Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,929
Naandika haya baada ya kuibukia huko Arusha kwa kiongozi mmoja wa dini mwenye utata mwingi akitafuta kuombewa kwakuwa anajihisi ana mikosi, mambo yake hayaendi na pengine kuna watu wamemsagia kunguni kiroho kiroho na kimwili.
Kwenda kutafuta tiba (ya kiroho) kwa kiongozi wa kidini sio tatizo kabida! Ishu ni kwamba unakwenda kwa nani? Matatizo binafsi huwa hayatatuliwi mbele ya camera na macho ya watu.
Shabani anaumia sana kuona mpinzani wake Mandonga aliyemchakaza kwa TKO aking'ara na kuwa maarufu kuliko yeye..kuna vitu vya kujifunza hapa ambavyo pengine Kaoneka hajavijua bado.
Pamoja na kwamba Shabani Kaoneka ameathiriwa na kabila! Dhana ya kupenda HAKI! Lakini kuna haya pia.
1. Kuteleza si kuanguka
Kipigo chake kwa mandonga kilimpa ushindi sawa kabisa, lakini mpinzani wake akaweka nia, kipigo kilimjeruhi mwili sio nafsi akajiona ana nafasi ya kusimama tena na kusonga mbele. Kwa hili Mandonga ni mshindi.
2. Kukunjua nafsi
Nafsi iliyokunjamana haina nuru na huleta giza usoni, nafsi iliyokunjamana imejaa maumivu, sononi na taharuki
Nafsi iliyokunjamana huleta uzito wa kimwili na kiroho pia! Ushindi wa ulingoni haimaanishi ni ushindi wa maisha. Kuendelea kusononeka kwamba mshindwa wako anapata support kubwa kuliko wewe hakutakusaidia zaidi ya kuzidi kukudidimiza.
3. Mlikutana na mpinzani wako jukwaani
Wewe tayari ukiwa ni bondia wa siku nyingi na ukicheza kwa mazoea kama siku zote za nyuma! Unashinda ama unashindwa na maisha yanasonga, hakuna zaidi.
Mpinzani wako kaingia ulingoni akiwa kapania kusonga mbele na pengine kulitumia pambano lenu kama njia yake ya kutokea bila kujali atashindwa ama atashinda. Mawio na machweo vilikutana. Determination ni kitu kikubwa sana katika maisha.
4. Watu
Kaoneka ogopa sana kiumbe kinaitwa binadamu, siyo wakweli, siyo wema, hawana huruma, wamejawa na unafiki na ghiliba. Kitendo cha kuongea ya moyoni kuhusu mpinzani wako mbele ya watu kimekubomoa badala ya kukujenga! Hao watu ndio pembeni wanakuita kila jina baya. Kamwe katika maisha yako usioneshe maumivu yako mbele ya hadhira
5. Kipimo katika maisha
Kila mtu ana kipimo chake katika maisha, na kila mtu ana nyakati zake za kupata! Hupaswi kuumia sana kwakuwa hujui kipimo chako ni kipi na umeandikiwa nini na kwa wakati gani!
Kuna wenye elimu kubwa lakini ni maskini wa kutupwa lakini kuna standard zero halafu maisha yao ni neema tupu. Kuna ambao wamesota sana na maisha lakini mpaka leo wanasugua gaga! Na kuna waliogusa kidogo tu halafu ikaitika!
6. Haiba
Kaoneka haiba yako ni ukimya na upole na unaishi katika uhalisia sio mtu wa maneno na kelele nyingi.. Haiba huponza na kuathiri wengi. Mpinzani wako ni tofauti kabisa na wewe, background zenu ndio zimewapa matokeo ya sasa!
7. Kuna ishu za kifamilia ukoo nk
Kuna baadhi ya familia hata zipambane vipi kutoboa ni ishu kwakuwa tayari kuna limitations za kiroho wamewekewa.
Kitendo chako cha kuibukia Arusha kwa nabii kina mengi ya kuangazia, pengine hata yule muimba singeli aliyepewa gari kuna mahusiano. Lakini Kaoneka ogopa sana vitu vinavyofanyika mbele ya kamera vina mengi nyuma yake!
Mimi niishie hapa! Ninachoweza kukushauri usijilize wala kulalama tena mbele ya hadhira. Jitenge na haya maisha ya 'macho' ya viumbe wanaoitwa binadamu. Tiba yako unayo mwenyewe, katafute chumvi yako ya mawe itakutoa kutoka kwenye kuonekana mpaka kuonekana kama jina lako lilivyo.
Nakuombea.