Ushauri wenu kwa ndugu yetu huyu

scientist 08

Member
Aug 8, 2017
66
39
Kisa kipo hivi, Jamaa walikuwa kwenye mahusiano na mdada miaka sita, huyu dada alikuwa amalize huu Mwaka chuo harakati za ndoa zianze, kuna miezi iliyopita Mdada alipitia kwa jamaa akitokea chuo hivyo wakafanya ya kiutuzima, badae mdada akasema amepata mimba Yake, hivyo wakatambulishana nyumbani na Jamaa akaanza kulea mimba.

Mdada amerudi chuo akiwa na mimba huku Jamaa anajiandaa akitoka amuoe akajifungulie Nyumbani kwake kama walivyokubaliana wazazi wa pande mbili. Sasa gafla binti akasema anaumwa na jamaa akatuma pesa ya matibabu , baadae mdada anamwambia amejifungua mtoto mzma na mwenye miezi timilifu

Mdada alipoulizwa mimba gani ya miezi hii mtu anaweza jifungua?? Mdada kajibu kumbe alijichanganya kuna jamaa walikutana itakuwa ndo mimba yake hivyo anaomba jamaaa amsamehe na wazazi wasijue, binti amelia hii Week nzima lakini jamaa nae amegoma hamtaki tena na anataka wazazi wajue

Upande wangu nimemshauri amsamehe na maisha yaendelee, mtoto akikuwa apewe Baba yake
 
Hakuna huruma hapo alikuwa anajua anayo mimba ya jamaa mwingne kabla hata ajaenda kujitegesha kwa huyo mwingne sasa kaumbuka, pole yake sana.
 
Hapo ni kuachana maana huyo mwenzake ni Msaliti' kama alikua anajua yuko ktk mahusiano na malengo ktk hayo kwann ilitokea akalalwa na mwingine tena kavu???? Au ndo yale ya kuliwa kimasikhara!!!!!!!!!!!
 
Bila shaka huyo mtot atakua wako ndo maana unaongea neno msamaha kirahisi kwenye huo ujinga
 
Mabinti wa chuo ni kisangaa apo ata samehe. dem aki rudi chuo michapio ina endelea kama kawaida
 
Asa anasamehe nini hpo? Mdada ampelekee mtoto muhusika. Alijua tokea mwanzo akaamua kumbambikizia mtoto wa watu mimba
 
Kusamehe kwa mwanadamu ni jambo la hekima hapo amsamehe kwamaana si wa kwanza kukosea

Ila ukumbuke kwenye kusamehe haimaanishi kwamba ndo aendelee nae anaweza kumsamehe na kila mmoja akawa na mishe zake huyo manzi apeleke mimba kwa muhusika na mchizi nae atafute kigori mwingine atie ndani maisha yaendele
 
pia wote ni wasomi wa vyuo vikuu
Jf bhana watu wa Jf ni mabingwa wa kujifanya wanasamehe wakisalitiwa,Mabingwa wa kutoa mitaji mikubwa mikubwa wa mademu zao,mabingwa wa kuhonga gari na nyumba,hakika Jf kuna watu wastaarabu Sana.
 
Awambie wazazi kila kitu watambue, hakuna mwanamke hapo aachane nae...
 
ndo ushauro au utopolo
Jf bhana watu wa Jf ni mabingwa wa kujifanya wanasamehe wakisalitiwa,Mabingwa wa kutoa mitaji mikubwa mikubwa wa mademu zao,mabingwa wa kuhonga gari na nyumba,hakika Jf kuna watu wastaarabu Sana.
 
Back
Top Bottom