MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Kwa waliokuwepo ama kufuatilia hotuba ya Hawa Ghasia bungeni leo, huenda wakaungana nami kuishauri serikali kuanzisha kikao maalum cha Bunge kwa ajili ya kupongezana, kupeana pole na kutoa shukurani. Hivi vikao vya bajeti na vingine ambavyo vinahusisha maswali na majibu kuhusu utendaji wa kawaida wa shughuli za serikali visihusishwe na utoaji wa pole na shukurani, kwani ni watu wengi wanaojitolea muda wao na wengine kusafiri hadi Dodoma kwa ajili ya kufuatilia mambo ya msingi. Muda ambao unapotezwa na Mawaziri na wabunge kwa ajili ya mambo yasio na tija kwa serikali na wananchi huku wakilipana posho kwa ajili ya kupeana hizo hongera na pole kwa watu walio wengi ni kuwapotezea muda tu.