Urafiki wa Police jamii, shirikishi kwa wananchi ni sawa na urafiki wa Chui na Mbuzi

Msandawe Halisi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
647
350
Police jamii, police shirikishi ilinifanya kupoteza maumivu yangu ya Muda mrefu juu ya kifo cha rafiki yangu, ndugu yangu kijana mwenzangu ailiyekuwa anatambulika kwa jina la Issa Nassor miaka ya Ninetiz, kijana aliyekuwa anaasili ya Arabuni. Kijana huyu alikuwa akifahamika kwa jina maarafu Issa Nyaku.

Huyu Issa Nyaku kwa kipendi kirefu alikuwa akitafutwa na askari wa kituo cha Police Kwamtoro Kondoa. Hilo alikuwa tabu kwangu, ni kawaida wa mtu yeyote yule ambaye amevunja sheria na taratibu za nchi. Kilicho niuma ni jinsi huyu kijana alivyo kufa, alikufa kinyama sana chini ya mikono ya Police.

Nakumbuka, alipokamatwa alitembezwa takriban kilometa 20 akiwa uchi wa mnyama. Njiani kote alipigwa sana na hao Police. Alipofika kituo cha Police Issa alikataa roho. Wale Police wote walio husika walikamtwa, na moja wapo nilikutana naye Dar siku moja. Sipendi kufahamu sheria ilichukua nafasi gani.


Sikupendezwa sana na Uongozi wa Jeshi la Police Chini ya IGP Omar Mahita kwa taratibu za jeshi kipindi hicho. Moyo wangu ulirudisha matumaini kwa jeshi la Police Chini ya IGP Said Mwema. Hasa alipoanzisha utaratibu wa Police shirikishi na Police jamii. Nia ni kutaka Mwanachi ajione sehemu ya Police, Police sehemu ya mwananchi.


Kitu ambacho kimerudisha maumivu yangu tena, ni kitendo cha police kuua raia wasio na hatia Arusha. Nikajuuliza, hawa sio ndungu zetu, hawataki tena kufunga harusi na sisi. Nikaona huu siyo urafiki mwema, urafiki wa mbuzi na chui. Nikatafakari kwa kina, nikaona kwa umbali siyo makosa ya mtu ambaye nilimkubali sana, IGP Mwema. Nikagundua ni makosa ya katiba. Katiba ambayo inampa uwezo Rais amteue IGP.


Mimi ni moja wa wanaokandamizwa na katiba hii, Wanachi hima hima kwa pamoja tuungane juu ya ombi la katiba mpya. Tupate katiba ambayo aina udikitekta ndani yake.


Wana JF Still nipo kwa ndugu zangu Warangi, Siku njema wana JF
 
Police hana Rafiki ndugu yangu! yan ni kama kufuga simba, siku akiwa na njaa anakumaliza wewe mfugaji! hatambui tena mchango wako uliompa kwa muda wote huo. Ni kweli katiba mpya yaweza kuwa suluhisho.
 
Uhusiano wowote mzuri kati yetu wananchi tayari ulizikwa siku ile ambapo mashujaa wetu Denisi Michal na Omary Ismael walipopumzishwa kaburini. Sasa hivi na polisi tupo tupo tu tukisubiri kuwatia adamu kwenye katiba mpya.
 
Kweli Msandawe! Katiba mpya ni muhimu sana. Hii katiba tuliyo nayo, ni ya kiujangili kabisa.
 
Hiyo habari nami niliisikia kipinde hicho nikiwa Dodoma. Kwa kweli vyombo vya habari avikuwa vingi hususani magazeti. Tupo pamoja katika kupigania katiba mpya. Tuondokane na huu ukungu tulionao
 
Back
Top Bottom