[USHAURI] Biashara ya Computer Repairs and Maintenance

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
Habari wanaJF,nina mpango wa kufungua ofisi katika mtaa flani katika jiji la Arusha,na ofisi itahusu computer repairs and maintenance,nimejaliwa sana kuwa competent katika kazi hii na ninaifanya kwa muda sasa,nimeshapata fremu,na ninategemea kuilipia karibuni.ningependa ushauri wenu kuhusu ufahamu wenu kuhusu biashara similar,nitafanyaje ili niweze kupata fedha zaidi kuliko hiyo kazi yangu maalum maana nitakuwa muda mchache(labda nusu siku),maana muda mwingi nipo kwenye masomo.ningependa kupata idea zenu katika vitu vinavyoweza kuniongezea mapato kama movies,kuflash simu,vocha,CD rentals na vinginevyo….nitafurahi sana mkinisaidia kimawazo ….natanguliza shukrani zangu.
 
Oya brother mimi ninakipaji cha makorokocho yote ya com! So nipigie kupitia: +255719665022. Napatikana Moshi! Nitakusaidia kinachotafutwa ni pesa utaipata mwenyewe utashangaa.
 
nashukuru sana chriss,nitakucol muda si mrefu...wengine mkinisaidia kimawazo sio mbaya pia
 
Habari wanaJF,nina mpango wa kufungua ofisi katika mtaa flani katika jiji la Arusha,na ofisi itahusu computer repairs and maintenance,nimejaliwa sana kuwa competent katika kazi hii na ninaifanya kwa muda sasa,nimeshapata fremu,na ninategemea kuilipia karibuni.ningependa ushauri wenu kuhusu ufahamu wenu kuhusu biashara similar,nitafanyaje ili niweze kupata fedha zaidi kuliko hiyo kazi yangu maalum maana nitakuwa muda mchache(labda nusu siku),maana muda mwingi nipo kwenye masomo.ningependa kupata idea zenu katika vitu vinavyoweza kuniongezea mapato kama movies,kuflash simu,vocha,CD rentals na vinginevyo….nitafurahi sana mkinisaidia kimawazo ….natanguliza shukrani zangu.

Hongera Snochet, inaonekana uko tayari. Unataka mawazo ya kuongeza mapato. nachukulia kua hauna business plan. kwa sababu ungelipitia swali hili. nadhani kuna mkuu hapo juu amakuarifu kua ni fundi wa mambo ya dot com, na makorokoro memgine, kama alivosema. Nadhani biashara yako au nimeona wengine wenye ujuzi kama wako, wana gawanya biashara katika sehem mbili. Sehem moja inayohusiana na kuhudumia Biashara (maofisi) na sehem ya pili kutuo huduma za Majumbani. Kawaida mahitaji yao ni tofauti. kwa mfano, Huduma za biashara zaweza kua, Ushauri, matengenezo, Networking, Support na data recovery na vinginevyo. Huduma za Majumbani ni kama matengenezo, Kuondoa Virusi, Wireless networking, LAN, repair registry errors, kuondoa application wasizotumia, kufanya computer iwe faster, Home theater, TV-Video installation. Ok ukitaka unaweza kuuza sim lakini usifanya wakujue kwa uuzaji sim. Uwe maarufu kwa huduma zako. Unaweza kuongeza web design kwani tayari una expert wa dot com.

Pia Ningetembelea maduka ya wafanya biashara kama hiyo wa hapo Arusha, ili kupata mawazo ya jinsi gani ya kushindishana nao kibiashara. kwani watu wa arusha wanapenda nini katika hizo huduma. Weka mteja awe ndio focus yako kwa sababu kumbuka kua kazi ni kuhudumia watu. Si ajabu watu wakaja kwako zaidi kwa sababu ya huduma nzuri. (customer service). Tafuta namna ya kufanya duka lako liwe tofauti na maduka mengine, aidha kwa bei au kwa huduma.
Good Luck
 
Kaka hapa juu kamaliza kila kitu kwa kweli.zaidi ya hapo utatoka nje ya mstari.labda jiongeze ufikie kudesign software,like games coz watoto wengi utapata soko
 
Back
Top Bottom