Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Mtu unayemdharau either Kwa mwonekano au kazi anayofanya .wengi wamebeba vitu unavyohitaji maisha mwako 100%.kama Kuna kitu unakihitaji duniani haijalishi nicha ukubwa kiasi gani basi watu wa Hali hiyo wanajua namna gani ya kukusaidia...

Mimi nilishasaidiwa vitu viwili vikubwa sio vidogo na MUUZA MAJI YA MADUMU anayesambaza kwenye majumba..unaweza kusema mtu huyu atanisaidiaje na Hali yake hii ya chini? Nilidhani mtu anayevaa tai na smart ndio anaweza kunisaidia ..Ukimwona mtu anafanya kazi ya Hali ya chini usimdharau wengi wao huwa pia na michongo mikubwa Sana na wakikupa unatoboa..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nil
Simple tu mavazi ndio njia pekee ya kujitambilisha kwa watu wewe ni mtu wa aina gan bila kutumia cheo wala mdomo wako
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.
a za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.



Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Ndio maana siku zote naheshimu code za maeneo kila eneo lina code zake
 
Ungevunga baada ya kutambuana. Ungechukua point tatu vyema, kabisa. Badala ashoboke yeye ukashoboka tena kwa mara ya pili.
This is the best sigma comment ever.

Mwanaume mwenzetu hakujua acheze vipi hiyo scenario.
 
Japo sijaelewa story ila alivyotaja mwenyewe ulitakiwa uwe Cool usingemuuliza mwenyewe ndio angejiuliza mbona mwamba haja give fuc***k ndivyo Gentlemen anavyofanya
Mate nilitafuta sana comment kama hii.

Mtu akijifanya anakujua usiulize kakujuaje,kitendo cha kuuliza tu unapunguza vyeo vyako,akijifanya anakujua na wewe unajifanya unajua kama anakujua so unapiga kimya mwishowe unakuwa umemzidi kete.
 
Miaka fulani nilikuwa na likizo ndefu ya chuo basi nikaona nisikae bure nikafungua kamgahawa katikati ya mji. Nilikuwa nauza bites zote, juice fresh na matunda fresh.

Nilikuwa karibu na ofisi nyingi na banks. Basi nikawa napata oda ya kupeleka bites na maziwa asubuhi pamoja na matunda.

Dada mmoja staff wa pale CRBD aliweka oda ya matunda kila ikifika saa 6 mchana, ikawa siku nyingine ukipeleka anakwambia umechelewa nishakula kwingine, au leo sili basi narudi nayo. Au ukienda siku nyingine anakuangalia tuu hapokei matunda unabaki umesimama kama sanamu na matunda yako.

Siku moja nikaenda nikiwa na shida ya kufungua joint acc, kufika kwake hata sijamsalimia kanijibu leo sitaki matunda. Nikamwambia nina shida nyingine kabla sijaeleza akajibu tena "hapa tunasikiliza za kiofisi tuu hivyo ondoka". Sijui alijua nataka msaada wa hela au vipi.

Ikabidi niwe mpole maana alikuwa peke yake kwa muda ule customer service pale. Nikamweleza nahitaji fomu kufungua joint acc na mama yangu. Akachukua fomu akanipa akaniuliza "utaweza kusoma na kuzijaza kweli na mama yako??" Nikamjibu ndio. Akaniambia viambatanisho vinavyohitajika nikaondoka kesho nirudishe fomu.

Kesho yake nimeenda na mama, kufika pale akamkaribisha akakae kwenye kiti mimi akaniambia kasubiri pale yaani pembeni, ndio mama akamwambia nimekuja na binti yangu tunafungua joint acc, kwanza alistuka akamuuliza ni mwanao kumbe mama sikujua. Akaishiwa pozi.

Basi katika kupiga stori na bimkubwa akamwambia sikujua kama una binti mkubwa, bimkubwa akamwambia mara nyingi hayupo nyumbani kwasasa yupo likizo anasoma masters huko mkoa X. Alishangaa kwa nguvu Masters?? Aliniangalia sana. Miaka hiyo bimkubwa na mzee walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana mkoani na chapaa zipo za kutosha wanajulikana kila kona. Bank pale walikuwa wanajulikana sana.
Enzi hizo bimkubwa na mzee CRDB wana zile VisaGold so wanahudumiwa kishua....kwahiyo dada akajua huyu sio kwamba anauza matunda kwa dhiki

Dada alikosa raha sana hadi muda anatoa copies akaniambia dada kakae kwenye kiti toka siku hiyo alianza na kunisalimia na kunichangamkia. Mimi wala sikumwonyesha tofauti nikaendelea kumpelekea matunda.
 
Kuna demu fulani tulikutana Masaki(Chole road) nipo very normal. Daaaaah yule demu si akajua kuwa nafanya kazi ya usafi hapo ofsini kwetu.Siku anaujua ukweli nilishitukia nipo nae magetoni.
Sijui wadada wanafeli wapi kwani mifano hii kila siku inasemwa humu ila hawajifunzi, I do know why.
 
Mimi kuna 'Wajeda' Wawili hivi nakumbuka Siku moja nilikumbana nao 'Kichochoroni' wakiwa 'wamemkwida' Dada Mmoja hivi wa 'Kitaani' huku wakiwa 'Wanampiga' na Yule Dada akiwa 'anawatukana' Matusi makubwa makubwa tu. Na huyu Dada nakumbuka amekuwa 'akinipuuza' mno tu pengine kutokana na 'Ukapuku / Umasikini' wangu ( kama tuwajuavyo Dada zetu wa Dot Com Generation walivyo )

Tuacheni 'Kupuuziana' na 'Kudharauliana' tafadhali kwani huwezi jua ni nani 'atakusaidia' au 'kukuokoa' hapa duniani na wengine wameshabarikiwa.
Hapo kwenye red ni vigumu sana kwa Wanawake kukuekewa kwani wao mara zote wanatekwa na muonekano wa nje yaani mavazi, vyombo vya usafiri n.k. wanasahau kuwa hivyo vinaweza kuwa ni vitu vya kuazima tu ili muazimaji atimize lengo lake alilo likusudia.
 
Ungevunga baada ya kutambuana. Ungechukua point tatu vyema, kabisa. Badala ashoboke yeye ukashoboka tena kwa mara ya pili.
Kuna jambo nilitaka kumuambia ila bora umegusia. Ukishaona dem analeta mashauzi na ww unajiamini upo tofauti kausha hizo mambo za unanikumbuka ni ushamba na kujishusha kwa dem.
 
Juzi tu NMB Dodoma:

Jamaa flan kavaavaa tu afu na midevudevu hivi

Kaenda NMB ATM kakuta na wadada wa benki wameweka meza ya kutoa huduma kwa wateja pemben hapo. Akafika tu kauliza (bila hata kusalimia).....kwanini kadi yangu inakataa kuniunganisha NMB mkononi

Dada kamjia juu...."kwanza salimia;...vipi habari za huko,...haya tukusaidie nini??"

Jamaa hakupokea. Mie nawaangalia tu.

Dada karudia tena ...."vipi mzima mwenzetu?? Za ulikotoka??!.....mbona umekuja kasi sana??!"....

Jamaa anaeaangalia tu. Mara akauliza...."ivi ni lazima kusalimia/ au kupokea salam ya mhudumu ili nipewe huduma NMB???...

Wakaanza kumshangaa ..."unatokea wapi wewe, yani unakuja kuvamia tu bila kusalimia..." ....wamamzodoa flan.

Jamaa akaingia Benki ndani. Straight kwa Meneja. Nafkiri hakueleza shida aliyopata nje. Alimueleza tu kama kutaka kusaidiwa shida yake. Sijui ndani waliongea nini??

Wametoka na meneja...hadi pale ATM kwenye meza ya wale wadada....meneja akiwa kashika mkononi kadi ya yule mshua....akawambia wale wadada mmoja wao (sikumbuki jina)...

Meneja: .....hebu msaidie Katibu Mkuu hapa kumuunganisha na NMB Mkononi...(Meneja akaongeza:....mkuu hapa utahudumiwa)...mara meneja katuomba wote wa kwenye foleni ya ATM..."naomba ndugu tumpishe kiongozi anajambo kidogo kwenye ATM ...samahani"...wakaingia ATM meneja, mshua na yule dada.

Wakafanya mambo humo ...kidogo wakatoka. Tukaendelea.

Meneja akamsindikiza yule mshua hadi kwenye gari akaondoka meneja anapunga mkono.

Niliwaangalia wale akina dada mavi yalivyowagonga chupi. Walitoa macho sana wakawa na wasiwasi mkubwa....

Walimchukulia poa
Nimeipenda!
 
Nakumbuka nilikua nimeenda ku report kazini mara ya kwanza. Askari wakanifanyia ukaguzi na kufuata taratibu zote za kiusalama kuruhusiwa kuingia kwenye jengo.

Nilikua na bag nikaliacha pale kwao, ikaja kuniuliza majina yangu, nikataja la kwanza, wakatizamana, akauliza la pili, nikataja akatabasam, akaniuliza la tatu nilivyotaja akamtizama mwenzake akacheka sana. Na kuonyesha hali ya kuwa tuko mrengo tofauti wa kiimani na wao. Nakumbuka nililazimisha tabasam na kutokusema kitu nikapanda juu ofisini.

Baada ya muda kama masaa matatu hivi nikapitishwa kutambulishwa ofisi zote baadae tukamalizia kwa wale ma askari...walihofu sana lakini sikuwahi kuwaonyesha kinyongo chochote licha ya kuwa na hofu mara kwa mara kwamba ningewafanyia kitu..kuna siku nikaona niwatoe wasiwasi kwamba yaliyotokea yalishapita ila siku ingine wasimfanyie hivyo mtu mwingine. Ikaishia hapo.
Safi🙏
 
kunasiku nilipomaliza chuo(unesi) nilienda kufanya kazi ya kuchuma chai pale njombe(luponde) sasa kuna kiongozi mmoja alikua ananinyanyasa sana kosa dogo tu ananikata kilo za chai sasa nilipomaliza mkataba nikawa najitolea hospitali moja bwana we kuna siku nilikua nagawa dawa za kufubaza nakaona mwamba huyu hapa mara nampa ushauri nampima uzito aloo alisa aman kabsa
 
Mimi hizo huwa nakutana nazo sana na imefika kipindi sasa nimezoea na pia nachukulia kama advantages yakuweza kusikia hata watu wanakuongea bila kujua kuwa ni wewe.

Hii imetokana na asset nazomiliki haziendani sana na muonekano wangu kwamaana hiyo Kuna kipindi nanunua viwanja nakuwa nimeshafika site ila bado unakuta muuzaji ananisubiri huku ananisema kuwa boss wenyewe hajali muda bila kujua ndie mimi.

Moja Kali nayokumbuka nilikuwa kwenye ujenz wa nyumba yangu yakuishi sasa kipindi nanunua mtendaji hakuwepo japo muhuli wake ulitumika kwa niaba, sasa nimeanza ujenzi nikawa nimemtoa mwenyekiti kidogo Ili anisimamie mambo ya kibali Cha ujenz kama mnavyojua ujenz wa dar unamambo mengi, basi nipo na mafundi nimejichanganya mara naona jopo la watu limenituzunguka wanataka mwenye nyumba yupo wapi, mafundi wakasema ongeeni na huyo wakanioneshea mm , nikamsogelea dada habari yako akajibu ahaa Mimi sitaki msimamizi nataka mwenye nyumba Yani anayejenga maana huyu atanielewa nn?


Mafundi wakacheka huku wanasubiri kitatokea nn. Nikauliza sasa kama msimamizi maana kwaakuwa kaamua kunichukulia hivyo basi nikavaa huo uhusika, kwani dada Kuna shida gani? Akaanza nyie mnakibali au unakuja kusimamia vitu hujui kitu, kwanza taarifa yenu Sina kbsa asee taarifa ya huu ujenzi naamuru usimame mpigie boss wako, mwambie mtendaji kasimamisha ujenzi mpaka mpate kibali. Bahati yake site for men akatokea akamuita kwa jina we Fulani vipi hapo mbona mnaongea na boss wangu kwa ukali? Akabaki kamtolea macho kwa mshangao, akajikaza akasema namtaka mwenye nyumba. Jamaa akamjibu si huyo hapo ukonae

Nikabaki natabasam tu yy macho yamemtoka maana mjengo si haba ikambidi avunge, haijalishi anakibali sasa kwa sauti ya chini sasa , jamaa akamwambia kamuulize mwenyekiti wako huyo kashamaliza Kila kitu. Daaaah akalowa eh basi kaka karibu sana tutasaidia kwenye mambo ya maendeleo mm huwa sipingi maendeleo ni utaratibu tu jamani, nikamuangalia tu akajizoazoa akasepa ikabaki gumzo tu pale aasee.
Mshukuru Mungu!
 
Nawambiaga watu.. Muuza Karanga alie na Degree na Muuza karanga ambae halijui Daftari ni vitu viwili tofauti.

Mpika Chips mwenye Diploma na Mkaanga chips wa darasa la saba ni vitu viwili tofauti.

Elimu haijifichi hata ufanye kazi ya zege au uwe kondakta ,kuna kitu common kinapatikana kwa WASOMI tu huwezi kikuta kwa mtu ambae hajasoma.

Ndio mana nimesema Ntakujaga rudi kuzitafuta MASTERS na PHD baadae,sina kazi nazo ila nazitaka tu cause najua kuna kitu kikubwa sana nitajiongezea nikiwa kama MACHINGA wa biashara ya mtaji ELUFU HAMSINI.
✅🙏
 
Mtu unayemdharau either Kwa mwonekano au kazi anayofanya .wengi wamebeba vitu unavyohitaji maisha mwako 100%.kama Kuna kitu unakihitaji duniani haijalishi nicha ukubwa kiasi gani basi watu wa Hali hiyo wanajua namna gani ya kukusaidia...

Mimi nilishasaidiwa vitu viwili vikubwa sio vidogo na MUUZA MAJI YA MADUMU anayesambaza kwenye majumba..unaweza kusema mtu huyu atanisaidiaje na Hali yake hii ya chini? Nilidhani mtu anayevaa tai na smart ndio anaweza kunisaidia ..Ukimwona mtu anafanya kazi ya Hali ya chini usimdharau wengi wao huwa pia na michongo mikubwa Sana na wakikupa unatoboa..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hakika
 
Back
Top Bottom