Nakuombea Mungu akupe hekima wewe na wasaidizi wako muweze kulitatua sakala hili vema na kwa wakati. Inahitajika HEKIMA KUBWA kuliweka sawa jambo hili, kwani sioni matumizi ya nguvu, mabavu, vitisho kama itasaidia zaidi ya HEKIMA. Sana sana yataenda kuongeza ukubwa wa tatizo badala ya kulipunguza kama sio kuliondoa.
Wiki hii, Jeshi la Polisi limetoa taarifa ya kuyazuia maandamano yenye lengo la kupinga wazo la mkataba huu - hili ni kosa kubwa la kiufundi. Ushauri ni kwamba yaruhusu maandano ambayo sote tunajua kwamba ni ya amani, yapewe ulinzi, ukiwa na muda yapokee, pokea salam za maandamano hayo, au ukiwa umetingwa na kazi basi mwagize hata Makamu wako, au Waziri Mbarawa au hata Mkuu wa Mkoa ayapokee. Hii itatuma ujumbe kwamba unasikiliza kilio cha wengi, uko tayari kuondoa wasiwasi walio nao watanzania wengi kuhusu sakala hili. Athari za kuzuiwa maandamano ni mbaya zaidi kuliko faida za kuyaruhusu na kuyapokea. Hii ni fursa nzuri kwako ya kujipambanua na utawala uliopita uliotumia nguvu, vitisho katika kukabiliana na masuala mazito yenye kuathiri wenye nchi - Watanzania. Hii ni fursa nzuri sana ya kudhihirisha falsafa yako ya Maridhiano, Ustahamilivu, Mabadiliko, na Kujenga Upya (Reconciliation, Resiliency; Reforms; and rebuilding)
Hata Waziri Mbarawa wakati anahitimisha mjadala kuhusu suala hili Bungeni alisema anakaribisha maoni ya wadau mbalimbali kuhusu suala hili lililolalamikiwa sana. Kuruhusu maandamano ni kwenda sambamba na kauli ya Waziri Mbarawa Bungeni kwamba anapokea na kusikiliza maoni ya watu wote.
Sio siri tena kwamba suala la mkataba wa Bandari (Yetu/zetu?) na DP World (Dubai) kwa hapa ilipofikia, limegeuka kuwa kero kubwa kwa wote, kwa aliyelileta (Serikali) na walioletewa, yaani wananchi. Kero kwa sababu serikali imejaribu, inahangaika na inatumia nguvu nyingi kuwaelimisha Watanzania juu ya manufaa ya mkataba huu, lakini bahati mbaya Watanzania walio wengi aidha hawaelewi au hawajakubaliana na wazo hili. Kero kwa Watanzania kwasababu maswali mengi wanayouliza hayapati majibu, au hata majibu yakipatikana hayawaridhishi na yanawaacha wakiwa na mashaka - ni kero. Kwa kweli ni haki yao kuwa mashaka kutokana na historia ya mikataba ya huko nyuma, lakini hii ni nchi yao, hivyo wanapaswa kuhoji kila kitu kwani atakayeathirika zaidi ni mwananchi huyu wa kawaida.
Uzoefu unaonesha kwamba, ukiwa na tatizo na ukashindwa kulitatua vizuri kwa wakati, ni wazi kwamba tatizo hilo litazaa tatizo lingine, na huenda tatizo la pili litakalozaliwa likawa kubwa zaidi na lenye athari nyingi kwa wote kuliko tatizo la msingi.
Hekima ikuongoze ikikupendeza ufikirie namna ya kuusitisha mkataba huu, kwani serikali ikiendelea na mkataba huu kwa kulazimisha, ni wazi kwamba wananchi wengi watapoteza imani na wewe na serikali yako kwa ujumla.
Ni ushauri tu, unaweza kuchukuliwa ama kuachwa.
Nawasilisha.