Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
Gazeti la Nipashe linatuhabarisha ya kuwa ushindi wa Mbunge wa Ludewa huko Njombe Mheshimiwa Deo Phillip sasa kuamuliwa na mahakama baada ya kupingwa huko...............
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, amefunguliwa kesi ya kupinga ushindi wake.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa akipinga ushindi wa bila kupingwa wa mbunge huyo.
Aliyefungua kesi hiyo, Manfred Peter Mtitu, anaiomba Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa kutamka kwamba ushindi wa bila kupingwa wa Filikunjombe ni batili na kuamuru uchaguzi mdogo ufanyike katika jimbo hilo.
Msajili wa Wilaya wa Mahakama hiyo, Firmin Matogolo, amethibitisha kesi hiyo kufunguliwa mahakamani hapo na kueleza kuwa kesi hiyo ni Namba 02 ya mwaka huu.
Kwa mujibu wa Matogolo, Mtitu amefungua kesi hiyo kupitia kampuni ya uwakili ya Mpoki ya Jijini Dar es Salaam ambapo mshitakiwa wa kwanza ni Mbunge wa Ludewa, mshitakiwa wa pili ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa na wa tatu ni Mwanasheri Mkuu wa Serikali.
Mtitu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema na aliteuliwa kihalali na chama chake kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa.
Anadai kuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo alimtangaza Filikunjombe wa CCM kuwa mgombea pekee baada ya mtu mbaye hakuteuliwa na Chadema, Geofrey Mgaya kuenguliwa.
Anadai kuwa Mgaya hakuwa mgombea wa Chadema kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu wa Chadema, mgombea ubunge anateuliwa na makao makuu ya Chadema na kwamba yeye ndiye aliyeteuliwa.
Anadai kuwa alipopeleka fomu zake kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, alizikataa kwa madai kuwa hawezi kupokea wagombea wawili kutoka chama kimoja (Chadema).
Mlalamikaji katika kesi hiyo anadai kwamba alipeleka barua ya kulalamikia hatua hiyo kwa msimamizi huyo, lakini aliidharau, kitendo ambacho kilimnyima haki yake ya kikatiba.
Anadai kwa kufanya hivyo, uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi ikiwemo ya kutozingatia sheria ya uchaguzi namba 343 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002 pamoja na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali namba 279 la mwaka huu.
Aidha, anadai kuwa kwa kushindwa kupokea fomu zake, msimamizi wa uchaguzi alikiuka kifungu namba 38, kifungu kidogo cha 5 cha sheria hiyo ya uchaguzi.
Kwa msingi huo, mlalamikaji anaiomba Mahakama kutamka kwamba kushinda bila kupingwa kwa Filikunjombe ni batili na uchaguzi mdogo urudiwe.
Pia, anaiomba Mahakama itamke kwamba tamko kuwa Filikunjombe alipita bila kupingwa ilikuwa ni batili na ombi lake la tatu ni kwamba Filikunjombe na washitakiwa wengine katika shauri hilo, warejeshe gharama za kesi na gharama nyingine ambazo Mahakama Kuu itaona zinafaa.
CHANZO: NIPASHE
Fully appreciated........................MwanaJF Ruta thanks alot kwa kufungua thread hii! Ina mchango mkubwa sana kwa support yetu kwa Mwanakijiji!!!!!!!!!!!!!!!!
Mwanzo mzuri sana!!!!!!!!!!!! Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetakiwa itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni batili; huu hasa ni mwanzo mzuri kwa move yetu ya kum-support MwanaJF M.M.Mwnakijiji kwa ajili ya jumla ya wabunge wote 19; Filikunjombe, ambaye ni mbunge wa Ludewa, ni mmoja wa waliolalamikiwa katika kesi Na: 02/2010, yeye akiwa mlalamikiwa na. 1; wengine, na.2 ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ludewa, na na. 3 ni Mwnansheria Mkuu wa Serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wakili -Kampuni ya Uwakili ya Mpoki ya Dsm-itathibisha mbele ya mahakama hiyo jinsi sheria za uchaguzi na. 343 mapitio ya 2002, na kanuni zake ambazo zipo kwenye tangazo la Serikali na. 279 la 2010 zilivyovunjwa!!!!; Naamini sheria hizi zitakuwa zimetokana na sheria mama ya msingi-KATIBA!!!!!
Mlalamikaji ameiomba mahakama itamke kwamba kushinda bila kupingwa ni BATILI-hivyo uchaguzi URUDIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!