Upi ni uhusiano wa Marekani na Misri

Mwita Matteo

JF-Expert Member
May 16, 2010
216
55
Baada ya Marekani kusitisha msaada wake kwa Tanzania kupitia MCC, kumeibuka mijadala mikubwa sana, kuhusu uhalali wa Marekani kufanya hivyo, na ni kiasi gani Tanzania kama inchi inaweza kuathirika na uwamuzi huo wa Marekani. Sababu kubwa za wamerakani kusitisha msaada huo zimeelezwa kuwa ni ni; kusikitishwa na swala la Zanzibar na Serikali kutositisha matumizi ya sheria ya makosa ya kimtandao au kutoifanyia marekebisho ili iendane na ulinzi wa haki za raia na uhuru wao wa mawasilianoi, Marekani imebaini kuwa Tanzania imeendelea kuitumia sheria hiyo mbaya kukandamiza uhuru wa wananchi kimakusudi (kama ilivyoelezwa na Mchambuzo Mtatiro J). Wachambuzi mbalimbali wa maswali ya kisiasa na uchumi wamechambua kuhusu swala hilo na wakatoa mitazamo yao kuhusiana na sakata hilo. Mmoja wa wachambuzi hao akiwa bwana Polepole, pamoja na uchambuzi wake mzuri na wakina ila kuna ufafanuzi alioutoa ulikua si sahihi kwa mtazamo wangu hasa aliposema, “kama mrudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo basi Marekani isingekua inatoa zaidi ya dola 3 bilioni kila mwaka kwa Misiri iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Misiri na Israeli.” Kimkakati, kisiasa na kiuchumi Marekani wanahaki kuendelea kuisaidia Misiri zaidi ya Tanzania. Katika makala hii nitaangalia uhusiano uliopo kati ya Misiri ya Marekani ili kuweza kuthibitisha ni kwanini Marekani inaendelea kuikumbatia Misiri japo Misiri haina rekodi nzuri ya demokrasia na utunzaji haki za binadamu.


Marekani imeanza uhusiano na Misiri kabla ya mwaka 1882, wakti huo Misiri ikiwa chini ya himaya ya Ottman na baadaye ikawa chini ya wingereza (1882-1945). Japo mahusiano hayo hayakua makubwa na imara.


Rais Gamal Abdel-Nasser (1952-1970) aliutia nyongo uhusiano huo pale alipoamua kukumbatia sera za Urusi na kuipinga Israeli. Pamoja na hayo Marekani iliendelea kumsaidia Nasser kusalia madarakani kwa kuwalazimisha waingereza na wafaransa kukomesha uvamizi wao mwaka 1956. Sera ya marekani imekuwa ni kuwasaidia madikteta wa Misiri wanaolinda maslai ya Marekani na Israeli katika eneo la uarabuni, na hili limethibitika wazi kwa maraisi Anwar Sadat (1970-1981) na Hosni Mubaraki (1981-2011)


Mwaka 1956, Marekani iliiingiwa hofu pale Misiri ilipoanzisha uhusiano wa karibu na urusi, kitu kilichopelekea Marekani kuanzisha OMEGA Memorandum kama mkakati wa kumpunguzia nguvu na ushawishi Rais Gamal Abdel Nasser katika eneo la Uarabuni.


Baada ya vita kati ya Waarabu na Waisraeli mwaka 1973 sera za mambo ya nje za Misiri zilianza kubadilika nahii ni baada ya mabadiliko ya uongozi kutoka kwa Nasser aliekua na msimamo mkali na mfuasi wa sera za kijamaa kwenda kwa Anwar Sadat aliekua na msimamo wa wastani na mfuasi wa sera za kimagharibi. Kuibuka kwa mchakato wa mazungumzo ya amani kati ya Misri na Israeli, Sadat aling’amua kuwa kufikia makubaliano ya a amani kati ya waarabu na waisraeli ni moja ya kigezo cha kuiletea maendeleo Misri.


Tarehe 28/4/1974 kwa kuendena na sera za mambo ya nje za Marekani, Sadat akifanyakazi na Rais wa Marekani wa wakati huo Richard Nixon waliwafukuza wafanyakazi na wanajeshi 20,000 wa kisovieti na wakaufungua mfereji wa Suezi.


Kufuatia mkubliano ya amani kati ya Misri na Israeli kati ya mwaka 1970 na 2003, Marekani imeisidia Misiri kiasi cha dolla billion 19, kama msaada wa kijeshi na kuifanya Misiri kua nchi ya pili ambayo sio mwanachama wa NATO kupata msaada mkubwa wa kijeshi baada ya Israeli. Pia Misiri ilipokea kaisi cha dolla bilioni 30 kama msaada wa kiuchumi.


Mwaka 2009 Marekani iliipatia Misiri msaada wa kijeshi wa dola 1.3 bilioni na dola 250 milioni kama msaada wa kiuchumi. Ikumbukwe kuwa Misri na Israeli ni washirika wakubwa wa Marekani ambao sio wanachama wa NATO.


Ushirika wa kijeshi kati ya Misiri na Marekani ni kipengele cha muhimu cha kimkakati kwa Marekani. Misiri inangaliwa kama kiungo muhimu cha Marekani na nchi za mashariki ya kati. Misaada ya Marekani kwa Misiri kiutawala na kiuchumi huangaliwa kama kitendo cha Marekani kujitanua na kuendelea kujipatia malighafi ya mafuta katika Ghuba ya Uajemi na kuendelea kuutumia mfereji wa Suezi kama njia muhimu ya kusafirisha sio tu mafuta bali manoari zake za kijeshi zinazofanya kazi kati ya bahari ya mediteraniani na bahari ya hindi au ghuba ya Uajemi. Misiri kijeshi ni nchi ya kwanza barani Afrika na ya pili katika Mshariki ya kati baada ya Israeli.


Tukingalia kwa kina uhusiano uliopo baina ya Misiri na Marekani, ni dhahiri Marekani wanakila sababu ya kuing’ang’ania Misiri na kuitosa Tanzania, na tukumbuke Marekani hii hii iliambiwa na baraza la umoja wa Mataifa waichukue Tanganyika kama koloni lake baada ya vita ya pili ya dunia na walikataa, ila kwa miaka mingi hata kabla ya vita ya pili ya dunia walishaonesha kila dalili za kuimendea Misiri.
 
Back
Top Bottom