MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,606
Tumekuwa tukisikia mara kadhaa, Mh. Mbunge, hasa kutoka kambi ya upinzani, akitoa shutuma juu ya suala ambalo hata kama ni la kweli, lakini wamekuwa wakinyamazishwa kwa kutakiwa watoe uthibitisho wa kile wanachodai.
Sasa ikiwa mbunge amepeleka bungeni shutuma hizo kwa suala la kweli lakini hakujitayarisha na ushahidi kamili, hii ni kuwapa kichwa CCM na kuwafanya wapinzani waonekane hawako makini. Pia ni kuwapa nafasi washukiwa kutoka mbio hapo na kwenda "kufukia mashimo yao".
Ili kuepusha hayo, ninawashauri waheshimiwa wetu watayarishe makombora yao kisawa sawa, ili linapokuja suala la "lete ushahidi", ushahidi huo uwepo na wa ziada. Msigeuke kama CCM wa kukimbilia "tupeni muda". Ni bora kulifuatilia suala hata kama litachukua muda gani, lakini siku likitinga bungeni liwe ni kombora la kweli. Hii itawaongezea kuaminika zaidi kwa wananchi na kuwakosesha raha CCM na kimbilio lao la sasa la "Lete ushahidi".