Ushauri kwa machemuli wa chadema

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,599
435
Mh machemuli umeanza vizuri lakini kuna tetesi kuwa kazi yako ni kujenga nyumba Dar na Mwanza pia huko Ukerewe kutoka pesa za mgao za majimbo.

Kama ni kweli ama la wewe jitahidi kupeleka maendeleo Ukerewe. Anza mapinduzi ya KILIMO kwa kuboresha kilimo cha zao la MUHOGO kwa kutumia mbolea ya samadi au kompsti. Tanzania nzima Ukerewe mnaongoza kwa muhogo mzuri usio na sumu, matunda matamu kupita kiasi, viazi vyenye vitamini A.
pandeni miti na anzisha operation ya kujenga vyoo na zungumza na AZAM AWEKE KIWANDA cha kusindika matunda au juisi huko kwenu. Usikae kae kama MAGAMBA Msekwa na Mongela Yalivyo haribu hicho kisiwa bila kuleta maendeleo yoyote.
 
makamada hawatangulizagi maendeleo yao, atoe kwanza shukrani kwa wapiga kura wake then mambo mengine baadae lasivyo anakiuka katiba ya chadema
 
Fedha za maendeleo ya Jimbo hutunzwa na ofisi ya DED, hutumika baada ya program kupitishwa, wewe unadhani zinakaa mfukoni mwa mbunge? Umesahau Shibuda akiwa CCM alikuwa na mgogoro na DED Maswa kwa kumnyima sh milioni 10 kutoka katika mfuko huo?
 
Mh machemuli umeanza vizuri lakini kuna tetesi kuwa kazi yako ni kujenga nyumba Dar na Mwanza pia huko Ukerewe kutoka pesa za mgao za majimbo.

Kama ni kweli ama la wewe jitahidi kupeleka maendeleo Ukerewe. Anza mapinduzi ya KILIMO kwa kuboresha kilimo cha zao la MUHOGO kwa kutumia mbolea ya samadi au kompsti. Tanzania nzima Ukerewe mnaongoza kwa muhogo mzuri usio na sumu, matunda matamu kupita kiasi, viazi vyenye vitamini A.
pandeni miti na anzisha operation ya kujenga vyoo na zungumza na AZAM AWEKE KIWANDA cha kusindika matunda au juisi huko kwenu. Usikae kae kama MAGAMBA Msekwa na Mongela Yalivyo haribu hicho kisiwa bila kuleta maendeleo yoyote.

"Toka mbele ya uso wa mpumbavu maana hutaona kwake midomo ya maarifa"
mithali 14:7
 
Kama ni kweli ni makosa makubwa anafanya Machemuli.
 
Hv kumbe utaratibu mpya ni kua fedha za mfuko wa maendeleo wa jimbo zinatunzwa na mbunge?nilikua sijui utaratibu huo mpya!
 
Back
Top Bottom