Usilogwe ukaondoka nyumbani na kwenda usipopajua kwa kigezo cha kutafuta maisha

Basi tukapanga siku twende pale zahanati ya chuo tukapime, nikasema poa maana ile zahanati ya chuo naiamini, chochote utachopima pale utaambiwa hauna, kuna siku nilienda pale nnaumwa balaa, yaan nashikiliwa nisianguke, ajabu nikapimwa maleria nikaambiwa sina, kwenda kairuki kupima nakutwa na maleria za kufa mtu, basi nikasema pale ukienda kupima hata uzito si ajabu ukaambiwa hauna
😂😂😂😂😂
 
Kwenye mabomu ya Gongo la mboto hapo ni kweli tulikuwa tunasuburi Practical ya chemistry Pugu Boys. Ila nimejaribu kufungua code nimeshindwa kukufuhamu maana Kwa maelezo hayo tulikuwa wote PCM.
Pole sana Classmate PCM na COET na hongera Kwa kula shavu
 
Kwenye mabomu ya Gongo la mboto hapo ni kweli tulikuwa tunasuburi Practical ya chemistry Pugu Boys. Ila nimejaribu kufungua code nimeshindwa kukufuhamu maana Kwa maelezo hayo tulikuwa wote PCM.
Pole sana Classmate PCM na COET na hongera Kwa kula shavu
Nyie mlikua nyuma yetu, jamaa alielezea vizuri sana maisha ya Puguni
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO

ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Kweli kesho ikafika, Daah ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu, yani yaliyonipata siku ile ni Mungu tu aliingilia kati, daah!! We acha tu, Basi bana siku ilianza fresh tu yaani,kulipambazuka vizuri nikajiandaa pale niende zangu moshi,

Endelea,,,,,,,,,,,,

Nikachomoka kiwandani nikapanda daladala pale nje huyoo paka town, Nikashuka pale nikadandia kosta ya moshi nauli buku mbili fresh,

Nikafanikiwa kufika moshi town pale, basi nikaona hieace za majengo, nikamuuliza konda zinafika majengo secondary akasema eeeh!! panda twende, Nikapanda pale ngoma ikajiachia hiyoo,

Basi tukafika sehemu konda akasema we wa sekondary sogea mbele, basi nikajivuta mbele, mara gari ikasimama nikashuka, Kumbe shule ipo njiani kabisa haina hata haja ya kuulizia, Maana nliposhuka tu nikaona wanafunzi, nikaona na kibao Majengo Secondary school nikasema yes mambo si ndo hayo, maana mi nlijua kuna mambo ya kuchukua bodaboda,

Basi nikasogea pale getini nikakuta mlinzi pale, nikamwelezea shida yangu, basi mlinzi akaniambia, bwana hata nikikuruhusu kuingia hutofanikiwa sababu mwalimu mkuu wiki ya pili sasa hayupo, Kaenda dodoma kwenye vikao vyao, na yeye ndo muhusika mkuu, Nikushauri tu uende alafu urudi siku nyingine, Basi nikasema sawa,

Basi nikaondoka zangu sijui hata nielekee wapi, Wakati nawaza au nirudi zangu nikapande gari nirudi Arusha basi nikaona upande wa pili zile fremu za maduka zilivyojipanga lazima zitakuwa zimezunguka uwanja wa mpira,

Basi wazo likanijia niingie huko ndani uwanjani, Basi kuna kageti hivi nikaingia kweli bana ni uwanja mkubwa sana wa mpira, Basi nikawa natembea tembea huko uwanjani na begi langu mgongoni,

Sa wakati natembea nikahisi kama kuna watu nyuma yangu, ile kugeuka hivi kweli bana kuna majamaa mawili yananifata, Nikipinda kushoto nao wana pinda, nikienda kulia nao wanaenda nikasema hawa ni vibaka, sasa hapa cha msingi ni kufunga mota tu, Basi kwa mbele kule kulikuwa kuna dada mmoja na yeye anapita pale uwanjani, Nikasema nikimbilie alipo yule dada,

Basi nikatoka nduki hiyo, jamaa wakaanza kunikimbiza, sasa wakawa wanapiga makelele kamata mwizi huyo!!, kamata mwizi huyoo!! , Basi yule dada alipogeuka akaniona nakimbilia ule upande wake akajua mi ndo mwizi, acha aachie yowe hilo, mwiziiii!!! Mwizi!!! huku anakimbia, heeeh! , Mara naona watu hao wanatoka pande tofauti tofauti wananikimbiza, basi nikasema nisimame, wale vibaka wakanikamata wakaanza kunipiga, wakachukua lile begi langu,
wananipiga wanasema mi mwizi,

Basi watu wakajaa nikaanza kupigwa, Najitetea jamani mimi si mwizi, wezi ni wale wamechukua begi langu, hakuna mtu ananisikiliza, Nikapigwa mtama huo,Nikaanguka chini, nikapigwa, Nikakatwa katwa, najaribu kujitetea hakuna mtu ananisikiliza, mwenye jiwe, mwenyet fimbo, mwenye rungu, mapanga ndo usiseme, nilipoona nimezidiwa nikainama chini wapige tu sehemu zote lakini si usoni,

Basi nikapigwa sana, yaani namaanisha sana yani, Mwili wote umetapakaa damu, basi mi nimejiinamia nalia tu, Nalia paka makamasi yanatoka yanachnganyikana na damu, Nasema jamani mnaniua mimi nimewakosea nini, msiniue jamani mimi si mwizi,

Basi nilipigwa na kitu hicho mgongoni nahisi ni tofali lile, nikasikia kama uti wa mgongo umevunjika yaani, nikajinyoosha nikalala na tumbo, hapo sa ndo naona nakufa sasa, maana nalia hata sauti haitooki, Watu hawajui mzee, waoo wanapiga tu, basi sasa nikawa siskii tena hata maumivu, wanapiga mi hata siskii,

Mara macho yakaingia nuru flani hivi kama miale ya jua la jioni, Basi nikawa naona kama naelea angani vile, Mara nikamwona Sity anakuja kunikumbatia anatabasamu na vidimpo vyake vile, Mara namwona Da J kama ananipa mikono hivi anipokee, Mara anatokea mama kama ananiita vile, namwona baba na yeye, Mara nikaona watu kama malaika hivi wanakuja kunichukua, mara wakapotea, nahisi fahamu zikawa zimenirudi nikawa naskia kelele za watu, kumbe bado wanajipigia tu mi sijui,

Basi nikaona kama nimekalishwa hivi, nikahisi kitu kama tairi nimevalishwa huku nikekaa, Mara namwagiwa kama maji hivi kumbe ni mafuta taa, nikajaribu kufungua macho kwa mbali nikaona watu wamenizunguka, mmoja ana kibiriti anahangaika kukiwasha, Basi nataka nimwambie nisamehe usifanye hivyo ila mdomo haufunguki, nataka ninyooshe mkono nimzuie ila siwezi, Mara nikapigwa na kitu sjui ni nini, kuanzia hapo ndo sikujua nini kiliendea tena, nikawa nimefloot,

Itaendelea
Dah! Pole sana mkuu
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,

Tukarudi kwenye magari tukaanza kupiga stori, kumbe wale jamaa wameenda kujikusanya limekuwa kundi kubwa wamekuja pale yard wanataka wafunguliwe waingie lasivyo wanavunja geti, wapo na mawe, mapanga, mafimbo, basi ikawa fujo pale, kesi ikawa kwamba Wakongo wameshirikiana na Watanzania kuwapiga wazambia, fujo zilipozidi wale walinzi ikabidi wapige simu polisi, Polisi wakaja pale wakapewa maelezo na wananchi na wale walinzi, wakaja kwenye magari wakatuchukua,

Endelea,,,,,,,,,,,,,,

Tukapelekwa Kituo cha polisi Nchelenge, Tukatoa maelezo pale, kweli ikaonekana tumewashambulia wazambia, halafu sisi ni wageni, polisi wakatutisha pale kuwa hii kesi ni kubwa na kama itaenda mahakamani lazima tufungwe, kwaiyo tuangalie mifuko yetu hii mambo iishie pale,

Wao wakawa wanataka kila mtu atoe kwacha elf moja sawa laki moja ya kibongo, Kisoda akasema hiyo hela sisi hatuna, sisi tutatoa kwacha hamsini hamsini kama haifai bora twende huko mahakamani,

Wakajitafakari pale ,wakasema leteni hiyo hela, kweli Kisoda na Anko wakatoa hiyo hela , Wale polisi wakatupa escort mpaka kwenye magari yetu tukarudi tukalala,

Kesho yake jumapili tukafua fua pale, na mimi nikafua maana nguo zangu ni zile alizonipa Kisoda na zile nlizokuwa nimevaa mwanzo,

Jumatatu asubuhi tukaenda kwenye zile ofisi za migration na ZRA, tukafanya process pale tukamaliza, tukarudi kwenye magari, wenyeji wa pale wakatuambia kutoka pale mpaka ufike Pweto boda ni kama km 100 hivi ila barabara ni mbovu kichizi, yaan ukitoka hapo asubuhi unafika boda jioni,kwaiyo tukaona kwa huo muda tutachelewa bora tulale tuanze safari asubuhi, Siku hiyo tukalala,

Asubuhi tukaamka tukajaza maji kwenye madumu maana huko tuliambiwa maji ni shida, kumbe yale mafuta yanaenda mgodini huko kongo kijiji kimoja kinaitwa kapulo, Tukalipia parking pale tukaondoka, tukafika sehemu lami ikaisha ikaanza barabara ya vumbi, yaani huko magari kupita ni nadra sana, hadi watu wanashangaa magari yakipita, barabara yenyewe kama za mtaani jinsi ilivyo mbovu, basi ikawa ni mdogo mdogo, gari unaibembeleza kuingia kwenye korongo usije ukapasua busta,

Tukawa tunaambaa ambaa na mwambao wa lile ziwa, tukafika sehemu mvua acha ianze kupiga, ikapiga mvua balaa, barabara haipitiki, tukatafuta sehemu tupaki magari mpaka mvua ikate, kabla hatujapata gari ya anko ikateleza ikaingia mtaroni, piga resi pale kuitoa haitoki, hiki kisanga kingine tena, mvua ndo imechanganya kichizi, tukasimama tukazima gari katikati ya barabara maana tungesema tupaki pembeni na sisi tungeingia mtaroni, tukatulia kwenye gari mpaka mvua ikate, ikanyesha wee mpaka ikaamua kukata, sasa mtihani ni kuitoa ile gari ya Anko, hatuna rope wire hatuna nini!,

Tukenda kwa wanakijiji kuazima jembe na beleshi tukaja kuchimba, jaribu kuitoa lakini wapi, zama huko chini chimba weee, tukajaza majani lakini ngoma haitoki,hapo tumechafuka matope balaa, tukapambana pale mpaka jioni ilkaingia lakini wapi, ajabu ile njia magari hamna kabisa, yaani tumepaki katikati ya barabara lakini hakuna hata gari moja iliyofika pale,

Basi tukawa hatuna jinsi, ni kulala tu mpaka kesho , tukaomba kuni kavu pale kijijini tukawasha moto tukatafuta vijana wawili wa pale kijijini tukasaidiana kulinda magari,

Tukakaa pale mpaka kukakucha, tukaendelea na mchakato wa kutoa gari, uzuri kulikuwa kumenyauka kwaiyo tukachukua belt, tukaikunja, kisoda akarudisha gari yake nyuma, tukaifunga ile gari ikavutwa ikatoka, ikabidi twende ziwani kuoga maana tulikuwa tumechafuka sana, tuliporudi safari ikaendelea,

Tulifanikiwa kufika pale boda ya Pweto kwenye saa nne hivi, tukapeleka documents pale tukaruhisiwa kuvuka, tukatembea kama kilomita mbili hivi tukakuta migration ya upande wa kongo, kuna kulipia pale na process nyingine, nao wakaturuhusu kuendelea na safari,

Barabara ya huku kidogo ilikuwa na afadhali maana ilikuwa na moramu, ngoma zikatembea, kuonesha kule ni nadra magari kupita basi watoto wanatoka kwenye vinyumba vyao wanakuja kushangaa magari yakipita,

Hatimae tukafika pale kapulo kwenye ule mgodi, tukaingia huko ndani tukaoneshwa sehemu ya kuegesha magari, tukapaki, kwa vile ilikuwa jioni tayari ikabidi tufanye mpango wa msosi pale, tukala tukaoga usiku ukaingia tukalala,

Kesho yake tukashusha mafuta, tukapewa documents safari ya kurudi ikaanza, Kweli tulirudi salama mpaka dar hakukuwa na shida yoyote,

Chuma ikaenda service, mi nikatumia muda huo kwenda msewe kwa Da J ila sikufanikiwa kumkuta, nilikuta milango imefungwa nyumba nzima haina mtu,

Basi safari nyingine tukaenda tena kongo lakini sasa hivi tukaenda Lubumbashi, tulipitia mpika, serenje, kapiri, ndola, tukaingia kasumbalesa, tukaingia 114( kasumbalesa upande wa zambia), siku hiyo hiyo tukafanikiwa kuingia 200( kasumbalesa upande wa kongo) tukalala pale,

Kesho yake tukatimba mpaka lubumbashi kampuni moja inaitwa Kongo petrol ndo tukaenda kushusha mafuta hapo, Basi wakati wa kurudi upande wa zambia magari ni machache hivyo kisoda akawa ananifundisha kugonga gear, yale madude ni matamu asikwambie mtu,

Basi tukaenda safari kadhaa, Lusaka, ndola, lubumbashi ndo zilikuwa safari ndefu, Nilipata hela nikanunua smart phone kongo maana ni bei poa sana, Niliingia facebook nikamtafuta Sity, nikamtumia messej lakini hakunijibu,

Basi nikaingia kwenye email yangu, kwenye zile post za kazi nilikuwa natumaga, nikadownload vyeti vyangu, nika apdate cv yangu, nikaanza kutuma maombi ya kazi mitandaoni,

Nikawa nikipata nafasi naenda kwa Da J ila nakuta hayupo, nilipoulizia pale nikaambiwa alishahama, nikasema poa,

Siku moja tumetoka kongo, nipo geto ( maana ilibidi nikae geto kwa kisoda), mara simu ikaita namba ngeni, kupokea akaongea sauti serious kidogo, " Naongea na Akili sina", nikajibu ndio, " Ulituma maombi kampuni deshi deshi nafasi ya desh desh Manager ? " nikajibu ndio, " Jumatatu unahitajika kwenye interview kwenye ofisi zetu zilizopo posta",

Mzee simu ilipokata sikuamini eti, nikajiuliza naota nini!!, Kisoda akaja nikamsimulia, akaniambia sasa hayo mambo utayaweza kweli mambo ya kisomi hayo!, Nikamwambia mi sindo mambo yangu haya nimesomea, akaniuliza umesomea wapi, kumbe nilikuwa nimeshasahau kuwa nilimdanganya kwamba sikuendelea na chuo bali nianza biashara ndogo ndogo, basi pale ikabidi nimchane live, nikamwambia nilijiskia aibu tu kukwambia kuwa nilisoma chuo kwa ile hali niliyokuwa nayo,

Basi Kisoda akanisaport pale, nikaenda kutafuta nguo za interview na viatu, maana nguo zangu nyingi yalikuwa majinsi, Nikawa najiuliza sijawahi kufanya interview toka nimezaliwa, hii itakuwaje? Nikawa naingia google nacheki maswali yanayoendana na ile position na majibu yake,

Kweli siku yae siku nikatimba kwenye interview, nilijua nitakuwa peke yangu ila nikakuta tupo kama saba hivi, tukaanza kuitwa mmoja mmoja, ilipofika zamu yangu nikazama, nikakuta panel ina watu watano, wabongo watatu wazungu wawili,

Wakajitambulisha pale, wakaanza maswali yao, mwanzoni niliingiwa upepo ila kadiri muda ulivyozidi kwenda nikazoea yale mazingira, wakaniuliza maswali mengi sana ila nikayajibu yote, wakataka waone vyeti vyangu orijino, hapo ndo ikawa kimbembe, ikabidi nidanganye kuwa viliungulia ndani ila kwa sasa nipo kwenye process ya kupata vingine,

Interview ikaisha, nasubiri majibu sasa, lakini kila nikipima sioni nafasi yangu kuchaguliwa, maana nilikuta wana pale wamekuja na magari, mtu kapiga suti yupo smart sembuse mimi hata vyeti sina,

Siku zikaenda tukaendelea na mishe zetu, siku tupo njiani tunaenda zetu ndola, tukiwa mafinga pale tunapiga msosi mara simu ikaita, nikapokea , nikasikia " Ndugu akili sina" nikajibu naam, " Unaongea na flani flani kutoka kampuni flani flani, napenda kukupongeza kwa kupita kwenye interview , nikutaarifu kuwa kesho saa mbili asubuhi unatakiwa uwepo hapa kwa ajili ya mambo mengine" simu ilipokata nikajisachi kwanza, hivi ni kweli au naota,

Kisoda akauliza ni nini nikamwelezea pale, Akaniambia ndo ushakula shavu ivyoo mzee, nikawa siamini, sasa itabidi mi safari yangu iishie pale, ikabidi tufanye mchakato wa usafiri muda uleule nigeuze dar, kweli nikapata, kisoda akanipa kama elf 70 hivi akasema hizi zitakusukuma, nikachukua na ufunguo wa geto nikawaaga pale nikadandia gari kurudi dar, kwenye saa tano hivi usiku nipo dar tayari, nikafika geto nikaoga nikalala,

Kesho asubuhi nikatimba pale kampuni, nikapokelewa, nikapelekwa kwa director, nikakuta ndo yule mzungu, tukaongea pale, nikapewa mkataba niusome, ila wakasema huu mkataba hutasaini kwa sasa, kwa sasa utafanya kama intern kwanza kwa miez sita, wakiridhika na performance ndo nitasaini mkataba wa kudumu, na kipindi cha intern ntalipwa mshahara nusu, akaniuliza kama nipo tayari , nikamwambia yes sir!!

Basi nikapelekwa kwa hr ni mmoja kati ya wale wabongo wa siku ya interview, kuna documents za kujaza jaza na nyingine natakiwa kuleta,

Kazi ikaanza hvyo, nikapewa ofisi yangu pale iko poa, nikaambiwa nitafute leseni kuna gari la kampuni nitapewa, basi mambo yakawa byee,

Mwisho wa mwezi zikaingia M kadhaa kwenye account, nikasema huu ndo nusu mshahara au wamekosea?

Basi ikabidi niame pale kwa Kisoda nikatafuta nyumba kubwa inayoendana na meneja,

Nikaanza kumtafuta Sity, nikaenda kwa Ant yake mmoja madale alinipelekaga Sity, nikafika Anti akanipokea fresh, ila alichoniambia kilifanya nilie kama mtoto,

Akaniambia Sity alifariki, alipata ajali morogoro wakati anaenda kwao bunda, nililia sana, nikamwomba shangazi siku moja anipeleke huko bunda nikalione tu kaburi la Sity,

Siku kweli tukapanga tukaenda, tukafika mpaka kwao, tukamkuta mama yake Sity, ajabu akawa kama ananifahamu vile, aliponiona akaanza kulia, tukajikuta wote tunalia sasa, kumbe kwenye album ya picha za sity kuna picha tulipiga nae zipo kule ndo maana yule mama akawa ananijua,

Tukaenda kwenye kaburi la Sity ,nililia sana pale juu ya kaburi, nililia paka makamasi yakanitoka, nikawa kama nimefufua msiba upya, wote wanalia,

Tukatoka pale, tukaenda ndani, nikawapa pole sana, nikawasimulia jinsi Sity alivyokuwa msaada kwangu, nikamkuta mdogo wake pale wa kiume, ndo kamaliza four ila kafeli yupo nyumbani, Nikamwahidi mama nitamsomesha yule dogo mpaka chuo kikuu, pia nikamwambia nitamjengea nyumba pale pembeni yote ni kujaribu kulipa kwa sehemu tu fadhila zote alizonifanyia Sity, nikaondoka nikarud zangu town,

Kule kijijini kwetu nilitimba siku moja, hawakuamini, wakashangaa sana, wakasema walijua nimeshakufa zamani, mzee na mama walifurahi sana, nikakuta dogo ana watoto watatu sasa,

Nikakutana na Hapy, hakuamini kuniona, kwanza akajua nimeshaoa na sina hata time nae, nikamwambia nitamwoa nani na wewe ndo mke wangu umesahau nilikwambia,

hakuamini eti, nikakuta joyce kawa mkubwa nae shule ameshaanza , nikamwambia happy ajiandae nimekuja kumchukua, hakuamini mzee, pale home walifanya sherehe siku ile, nikalala siku moja, kesho yake nikawaaga maana mjini nipo kwenye kazi za watu,

Kesho yake nikamchukua Happy na Joyce tukaja zetu Dar kuanza maisha mapya,
Da J nilimtafuta mpaka leo sijamuona,

Mdogo wake Sity akarudi shule namsomesha na anaendelea vizuri, pia nyumba nimeshaanza kuijenga saiv ndo ipo kwenye lenta,

Na pale kwetu pia nimeshaanza msingi nataka niangushe mjengo pale,

Mshikaji wangu kisoda sijamuacha, mara nyingi naenda pale na nna mpa saport na yeye maana ana nyumba yake kigamboni anajenga kwaiyo nampa saport mara kwa mara,

Saiv nipo na happy mke wangu na tuna mtoto mwingine Anaitwa Angel maisha ni mazuri asee nakula hela ndefu kiasi, nna usafiri fresh yani,

Kwa wale tunaosota kitaa sababu ya ajira, niwatie moyo tu mlango wako upo, siku moja utafunguka, ila tu Sikushauri kujilipua na kwenda sehemu hukujui, huna ndugu, huna hela eti unaenda kutafuta maisha, siku shauri,

MWISHO

Na mimi Akili Sina nichukue nafasi hii kuwashukuru wote tuliokuwa pamoja kuanzia mwanzo hadi mwisho kwenye stori ya ndugu yetu huyu, Niwajuze tu huu mkasa haujanikuta mimi, nilihadithiwa tu na mtu na mimi nikaona niwasimulieni nyie, Karibuni Mbinga huku tule dagaa nyasa,

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA, HAIRUHUSIWI KUKOPI WALA KU EDIT BILA IDHINI
Hongera mkuu leo ndio nimeimaliza
 
Back
Top Bottom