Ushauri kuhusu ugonjwa wa kisukari

Terminator

Member
May 27, 2009
32
10
Wana jf

naombeni kujua kutoka kwenu maendeleo ya tafiti ya kupata tiba ya kisukari, maana ukimwi wataalamu wamejitahidi sana, ndio maana zamani mtu akipima akipewa majibu kuwa ana ukimwi watu walikuwa wanajinyonga ila sasa kuwepo kwa arv imekuwa mkombozi kwao.

Moja ya tiba ambayo watu wengi wa sukari wanatumia ni insulin na vidonge kwa type i na ii,
naomba kujua kutoka kwenu kuhusu ubadilishaji wa kongosho(pancrease transplantation) kama umekuwa na mafanikio kwa maana ya kutibu, pia kama kuna aina nyingine ya tiba,

nawasilisha ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom