Upinzani watangaza mapambano 2008

Tuendelee tu kumshambulia SHY lakini hoja yake ni ya MSINGI sana. Naamini nia yake ni kuwafanya Wapinzani wazinduke, waache kuhangaikia umaarufu wa mtu mmoja-mmoja. Vyama vya upinzani vinabaki hoi huku wanachama wake kama Mh. Zitto ni maarufu kuliko CHADEMA; CHEYO ndiye UDP; MREMA ndiye TLP, n.k., kwa staili hii HAWATAIWEZA CCM.
Halafu, hivi kweli tuliomo humu JF hatuwezi kujitokeza kwa uwazi zaidi kuvisaidia vyama hivi?
 
SHY,
Nimekusoma. Mawazo yako umeyaelekeza kwa upinzani kwamba 'they're trying to pollute the situation'. Fahamu kwamba, hali tuliyonayo kwa sasa Watanzania, imetuunganisha pamoja kupiga kelele dhidi ya mafisadi. Si mpinzani, si yule aliyepo kwenye system au si yule asiye na chama wote tu wamoja dhidi ya hao wachache.

Wakati hao unaowabeza kuwa ni wapinzani walipoibua hoja za nchi kufilisiwa na wachache pale Bungeni Dodoma, nchi nzima ilitetema, Bunge lilitetema, wafanyakazi na wakulima walishika viuno vyao kwa mshangao usio kifani. Baada ya hapo 'Sebene' lilianzia Bungeni kwa wabunge wote kuungana bila kujali vyama vyao. Huku nje nako wananchi bila kujali tofauti za itikadi za vyama vyao nao pia wakaungana kutaka kujua ukweli wa mambo. Kwa kiasi fulani ukweli huo ulionekana kwa baadhi ya watuhumiwa kuachia madaraka, kwani walioachiwa madaraka Bw. shy ni wapinzani? ila waliachia madaraka kutokana na hoja za kweli na za msingi zilizowasilishwa na Watanzania wenye uchungu na nchi yao ambao wewe suala la upinzania limetawala bichwa yako.

Ukiwa nje ya nchi, unahitaji kujua yanayotokea nyumbani. Ukitaka kujua ukweli wa mambo pata habari kutoka pande zote, hapa ni kwamba waliopo kwenye system wanakwenda nje na wanaongea na waTZ walioko huko hali kadhalika na wapinzania wanaongea nao. Kwa vile walio nje nao wanaufahamu wao wanachuja mbichi na mbivu.

Nisingependa kwenye masuala ya msingi Bw. Shy uingize ubaguzi. Ni ubaguzi huu huu ambao unaweza kudhoofisha mshikamano ambao 'automatic' umeibuka miongoni mwa wa TZ kutaka kulinda raslimali za nchi kwa faida ya nchi na vizazi vijavyo. Suala la nani mkweli na katoka chama gani hapa halina nafaisi. Tunachotaka umeambiwa na waliotangulia 'Aluta contunue -mpaka kieleweke'.
 
Wazee hawaongei hovyo hadharani. Hawa ni statemen, chukua muda, kaa nao utapata mengi mengi sana. Ni wale tu ambao hawataki kuheshimu uzoefu na kazi ambayo wazee hawa wamefanya ndio atataka kuwalaumu na kuwasuta. Hawa hawawezi kwenda MAELEZO kusema kama Zitto au Mnyika etc, hawa wanasema kikubwa kwa tahadhari na ukipata fursa kuwa nao unajifunza mengi sana na unaweza kuyasema 'with authority'. Tuwaelewe wazee wetu na tuwe fair kwao!


wakati fulani niliwahi kukaa na mzee Peter siyovelwa pale Ettien Hotel karibu na Nyumba ya "zamani" ya Mkapa kwa kweli wana mambo makubwa sana mbali ya udhaifu wao wa kibinadamu walio nao!
 
You are either with THE PEOPLE OR NOT!
Ilikuwa vipi akapigiwa kura za ubunge na CCM kule bungeni? badala ya kutegemea kura za wapinzani wenzake?

Kura za wapinzani pekee zingetosha kumfanya awe mbunge wa East Africa? tuwe reasoable kidogo jamani!
 
Nakumbuka hadithi ya Prince Bagenda na Mabere Nyaucho Marando walipoenda Rufiji na kulala katika kitanda cha kamba. Watu wazima 2 kitanda kimoja. Kitanda kikakatika na wote kuanguka. Walikuwa katika kueneza vyama vingi. Wakati ambao ulikuwa ukihubiri vyama unaonekana kichaa na watu wanakaa kuleeeeeeeeeee!

Lakini kwa ushujaa wa akina Mkwawa, Isike, Mazengo, Kinjikitile na wengineo!

tukijifunza kufikiri kimantiki basi kutakuwa hakuna haja ya kuwa na malumbano mareefu yasiyo na maana, kwani kwa vyovyote vile kila jambo litapimwa kwa kutumia mizani ya fikra pevu

wanaomshutumu Zitto kwa Hadithi hii wananikumbusha kadhia iliyomkumba Barack Obama pale aliposema anashindwa kwenda kuomba kura kwa wakazi wa Pennslivania kwa sababu ni "wachungu" they are bitter!

Basi wakatokea watu wakamshambulia Obama akiwemo na mpinzani wake toka chama pinzani cha Republic. BW. Mccain na yule wa democratic Hilary Clinton. Lakini Obama akawauliza wapinzani wake kimantiki maswali yaliyowatoa ulevi wa malumbano yasiyo na maana.

Hivi ni nani kati yetu anayekwenda vijijini na kulala kwenye kitanda cha kamba "teremka tukaze" tena kisicho imara achilia mbali kwa kuimarisha chama cha siasa,hata tu kuwaeleza wananchi wa vijijini wapi yalipo masoko ya mazao yao?
 
Kuna mahali watanzania tumekwama na tusipoondoka hapo basi hakuna jinsi ya kuondokana na CCM.na kila mara tutakuwa ni makasuku wa kuimba propaganda za CCM za nani ni msaliti na nani ni pandikizi ndani ya upinzani

wakati CCM ikichukua mtu toka vyama vingine wanasema anarudi nyumbani sisi tunawaita kina marando wasaliti,kwa nini tusiwapime watu kwa matendo yao kuliko kulishwa propaganda na CCM kwamba watu hawa ni wasaliti?
 
Upinzani ni dhana na wala si vyama vya siasa, kama dhana hii itajengeka ndani ya mioyo ya watanzania basi ni hakika hakuna chama kitakachotuchezea hata kama CCM iking'olewa madarakani
 
hofu yangu ni kwamba watu wanataka kufanya vyama vya siasa ndiyo upinzani jambo ambalo naamini siyo sahihi. tuchukue upinzani kwa mfano wa pombe ya Gongo.

Gongo ikiwa ndani ya Chupa ni gongo,au ikiwa ndani kibuyu ni gongo, hata kama ikiwekwa kwenye madhabahu, bado itakuwa ni gongo.kwa hiyo Upinzani ukiwa toka ndani ya vyama vya siasa ni upinzani au wa Mwanamke kukataa kunyang'anywa nyumba ya urithi na ndugu wa marehemu mume wake,nao pia ni upinzani!

kwangu mimi upinzani ni uasili (nature) ndiyo maana kuna wanawake na wanaume,kuna weusi na waupe lakini pia kuna binadamu na kuna wanyama au binadamu wenye hulka za kinyama!
 
kuna hoja za msingi watu hatutaki kuzijadili lakini hizo ndizo zitajenga upinzani imara hapa nchi kwetu. Tujiulize maswali kama vile Upinzani ni nini na kama jee ili nchi yetu iendelee inahitaji vyama vya aina gani vya upinzani.

pia waliomo kwenye hivyo vyama wajitahidi kukubali siyo wao tu ndiyo wenye hatimiliki ya upinzani katika nchi yetu,wawe wanakubali kukosolewa na watu wengine.
 
KWA KWELI SHY HUJATOA PICHA HALISI YA UNACHOSEMA.
BINAFSI NINA SWALI LA KUKUULIZA.
1. SERA YA UFISADI UNASEMA IMEPITWA NA WAKATI, JE ILISHAPATIWA UFUMBUZI? UPI?
2. UNAPOSEMA SERA NI ZILE ZILE, ULITAKA WASEME SERA MPAYA KILA MWAKA HATA KAM WALICHOKUWA WAMESEMA SIKU ILIYOPITA HAKIJATEKELEZWA?
3. NINGEPENDA KUJUA NANI MVURUGAJI WA NCHI ANAYEIBA AU ANAYESEMA JUU YA WIZI WA MWINGINE?
4. MTIHANI WA MAELEWANO NI KATI YA NANI NA NANI? KAMA NI CCM NA CUF KWA NINI WAWE CUF PEKEE YAO WA KULAUMIWA KUWA WAMESHINDWA MTIHANI WA MAELEWANO? WATAELEWANA NA NANI KAMA CCM HAWATAKI KUELEWANA WANATOKA NJE YA MKUTANO NA KUANZISHA AJENDA MPYA?

POST YAKO INALETA MASWALI MENGI ZAIDI KULIKO MAJIBU. LAKINI HONGERA KWA KUWA MPINZANI WA UPINZANI
 
Of course mtu (mtanzania) yeyote anayefikiri maisha ni yeye tu na hataki kutoa mchango wowote katika kuifanya jamii anamoishi iwe bora zaidi ni msaliti.

Lakini inabidi tuelewe na tukubaliane pia kwamba katika kutoa mchango wako sio lazima utoe kwenye siasa. Kuna watu kibao ambao hawajulikana wanalilisha taifa kwa kulima mahindi, n.k., kuna wanaofundisha, kuna wanaosaidia wagonjwa wetu mahospitalini, kuna wengine wako America, Europa na kwingineko wanatoa mchango wao wa hali na mali huko nyumbani, hawa nao wanasaidia jamii yetu. Kuna wanasanaa wetu wetu wazuri sana kila Jumamosi wanafurahisha na kuburudisha watu pale Mango Garden na kwingineko, hawa pia wanatoa mchango bila kuwasahau Ze Comedy.

Sasa tusiwe vipofu wa kufikiri kwamba mchango au mafanikio yanapatikana kupitia siasa tu! Mawazo kama haya ndiyo yanawafanya baadhi ya wataalamu wetu ambao hawakuwahi kufikiri kuwa wanasiasa kukimbilia kwenye ubunge ili nao waonekane wanatoa mchango katika jamii.
 
Kitila, nadhani Zitto alikuwa anazungumza katika kuangalia kwa ufinyu wa mwanga wa kisiasa na siyo kujumuiya kila kitu.
 
Atazunguka nchi nzima ya Australia au Cambodia, au kokote aliko anakosoma?

Mimi naomba unijibu kama Zitto nae kaharibu na faux pas yake ya 'wasaliti ni wananchi...'

Ni wapi ambapo Zitto amesema haya? mbona mzee mzima unataka kujiabisha tena siku za malipo (pay days) kama ijumaa ya leo?
 
Kitila, nadhani Zitto alikuwa anazungumza katika kuangalia kwa ufinyu wa mwanga wa kisiasa na siyo kujumuiya kila kitu.


I know. Lakini si umeona kuna watu wanawalaumu wenzao na kuwaona sio wazalendo kwa sababu wanaishi America na hawajashiriki siasa za moja kwa moja? Sasa kweli tunataka kusema kila mtu arudi nyumbani akawe mwanachama wa vyama vya upinzani ndio naye aonekane anatoa mchango katika jamii? That said, my comment was general and simply a note of warning and caution that there are many valuable things going on in our society other than and beyond politics!
 
I know. Lakini si umeona kuna watu wanawalaumu wenzao na kuwaona sio wazalendo kwa sababu wanaishi America na hawajashiriki siasa za moja kwa moja? Sasa kweli tunataka kusema kila mtu arudi nyumbani akawe mwanachama wa vyama vya upinzani ndio naye aonekane anatoa mchango katika jamii? That said, my comment was general and simply a note of warning and caution that there are many valuable things going on in our society other than and beyond politics!

Kitila Mkumbo una sound kama mtu mwenye busara sana!
Safi sana mkuu!
Hata kama kuna nyakati tumekuwa tukipingana ie kwenye issue ya Obama..Bado huwa na respect sana mawazo yako mkuu.
 
Halafu bado kuna vurugu nyingine wanaiendeleza kwenye thread ya upinzani Tanzania bado!
 
Hata kama kuna nyakati tumekuwa tukipingana ie kwenye issue ya Obama..Bado huwa na respect sana mawazo yako mkuu.

Hii ndio raha mojawapo ya kuwa binadamu: kutofautiana. Tukifanana mawazo humu ndani hii forum itaboa sana. Nami nafurahia sana michango yako hasa challenge na maswali yako hasa kwa opposition. Keep up the good work.
 
Upinzani ni dhana na wala si vyama vya siasa, kama dhana hii itajengeka ndani ya mioyo ya watanzania basi ni hakika hakuna chama kitakachotuchezea hata kama CCM iking'olewa madarakani

Ninakubaliana na usemi huu, lakini ni lazima pawepo na uongozi (presumably kutoka katika vyama vya upinzani na asasi za kijamii) wa kuamsha na kuendesha (to direct) dhana hiyo. Kwa hali iliyopo sasa, viongozi hawa wamekuwa nadra sana. Ndio maana hata CCM wanapovuruga, hakuna anayetumia uvurugaji huo kuwaonyesha wananchi njia mpya.
 
wapinzani wetu na degree zao FEKI


ca31.jpg


j6.jpg
 
Back
Top Bottom