvua kuziba sababu ya taka ngumu ambazo zinatupwa katika mitaro hiyo, mfano TARURA wanatumia gharama nyingi kila mwaka kuzibua madaraja na mitaro ambayo inaziba sababu ya taka ngumu, fedha hiyo ingetumika kujenga barabara na mitaro mipya katika miji na majiji hapa nchini. Hivyo kama pendekezo hili litanyiwa kazi, miundombinu itakuwa salama na kupunguza gharama za marekebisho kila mwaka ambazo zingetumika kujenga miundombinu mpya.

Kupungua kwa maambukizi ya magojwa yanayosababishwa na mrundikano wa uchafu; magojwa kama kipindupindu na typhoid yamekua changamoto katika sehemu nyingi Tanzania sababu ya usimamizi mbovu wa taka ngumu, imeshuhudiwa milipuko ya magojwa haya kama Dar es Salaam, Iringa na sehemu nyingine za nchi sababu kubwa ikiwa ni uchafu uliopindukia katika mitaa mbalimbali kutokana na taka zilizotelekezwa. Magojwa haya yamesababisha vifo kwa raia na kuathiri nguvu ya taifa katika uzalishaji. Hivyo ili kupambana na tatizo la mlipuko wa magojwa haya ni vema mamlaka husika kuzingatia mapendekezo haya.

Kwa hiyo; kutokana na miji na majiji mengi nchini Tanzania kama Dar es Salaam, Mbeya, na sehemu nyingine za miji kukumbwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na usimamizi mbovu wa taka ngumu ambazo zinatelekezwa katika sehemu za majiji na miji ni vema yakafanyika mabadiliko ya usimamizi kama ilivyopendekezwa katika andiko hili. Tanzania itakua miongoni mwa nchi zitakazo sifika kwa usafi duniani, tutaongea tija ya watalii kuja kutembelea vivutio vyetu sababu ya usalama wa kiafya zaidi ya yote kizazi kijacho kitakua katika misingi bora ya usimamizi wa taka kutokana na kile watakacho rithishwa na kizazi chetu.
 
Back
Top Bottom