Urais 2015: Walimu vijana watangaza kumuunga mkono January Makamba

Hawa ndio walimu tuliowakabidhi watufundishie watoto wetu, kwa kweli serikali imefanya jambo la maana "kutanua goli" otherwise sifuri zingekuwa zinaongezeka kila mwaka kama type ya walimu tuliokuwa nao ndio hawa
 
Maskini hawa "walimu".

Hawajui au ndio kama kawaida ambayo inasemwa huku mitaani kuwa "walimu" wetu hwajitambui! kama pia ambavyo siku hizi imetanda kwenye fani nyingi.

Maskini "walimu" hawa eti wanadai tumewaaamini na kuwaachia watoto wetu wawafundishe, nasikitika kusema kwamba kwa walichokileza hawa ndugu ni uthibitisho kuwawatoto wetu hawako katika mikono salama. maana hawa kama ndio sampuli ya walimu wetu tumeumia.

lakini kinachoniumiza zaidi ni walimu hawa ni wenyewe kushindwa kutambua matizo yao ya msingi ambayo yatawapelekea kutafuta njia nzuri ya kuyatatua. Kule Muleba walimu wanaofika ofisi ya elimu ya wilaya wanapaswa kuvua viatu ili kuingia ofisini hapa Ujana na Umakamba unaingia wapi, tatizo lakulipa malimbikizo ya madai ya walimu linahitaji kutatuliwa na Makamba? ukosefu wa nyumba za kuishi, mishahara isiyokidhin;k haya mpaka makamba awe rais ili yapate ufumbuzi?

Yule DC aliyewacharaza viboko mgepaswa kumualika katika mkutano huo awape changamoto!Zamani ukiwa mwalimu wewe ni wa kupigiwa mfano, sijui kwa hili ndugu zangu ninyi mnategemea watu wengine waige kitu gani. kwamba sifa ya "ujana" inatosha inatosha kuwa suluhisho la mtatizo yaliyoko kwenye sekta ya elimu?siwaelewi.

labd ninaweza uanza kuwaelewa ama mtanisaidia kufahamu haya masuala mawili. Mosi kwanini Mtandao huu uundwe wiki moja baada ya mwenye nia "kijana" kutangaza nia yake?i ingekuwavyema mkacheza karat zenu vizuri tofauti na mlivyokuja hivi sasa?. Pili, hawa walimu wanaolalamika kila siku juuya hali ngumu ya maisha, kimetokea nini wakusanyike kutoka mikoa tofati ya Tanzania kwa gharama zao ili kutangaza kumuunga mkono mgombea "Kijana"?
'

Walimu wanataka kiongozi wao wanayemuamini usiwasemee wewe

MTANDAO HUU, wenye lengo la kuunganisha nguvu za walimu vijana pale kwenye utengano, kuinua ari za walimu vijana pale ilipodorora,
kuhamasisha umoja wa walimu vijana pale unapoonekana kukosekana, lakini pia kuhimiza uwajibikaji wa walimu vijana pale unapopwaya.

huu ni mtandao utakaohimiza uchapakazi wa walimu vijana pale utapoanza kupotea, lakini pia ni Mtandao utakaoinua hamasa ya kazi kwa walimu vijana pale watakapoikosa.

VIJANA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

Ndugu wajumbe,

Kama Taifa tunapoelekea kwenye Chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani, tuna wajibu wa kulikumbusha Taifa na hasa vijana changamoto zinazotukabili na kushauri namna ya kuzitatua.

ndugu wajumbe,
ni wajibu wetu kuwakumbusha Watanzania kwamba Taifa letu lilikombolewa na walimu, na ndio maana kongozi wa kwanza wa Taifa hili alikuwa mwalimu, na mpaka anakufa si kaburi lake wala magazetini yaliyotanguliza cheo chake cha urais kwenye utambulisho wake, popote anapotajwa, anatajwa kwa hadhi yake ya UALIMU, baba wa Taifa Mwalimu Juliuas Kambarage Nyerere.

sisi walimu wa leo hasa sisi vijana tuna wajibu wa kuvaa viatu vya mwalinu mwenzetu baba wa Taifa, sio tu kushiriki kugombea uchaguzi, lakini pia kuwaelewesha na kuwakumbusha watanzania aina gani ya kiongozi bora na makini atakayeweza kutufaa na kutuvusha salama kwenye changamoto hizi zinazoitwa changamoto za kizazi kipya.
sisi walimu vijana kupitia huu mtandao wetu,

bila kuuma maneno tunasema tunataka taifa letu liongozwe sasa na kiongozi mwenye kuendana na changamoto za hiki kizazi, mwenye fikra za hiki kizazi, mwenye kujua mahitaji ya hiki kizazi, mwenye kuamini na kuaminiwa na hiki kizazi kipya mwenye kuweza kuzungumza lugha itakayoeleweka na kusikika na hiki kizazi kipya
tunataka sasa taifa liongozwe na Damu mpya, damu changa, yenye maarifa, maono, uwezo na kasi kubwa ya kufikiria na kufanya maamuzi yenye kuleta maslahi kwa wengi na wengi hao ni sisi ambao ni vijana.
tunafurahi kuona kijana mwenzetu JANUARY MAKAMBA amejitokeza mbele na kutangaza nia ya kutaka kulitumikia Taifa kwenye uchaguzi ujao, kwa kufanya kitendo hicho tunasema sio tu JANUARY ameonyesha Ushujaa na Uthubutu, bali pia ameonyesha ni jinsi gani vijana wana mapenzi ya dhati na Taifa lao na wanaheshimu michango ya wazee wetu na hivyo tunawataka tuwasaidie pale walipoishia ili sisi vijana tuliongoze Taifa lenye changamoto nyingi kwa fikra na maarifa mapya ya kizazi kipya zha vijana.

JANUARY ameonyesha namna gani watu waadilifu wanapaswa kuwa, Dunia ya watu waadilifu vongozi wenye kutaka kushika nafasi za juu kama urais, hujitangaza mapema ili jamii imchambue na kumchuja kisha kujiridhisha kama anafaa au la.

Dunia ya watu waadilifu haisubiri kiongozi kuja kuomba akagombee urais, Urais ni utashi unaoambatana na uwezo na karama za MUNGU, ni lazima ujipime mwenyewe kama unafaa, JANUARY AMEJIPIMA na ametupa nafasi nasisi tumpime, nasi walimu vijana tunamwambia asonge mbele, nyuma mwiko. VIJANA TULIWEZA, TUNAWEZA NA TUTAWEZA.
 
Huu ni upuuzi na utaahira wa hali ya juu,nna mashaka na mtandao wenyewe,kwani imefika mahali kikundi cha watu wapuuzi wachache wanaamua kukaa na kuja na matamko kwa migongo ya taaluma za watu,kuna maswali muhimu ya kujiuliza na kuwauliza ninyi mnaojiita MTANDAO WA WAALIMU VIJANA TANZANIA,
1.January Makamba amekuwa miongoni mwa watawala wa taifa hili kwa muda mrefu,mchango wake ni upi ktk matatizo yanayotukabili waalimu na taifa kwa ujumla???
2.CCM ya sasa imejaa mapapa wanaoliangamiza taifa letu kwa kasi ya ajabu,kwa kuiba na kudhulumu kila kinachoonekana mbele yao,je,January si sehemu ya wanufaika wa mfumo huo wa kidhalimu??na kama sio sehemu ya wezi na mafisadi wa mali za taifa letu,ni nini amefanya kupambambana na wezi hao,anaokaa nao meza moja???
3.kwa nini tusiwaite nyinyi mnaojiita mtandao wa waalimu vijana Tanzania kuwa ni waathrika wa ugonjwa wa "ujinga wa kihalaiki"???
Pendekezo langu kwenu,jiiteni MTANDAO WA WAALIMU WENYE NJAA,WALIOAMUA KUJIKOMBA KWA CCM,NA KUJITOA UFAHAMU.
HITIMISHO,
TABIA HII YA KUTUMIA MIGONGO YA TAALUMA ZA WATU KWA MALENGO YA KISIASA NI UPUUZI USIOVUMILIKA,UKOME UNATUDHALILISHA WAALIMU.
 
Mimi ni mwalimu na wala si ufahamu huu mtandao walimu tuna matatizo chungu nzima ametusaidiaje huyo januari? msipende kutusemea kila mtu atachagua kiongozi anayemtaka kwanza huyo bwanamdogo bado sana labda aendelee kusubiri 2030
 
Ni taahira tu au mwendawazimu anayeweza kukaa na kuandika tamko la namna hii.

Laiti Mwalimu Nyerere angekuwa hai walimu kama hawa angewacharaza viboko vya matakoni..!!
 
Tuko nyuma yako January kaza buti. Bado Wauguzi, matabibu, polisi, na masela. Hizi ni zama zetu. Kizazi cha Nyerere watuachie nchi yetu tujadili mustakabali wetu.

Utadhani watu hawakufahamu

Nasikia mmewahonga hao watoa tamko milioni 62.5 Source gazeti la Nipashe.

Mnapata wapi hela za kuhonga watu? Mtazilipaje?
 
Naunga mkono,tumewabeba sana sasa niwakati Wa vijana kujibeba wenyewe.Safi sana walimu

Tuko nyuma yako January kaza buti. Bado Wauguzi, matabibu, polisi, na masela. Hizi ni zama zetu. Kizazi cha Nyerere watuachie nchi yetu tujadili mustakabali wetu.

tunataka sasa taifa liongozwe na Damu mpya, damu
changa, yenye maarifa, maono, uwezo na kasi kubwa ya
kufikiria na kufanya maamuzi yenye kuleta maslahi kwa
wengi na wengi hao ni sisi ambao ni vijana.JANUARY SAFI SANA KWA KUTUONYESHA NJIA,TUPO NYUMA YAKO KAKA.

Naunga mkono hoja,vijana tuamke wakati ndio huu umeishawadia sasa tulilembe sana,tuchangamkie fursa hizo za uongozi,january ameishaonyesha njia kwa kujitangazi fursa yake ya kugombea urais 2015.

NI MTANDAO wenye lengo la kuunganisha nguvu za
walimu vijana pale kwenye utengano, kuinua ari za walimu
vijana pale ilipodorora,
kuhamasisha umoja wa walimu vijana pale unapoonekana
kukosekana, lakini pia kuhimiza uwajibikaji wa walimu
vijana pale unapopwaya.
huu ni mtandao utakaohimiza uchapakazi wa walimu
vijana pale utapoanza kupotea, lakini pia ni Mtandao
utakaoinua hamasa ya kazi kwa walimu vijana pale
watakapoikosa.

Njaa zitaua walimu... Kwa vyo vyote ni wanafiki walionunuliwa na kupewa vijisenti na fisadi JANUARY.
 
kijana una fikra mgando saaana

Ben saanane acha kuwatumikia mbowe na slaa,wameesha zeeka hao wanasubiri kufa tu na wanatafuta pa kufia hao na usipokuwa makini utakufa nao.ungana na vijana wenzako mlete mapinduzi mapya,fikra mpya na mawazo mapya.
 
bila kuuma maneno tunasema tunataka taifa letu
liongozwe sasa na kiongozi mwenye kuendana na
changamoto za hiki kizazi, mwenye fikra za hiki kizazi,
mwenye kujua mahitaji ya hiki kizazi, mwenye kuamini na
kuaminiwa na hiki kizazi kipya mwenye kuweza
kuzungumza lugha itakayoeleweka na kusikika na hiki kizazi
kipya
tunataka sasa taifa liongozwe na damu mpya, damu
changa, yenye maarifa, maono, uwezo na kasi kubwa ya
kufikiria na kufanya maamuzi yenye kuleta maslahi kwa
wengi na wengi hao ni sisi ambao ni vijana.

kijana unayempigia chapuo ni wewe tu uliyelipigania tonge,sasa baada ya kupata firsa unaitumia kuvuta wengine wamkubali mtu kama january makamba!!
Hovyoo kabisaa.
Nasisitiza tena january makamba hafai kuwa raisi.
 
kama walimu ni wa aina hii wataachaje kutumika?no wonder wanafelisha watoto.hivi ni lini january aliwahi kuwasemea waalimu ndani ya chama na serikali yake?

kamanda ben' tulia tafuta uenyekiti bavicha utupiganie makamanda kwa maslahi ya wanyonge.
Sisi acha tupambane na hii misukule ya kuazimwa toka lumumba.
 
Njaa zitaua walimu... Kwa vyo vyote ni wanafiki walionunuliwa na kupewa vijisenti na fisadi JANUARY.

fisadi ni nani au ni mtu gani?ebu niambieni january anakashfa gani ya ufisadi mnaodai?ebu tuambieni na hawa watu nao tuwaitaje,Lowasa,Mbowe,Slaa,Membe,Wassira n.k?
 
walimu hawa wanatumia vyeti vya kaka zao! sidhani kama ujana ndo sifa ya kuwa raisi hapa ndo unajua walimu wa siku hizi ni janga!

Tz haina walimu, ina wa.ganga njaa tu. Tambua kwamba walimu wana maadili ya kazi ikiwa ni kutokujihusiaha na siasa. Sasa hawa wanaompigia debe Makamba sielewi kama wamekunywa viroba au wanajitambua.
 
MTANDAO WA WALIMU VIJANA TANZANIA

MAAZIMIO YA MTANDAO

ndugu wajumbe,

Habarini za wakati huu....

ndugu zangu,

Kwa mapenzi ya Mungu Tumekutana hapa leo kufanya Jambo la Kihistoria kwenye maisha yetu ya kazi, hakika mimi na wenzangu hapa mbele, tunawashukuru kwa imani yenu mliyotuonyesha ya kutuchagua tuwe viongozi wenu wa mwanzo, hakika ni jambo jema na kwa niaba ya wenzangu, tunawaahidi hatutawaangusha.

leo Tutaandika kumbukumbu ambayo itakumbukwa sio tu na kizazi chetu bali na vizazi vingi vijavyo vitakavyopata bahati ya kupitia kwenye fani yetu hii ya Ualimu hapa Tanzania na popote Duniani Taarifa hizi zitakapowafikia.
leo, sisi walimu vijana, Tunazindua Rasmi MTANDAO WA WALIMU VIJANA TANZANIA.

MTANDAO HUU, wenye lengo la kuunganisha nguvu za walimu vijana pale kwenye utengano, kuinua ari za walimu vijana pale ilipodorora,
kuhamasisha umoja wa walimu vijana pale unapoonekana kukosekana, lakini pia kuhimiza uwajibikaji wa walimu vijana pale unapopwaya.

huu ni mtandao utakaohimiza uchapakazi wa walimu vijana pale utapoanza kupotea, lakini pia ni Mtandao utakaoinua hamasa ya kazi kwa walimu vijana pale watakapoikosa.

ndugu zangu,
mtandao wetu huu utakuwa chachu ya maendeleo miongoni mwa walimu vijana Tanzania nzima,
utatuunganisha kiuchumi kwa kutuwezesha kubuni namna mbali mbali halali za kutunusha mfuko wetu ambapo itatupelekea kubuni namna mbali mbali za miradi ya maendeleo ili kuendeleza gurudumu la maisha ya walimu.

ndugu zangu changamoto zinazotukabili walimu, hasa walimu vijana ni nyingi mno, changamoto hizi zinafika wakati mpaka zinakatisha tamaa na tunashuhudia walimu hasa vijana wenzetu walio wengi wakiacha kazi ya kufundisha na kujiingiza kwenye shuhuli nyingine.

sisi walimu vijana kwa kuanzia na uwakilishi wa walimu kutoka mikoa 18, tumeamua kwa mapenzi ya dhati kabisa kwa Taifa letu, kuanzisha MTANDAO HUU.

Huu ni mtandao utakaofufua matumaini kwa walimu vijana wa zamani waliopo makazini, na utakaotoa njia ya matumaini kwa walimu wapya wanaokuja makazini kwa mara ya kwanza.

huu sio mtandao wa kupambana na serikali, wala huu sio mtandao wa kushindana ama kuchuana na chama cha walimu, Hapana.

Huu ni mtandao utakaounganisha nguvu za walimu vijana kote Tanzania, kwa kushirikiana na Serikali na Chama cha walimu, kuhakikisha walimu hasa vijana wanafurahia kazi yao wanayoifanya ya kufundisha popote watakapokuwa wamepangiwa na kukabiliana na changamoto.

huu ni mtandao utakaohakikisha, walimu vijana wa Taifa hili wanaongeza juhudi kwenye ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwa watoto zetu wanaohitimu masomo yao
huu ni mtandao utakaohakikisha vijana wengi wanaokwenda vyuoni wanahamasika kusomea ualimu ili kuwa na walimu bora zaidi kwa siku za usoni na kuliendeleza vyema taifa letu.

Ni MTANDAO WA MATUMAINI, ni mtandao wa USHUNDI, huu ni MTANDAO WA NURU, UPENDO MSHIKAMANO Wenye kuhakikisha UWAJIBIKAJI wa kila mmoja kwenye jamii yetu.
ndio maana MTANDAO WETU umeadhimia kuwa na miradi ya kimaendeleo ili kujikwamua na umasikini bila kupigishana kelele na serikali.
ndio maana mtandao wetu umeadhimia kuwa na mashamba ya kilimo yatakayomilikiwa na walimu vijana sehemu mbali mbali Tanzania ili kuchochea maendeleo ya walimu hasa vijana
ndio maana mtandao wetu umeadhimia kuwa na utaratibu rasmi wa kushirikiana kwenye shida na raha dhiki na faraja kufa na kuzikana.

ndio maana mtandao wetu umeanza mchakato wa kuanzisha SACCOS kubwa ya WALIMU VIJANA itakayowawezesha walimu vijana popote walipo kuweka akiba na kukopa kwa kadri watakavyoona inafaa ili kurahisisha maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

SACCOS hii itakuwa ngao ya walimu vijana wake kwa waume, SACCOS hii itakuwa TUNU na MAFANIKIO ya walimu vijana BARA NA VISIWANI, SACCOS hii itakuwa kimbilio la kujiwezesha na kujistiri kwa walimu wapya hasa wanapopangiwa vituo vya kazi na kuchelewa kupata fedha kutoka kwa waajiri wao ambao ni halimashauri
ndio maana tunasema, wacha leo sisi walimu vijana kupitia MTANDAO HUU WA WALIMU VIJANA TANZANIA, tuandike historia itakayokuja kutukumbuka vizazi na vizazi.

VIJANA NA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU

Ndugu wajumbe,

Kama Taifa tunapoelekea kwenye Chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani, tuna wajibu wa kulikumbusha Taifa na hasa vijana changamoto zinazotukabili na kushauri namna ya kuzitatua.

ndugu wajumbe,
ni wajibu wetu kuwakumbusha Watanzania kwamba Taifa letu lilikombolewa na walimu, na ndio maana kongozi wa kwanza wa Taifa hili alikuwa mwalimu, na mpaka anakufa si kaburi lake wala magazetini yaliyotanguliza cheo chake cha urais kwenye utambulisho wake, popote anapotajwa, anatajwa kwa hadhi yake ya UALIMU, baba wa Taifa Mwalimu Juliuas Kambarage Nyerere.

sisi walimu wa leo hasa sisi vijana tuna wajibu wa kuvaa viatu vya mwalinu mwenzetu baba wa Taifa, sio tu kushiriki kugombea uchaguzi, lakini pia kuwaelewesha na kuwakumbusha watanzania aina gani ya kiongozi bora na makini atakayeweza kutufaa na kutuvusha salama kwenye changamoto hizi zinazoitwa changamoto za kizazi kipya.
sisi walimu vijana kupitia huu mtandao wetu,

bila kuuma maneno tunasema tunataka taifa letu liongozwe sasa na kiongozi mwenye kuendana na changamoto za hiki kizazi, mwenye fikra za hiki kizazi, mwenye kujua mahitaji ya hiki kizazi, mwenye kuamini na kuaminiwa na hiki kizazi kipya mwenye kuweza kuzungumza lugha itakayoeleweka na kusikika na hiki kizazi kipya
tunataka sasa taifa liongozwe na Damu mpya, damu changa, yenye maarifa, maono, uwezo na kasi kubwa ya kufikiria na kufanya maamuzi yenye kuleta maslahi kwa wengi na wengi hao ni sisi ambao ni vijana.
tunafurahi kuona kijana mwenzetu JANUARY MAKAMBA amejitokeza mbele na kutangaza nia ya kutaka kulitumikia Taifa kwenye uchaguzi ujao, kwa kufanya kitendo hicho tunasema sio tu JANUARY ameonyesha Ushujaa na Uthubutu, bali pia ameonyesha ni jinsi gani vijana wana mapenzi ya dhati na Taifa lao na wanaheshimu michango ya wazee wetu na hivyo tunawataka tuwasaidie pale walipoishia ili sisi vijana tuliongoze Taifa lenye changamoto nyingi kwa fikra na maarifa mapya ya kizazi kipya zha vijana.

JANUARY ameonyesha namna gani watu waadilifu wanapaswa kuwa, Dunia ya watu waadilifu vongozi wenye kutaka kushika nafasi za juu kama urais, hujitangaza mapema ili jamii imchambue na kumchuja kisha kujiridhisha kama anafaa au la.

Dunia ya watu waadilifu haisubiri kiongozi kuja kuomba akagombee urais, Urais ni utashi unaoambatana na uwezo na karama za MUNGU, ni lazima ujipime mwenyewe kama unafaa, JANUARY AMEJIPIMA na ametupa nafasi nasisi tumpime, nasi walimu vijana tunamwambia asonge mbele, nyuma mwiko. VIJANA TULIWEZA, TUNAWEZA NA TUTAWEZA.

Dunia ya watu waadilifu haihitaji Rais anayesubiri kuoteshwa na mizimu ya kwao kwamba sasa nenda kagomee,
wala Dunia ya Watu waadilifu haihitaji mgombea wa kufananisha Urais na kuvuka Daraja kwamba mpaka alifikie ndio atangaze, waadilifu hutangaza nia na jamii huwachuja.

narudia, bila kuuma maneno, sisi MTANDAO WA WALIMU VIJANA tunatangaza hadharani leo, kwamba tunaunga mkono nia ya kijana mwenzetu JANUARY MAKAMBA na kwamba tunamtaka asirudi nyuma kamwe.

vijana ndio tunu la taifa hili
kama Watanzania wametuamini vijana na kuturuhusu tuwafundishe wadogo zetu mashuleni, leo zaidi ya 85% ya walimu ni vijana, kwanini watanzania hao hao wasituamini na kuturuhusu tuongoze Taifa kupitia JANUARY MAKAMBA?.

Kama watanzania wametuamini vijana na kuturuhusu tulinde mipaka ya nchi hii leo zaidi ya 80% ya wanajeshi ni vijana, kwanini watanzania wasiamini na kutupatia amiri jeshi mkuu Kijana?
kama watanzania wameweza kutuamini vijana na kutukabidhi hospitali tuokoe roho za wenzetu, leo zaidi ya 90% ya madaktari na wauguzi ni vijana, basi watanzania wana kila sababu ya kutuamini na kutupatia Rais wa aina yetu
askari polisi wengi ni vijana, waandishi wa habari wengi ni vijana, vibarua migodini na mashambani wengi ni vijana, bankers wengi ni vijana, mama lishe wengi ni vijana, boda boda vijana, madereva na makondakta wengi ni vijana, wafagiaji maofisini vijana, wasafisha viatu vijana, wahudumu wa baa na hoteli ni vijana, wavuvi na waendesha mikokoteni wengi ni vijana na wasio na ajira wengi ni vijana. mbona huku hawaambiwi kuwa hawana Uzoefu?, mbona huku hawaambiwi kuwa wabaguzi na kwamba wanajipendelea?, kwanini tuulizwe uzoefu IKULU tu?.

mbona asilimia kubwa ya walio na uzoefu ndo wenye kashfa za wizi na ufisadi mkubwa mkubwa unaoliangamiza Taifa?.

tunahitaji kiongozi wa kizazi hiki, huu zio ubaguzi, huu ni ukweli, ukweli unatakiwa usemwe, sio kuogopwa na kufichwa, vijana ni wengi, na sauti yao ni ya wengi, sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na sauti ya vijana ni sauti ya Mungu.

tunamuunga mkono JANUARY MAKAMBA kwa nia yake hiyo, na kwamba aendelee hivyo hivyo na sisi tutaendelea kuwaunganisha walimu vijana kote Tanzania kumpigania ili aje asikie kilio chetu cha samaki ambacho machozi yake yamekuwa yanakwenda na maji kwa kipindi kirefu
january makamba ni mzalendo, na yeye ni muadilifu na ana uwezo mkubwa sana wa kutambua na kuchambua mambo na kwamba hatuna sababu ya kutokumuunga mkono, na luwaomba vijana wengine wengi zaidi wajitokeze kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo uenyekiti wa seikali za mitaa na vijiji, udiwani na ubunge.

sisi MTANDAO WA WALIMU VIJANA TANZANIA, tunaahidi kuwafanyia kampeni January na vijana wenzake wote watakaojitokeza kwenye ngazi mbali mbali mpaka ndoto yetu ya vijana kujiongoza na kujitawala itakapotimia.

tunataka kiongozi asiye na chembe wala nukta ya harufu za ufisadi, kiongozi muasadilifu ili tupumzike kusikia kelele za wizi wa mali za umma. january ni miongoni mwao.

MWISHO.
Tunawahamasisha walimu wa rika zote hapa nchini kutoka mikoa yote kuunga mkono harakati zetu hizi za kutaka Taifa liongozwe na kiongozi anayeendana na kundi kubwa mwenye sifa za kutosha na sifa ya ujana ikiwa ni ya umuhimu wa kipekee.

tunawahamasisha na kuwakumbusha vijana wenzetu wa kada na fani nyingine kwamba, tumekuwa wapiga debe vya kutosha, sasa tujipigie debe, tumekuwa wapambe vya kutosha sasa tujipambe wenyewe, tumekuwa wasindikizaji vya kutosha sasa tujisindikize wenyewe, tumekuwa walalamikaji vya kutosha sasa tujilalamikie wenyewe, tumekuwa wabebaji vya kutosha sasa tujibebe wenyewe, tumekuwa wasukumaji vya kutosha sasa tujisukume wenyewe na tumekuwa wawezeshaji vya kutosha sasa tujiwezeshe wenyewe.

kumuunga mkono January kwetu sisi Vijana ni Kuunga mkono harakati za uundwaji wa Taifa lenye fikra mpya.
Nawashukuru kwa kunisikiliza
na kazi ya ujenzi wa Taifa iendelee

Fredrick Mwakisambwe
Mratibu
MTANDAO WA WALIMU VIJANA TANZANIA
SIMU

Hongereni walimu vijana,Hongera Makamba,Songa mbele wengi tuko nyuma yako.Magazeti karibu yote Leo yanahabari hii.Wanajukwa unaweza kuyapitia Kwa Mengi zaidi.
walimu wote ni wale waliofeli form four au six wengi wao ndiyo maana wao siku zote wanashabikia chochote cha mwanasiasa;;; ndiyo maana nchi watoto wetu wanafeli shule kwa sababu ya walimu wote ni wao ni waliofeli pia;;;;;;''''''' lakini nawaunga mkono kwa sababu bila ssssssssm wao wangekuwa omba omba mtaani,,,,, bravo ssssm;;;; bravo makamba wa rais wa waaalimu tanzania
 
Jibu la swali lako hili.
sisi walimu vijana kwa kuanzia na uwakilishi wa walimu kutoka mikoa 18, tumeamua kwa mapenzi ya dhati kabisa kwa Taifa letu, kuanzisha MTANDAO HUU.

Walimu jeshi kubwa, wako nyuma ya makamba, historia mpya inaenda kuandikwa tanzania baada ya miaka 50, kijana kuongoza taifa letu.

kila la heri makamba jr
Wahuni tu wa Uvccm ninyi na makundi yenu acheni ujinga ninyi
 
kuna watu wakicomment kitu wala hushangai, uchama umewajaa badala ya kuangalia maslahi ya taifa letu,kwa style hii mtu wa namna hii ataendelea tu kuwa operator wa account za facebook za wazee flani ndani ya chama,vijana wenzako wanakuja wanakupita wanatumia vipaji vyao katika uongozi wa nchi yetu wewe unabaki ku post status za wazee facebook,shame on you!,kuwa na maono wewe

usiwe mpuuzi basi!
We unataka tumpe promo huyu january makamba kijana anayepigania nafasi ya kwenda kula ujana ikulu?
Hovyooo! Yaani bora nchi itawaliwe kijeshi kuliko kuongozwa na mtu kama january makamba.
 
Back
Top Bottom