Upepo gani mbaya umeukumba mji huu?

Giro

JF-Expert Member
Feb 9, 2009
359
22
Kilwa: Mji wa kihistoria uliodorora

Kwa wanaofuatilia historia ya nchi hii, Kilwa si jina geni masikioni mwao hata kidogo. Hiyo inatokana na ukweli kwamba mji huo una umaarufu mkubwa kihistoria pengine kuliko miji mengine ya Pwani ya Afrika ya Mashariki, ikiwamo Dar es Salaam.

Ukibahatika kusoma historia ya eneo hilo, kama ni mdadisi au mtu asiyependa kupitwa na jambo, basi, utatafuta kila njia uweze kutembelea eneo hilo. Eneo ambalo umuhimu wake wa kibiashara ulianza kushamiri tangu karne ya 9.

Kwa wasiofahamu eneo hilo, Kilwa ni moja kati ya wilaya sita za Mkoa wa Lindi. Kwa upande wa Kaskazini wilaya hiyo imepakana na Mkoa wa Pwani, Kusini imepakana na Wilaya ya Lindi Vijijini na upande wa Magharibi, imepakana na Wilaya ya Liwale.

Tofauti na Wilaya nyingine, Kilwa ni eneo ambalo limekuwa kivutio cha watu wengi kwa miaka mingi. kutokana na utajiri wa maliasili kama vile wanyamapori, misitu na mazao ya Bahari. Kwa miaka ya hivi karibuni, pia katika eneo hilo kumegundulika gesi asilia pia hivi sasa utafiti wa mafuta unaendelea katika eneo hilo.

Utajiri wa eneo hilo, ulikuwa kivutio cha wageni kutoka nje tangu miaka mingi iliyopita.Umaarufu wa eneo hilo si kwamba ulikuja baada uvamizi wa wageni, bali ulikuwapo hata kabla ya uvamizi huo.Hata hivyo, umaarufu wa Kilwa ulianza kushamiri kwa kasi tangu karne ya 13 na kushamiri zaidi katika karne ya 15.

Katika kipindi hicho, eneo la Kilwa lilikuwa mji wa kibiashara, hasa biashara za nje ambazo zilihitaji sana usafiri wa baharini. Eneo hilo lilikuwa kituo muhimu kwa wafanyabiashara wa maeneo ya ndani na wafanyabiashara wa kigeni waliokuwa wakitumia bahari kusafirisha bidhaa katika maeneo ya Uarabuni, India na China.Ilifika kilwa kuwa na sarafu yake.

Biashara zilizokuwa zimeshamiri wakati huo ni pamoja na vipusa, pembe za ndovu, na magamba ya kobe. Bidhaa hizo zilikuwa zikibadilishwa na nguo na vyombo vya udongo zilizokuwa zikitoka nchi za Mashariki ya mbali.Mji mkongwe wa Kilwa Kisiwani ulikuwa maarufu sana kutokana na utamaduni wa Kiswahili ambao ulikuwa umeota mizizi kwa wakati huo.

Utamaduni huo ulikuwa ukisifika kila kona za dunia kupitia wafanyabiashara wa kigeni waliokuwa wakitumia bandari ya Kilwa kama kituo muhimu cha kusafirishia bidhaa na Watumwa.Aidha, Kilwa Kisiwani, lilikuwa eneo muhimu kuelekea katika makazi ya wafanyabiashara katika visiwa vingine kama vile Sanje na Songo Mnara.

Wakati huo, eneo hilo liligeuzwa kuwa kituo kikuu cha kukusanyia Watumwa. Watumwa hao walikuwa wakichukuliwa katika maeneo ya kandokando ya mto Nyasa kabla ya kusafirishwa kwenda Mauritius, Uarabuni na India.

Pia Wafanyabiashara walikuwa wakinunua mchele, mpira na tumbaku. Bidhaa hizo zilikuwa zikipatikana kwa wingi katika maeneo ya Pwani.Mnamo Karne ya 19, eneo la Kilwa Kivinje lilijipatia umaarufu mkubwa kutokana na bandari bora ya mashua za kusafirishia bidhaa kwenda ng’ambo.

Sehemu hiyo iligeuzwa kuwa kituo kikubwa cha kukusanyia na kuuzia Watumwa waliokuwa wakikusanywa katika maeneo ya Kusini mwa nchi.Kutokana na biashara kushamiri katika eneo hilo, mwaka 1850, idadi ya watu ilianza kuongezeka. Wakati huo kulikuwapo na wastani wa watu 1500, wengi wao wakiwa wafanyabiashara wenye kipato cha juu.

Kwa kuwa eneo hilo lilikuwa limejengeka, Wajerumani walipoingia nchini mwaka 1886, walilifanya eneo la Kilwa Kivinje kuwa Makao Makuu ya Utawala wao.
Wajerumani walitumia eneo hilo kama kituo muhimu cha kupanga mikakati ya mapambano wakati wa Vita ya Majimaji. Vita hiyo ilishika kasi katika milima ya Matumbi iliyopo Kaskazini mwa wilaya hiyo.

Pia eneo hilo lilikuwa Kituo cha Kunyongea Watumwa waliokuwa wakikaidi amri ya kusafirishwa.Hata hivyo, wakati wa ukoloni wa Waingereza, makazi mapya yalijengwa katika eneo la Kilwa Masoko. Waliligeuza eneo hilo kuwa bandari mpya kutokana na kina kirefu cha maji katika pwani ya eneo hilo.

Tukiachana na hitoria hiyo, hivi sasa ukifika Kilwa, umaarufu wa eneo hauendi sambamba na ukuaji wa sekta ya utalii katika eneo hilo.Ingawa kulikuwapo kisingizio cha ubovu wa barabara iendayo katika mikoa ya Kusini, katika wilaya hiyo sekta ya utalii bado ipo nyuma ikilinganishwa na maeneo mengine.

Mabaki ya nyumba za Wakoloni hivi sasa ni makazi ya watu wenye kipato cha chini na mapango ya wahuni badala ya kutumika kama kivutio cha watalii.Pamoja na eneo hilo kuwa na historia ya kuvutia ni nadra sana kukutana na watalii wakivinjari katika mji huo mkongwe.Ni ukweli usiopingika kuwa Kilwa imedorora. Kilwa haivutii kama historia yake inavyovutia
 
Sababu kubwa Kilwa wameikataa CCM na utawala wake ,sasa wanalolipata Kilwa ni mapigo ya CCM kama inavyopatiwa Pemba ,msishangae popote pale ambapo utawala wa CCM hautakiwi basi hawapewi fungu la maendeleo kwa maana huduma zote zitolewazo na serikali zitadorora kwa mifano hai angalia zile sehemu ambazo CCM ilipata kibano ndio utaona kuwa hawa jamaa waliopo madarakani wanajaribu kupeleka maendeleo kwenye zile sehemu ambazo hazikuonyesha waziwazi kuikataa CCM.
 
kilwa,was the first town on the east coast of africa to mint its own coin.Vasco da gama made a stopover in kilwa to restock his supplies.how kilwa has dwindled,defies all belief
 
Tourism Tz ni ktk Northern Zone na Visiwani..ni kutokana na miundombinu mizuri na kuchangamkia tenda watu wa huko!

Ukiangalia mapato ya TANAPA over 30% pekee hupatikana kwa wapanda Mlima K'njaro!

Hata Tanga pamoja na miundo mbinu kuwa ok watalii bado wachache sana!

Sababu sijui ni uswahili wa watu wa haya maeneo au kukusekana kwa mahoteli n.k

Tz ingeamua tu tukawekeza ktk Utalii tu we have so much potential yaani Kilwa, Tanga, Mbuga za wanyama n.k
 
Back
Top Bottom