UPDATES: Yanayojiri Bungeni Dodoma, Leo tarehe 16 Juni 2014

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,782
336
Mambo muhimu yatakayojiri bungeni ni kama ifuatavyo:
1.hati za kuwasilisha mezani.
i.mwenyekiyi wa kamati ya bajeti amewasilisha ttaarifa ya kamati a bajeti juu ya hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2013 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2014/015
ii.msemaji mkuu wa kambi ya upinzani wa ofisi ya rais mahusiano na uratibu amewasilisha taarifa juu ya hali ya uchumi wa taifa 2013 na mpango wa maendeleo wa taifa 2014/015
iii.msemaji mkuu wa kambi ya upinzani wa wizara ya fedha amewasilisha taarifa juu ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/015

2.maswali
kipindi cha maswali kwa serikali kutoka kwa wabungevkinaendelea hivi sasa.

3.hoja za serikali
wizara ya fedha...kwamba bunge likubali kujaili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka 2014/015.....majadiliano yataendelea baada ya kipindi cha maswali kumalizika....

fuatilia uzi huu kwa updates....

===updates
swali la kwanza limeulizwa kwa waziri mkuu na mh nyambari nyangwine mbunge wa tarime.
kwamba ukosefu wa hati miliki za kimila vijijini unasababisha migogoro mingi ya ardhi kwa jamii.
i.je serikali kwann haitoi hati miliki za kimila?
ii.je, serikali ina mpango gani wa kupima miji midogo ya nyamongo,sirari,nyamwaga na komasqa ili ijengwe kwa mpangilio mzuri?
iii.je, kwann serikali haiushirikishi mgodi wa north mara kupima miji ya nyamongo na nyamwaga ambayo huhudumiwa na mgodi huo.
naibu waziri wa tamisemi anaendelea kutoa majibu ya serikali.

====Updates
2.ofisi ya makamu wa rais mazingira imeulizwa kwamba, mlima kilimanjaro ni kati ya maajabu makubwa ya dunia,je serikali na jumuiya za kimataofa zimechukua hatua gani kunusuru mlima huo na maeneo ya vijiji jirani? Je ni kiasi gani cha theluji kimepungua?
waziri anaendelea kujibu.

===Updates..swali kwa wizara ya afya.
mh elizabeth batenga anauliza...kwmba wizara ya afya ndio yenye dhamana ya kulinda afya za wananchi kwa kutoa matibabu bila kujali kipato/uwezo cha mtu, lakini cha kusikitisha wananchi wanajitokeza kuomba misaada kupitia vyombo vya habari kama vile tv na rdio, je serikali inasemaje katika hili?
waziri anazitaka halmashauri za wilaya kuhamadisha wananchi kujiunga ktk mfuko wa bima ya afya ili waweze kupatiwa matibabu kwa utaratibu rahisi

===updates
Mh. luckson mwanjale anauliza kwa wizara ya mambo ya ndani.
tarafa ya isangati iliyopo mbeya vijijini haina kituo cha polisi hata kimoja huku ikiwa na wakazi wanaozidi 100,000...hivyo wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo....serikali ina mpango gani ktk hili??
Waziri anasema bajeti imetengwa mwaka huu kujenga vituo vitano ktk maeneo tofauti ndani ya tarafa hiyo

===more updates
mh amina mwidau anaiuliza wizara ya kilimo,chakula na ushirika, serikali ina mpango gani na mashamba ya mkonge yaliyopo wilaya ya tanga na pangani ambayo yametelekezwa,hayazalishi tena mkonge na sasa ni mapori tu....waziri anasema serikali inaenda kufuta hati miliki na kuwarudishia wananchi

====updates
paul lwanji wa manyoni maghatibi anaiuliza wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia...serikali imeshindwa kutekeleza ahafi yake ya kuzishawishi kampuni za simu kuweka minara katika kata ya mwámagembe? Na je kuna ubaguzi ktk hili?
waziri anajibu kwamba hakuna ubaguzi na serikali inaendelea na ushawishi kwa makampuni ya simu kuweka minara eneo hilo na pa serikali hivi sasa imeamua kuifanua kazi hiyo na si kutegemea makampuni

===updates
muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2014 umesomwa kwa mara ya kwanza ......
===Updates
muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2014 (the finacial bill, 2014 umesomwa kwa mara ya kwanza....


-_---======mwenyekiyi wa kamati ya bajeti mh andrew chenge anawasilisha taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti kwa mwaka 2014/015
====change anasema kuna udhaifu mkubwa kwenye ofisi a mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
chenge anashauri serikali ibuni vyano vya maana vya kodi na siyo kuishia kutegemea kodi kwenye juice, soda na bia.
====kwamba serikali ianzishe kukopa fedha kwny vyanzo mbalimbali vya ndani na kuwa na cash bajeti badala ya kutegemea wafadhili wa nje

===updates
kamati a chenge inasema kuwa serikali idhibiti nidhsmu ya matumizi fedha za umma ili kuwe na tija kwa ukuaji wa uchumi wa nchi
===anahitimsha taarifá yake kwa shukran kwa watu mbalimbali waliotoa ushirikiano kuandaa hotuba hiyo.

===msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa ofisi ya rais mahusiano na uratibu esther matiko anawasilisha maoni ya wapinzani....yaelezwá kuwa hajawahi kuwasilisha maoni mbele a bunge,ni mara yake ya kwanza.....
===mh matiko ameanza kwa kumshukuru mume wake,watoto na famila yake kumta nguvu na moyo ktk majukum yake ya kichama na kibnge.

===updates

===mh matiko analálamika kuwa ccm imeshindwa kuwaletéa wananchi maendeleo na imeshindwa kuwatoa watz ktk umaskini....
===kwamba nchi ina rasilimali nyingi lakini watu wake wanazidi kuishi kwenye dimbwi la umaskini tena chini ya mstari wa umaskini...below poverty line

===updates
mh. Analálamika kuwa taarifa za wizara ya fedha zimejaa takwimu zisizo sahihi kwani wanasema hawajapokea fedha kutoka kwa wafadhili huku wakihadaa wananchi kuwa wametekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 90.
=== anakosoa mfumo wa utoaji elimu hapa nchini ambapo wahitimu hawaendani na mahitaji ya soko la ajira

==+=+=more updates
mh james mbatia msemaji mkuu wa kambi ya upinzani anawasilisha maoni ya upinzani kwa wizara ya fedha hivi sasa, anaanza kwa salaam za aadhimisho ya siku a mtoto wa afrika na pia kwa watoto wake wawili wa kuwazaa...anamshukuru mbowe kwa kumteua kuwa msemaji wa wizara hiyo

===mbatia anasema serikali imeshindwa kusimamia ipasavyomapato ya serikali
===anapendekeza mafao kea wazee wote nchini
=== deni la taifa linazidi kuumiza taifa kwani linaongezeka kila uchao....
......mbatia anasema kuwa mananchi wa rombo wana upungufu wa nguvu za kiume na mbunge wao anajua...hili liesababishwa na matumizi a gongo ....mbatia anaendelea
 
===Updates
muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2014 (the finacial bill, 2014 umesomwa kwa mara ya kwanza....

-_---======mwenyekiyi wa kamati ya bajeti mh andrew chenge anawasilisha taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti kwa mwaka 2014/015
 
Chenge anasema Serikali ina madeni makubwa sana kitu ambacho siyo kizuri
 
Chenge: Serikali imekosa ubunifu haitaki kupokea ushauri juu ya vyanzo vipya vya mapato. Imekuja na vyanzo vilevile sigara, bia, juisi na soda.
 
Mzee wa vijisenti ndo kamaliza kuwasilisha maoni ya kamati ila kaichana serikari waziwazi..!!
 
Chenge anasema Serikali ina madeni makubwa sana kitu ambacho siyo kizuri

Mzee wa vijisenti haoni kama anajidhalilisha kuishambulia serikali juu ya madeni wakati na yeye amechangia kuidhoofisha serikali kifedha kupitia kashfa yake ya rada?
 
Namuona mbatia anawakilisha

HOJA KUU
1. Shukrani
2. mapitio ya bajet iliyopita
3. deni la taifa juu
...........................

4. matumiz ya serikar na uhalisia wa makusanyo haviendani
 
Naona asilimia kubwa wanapiga story tu hata hawako makini nini kinasemwa.
 
Akichangia hotuba ya Wizara ya Fedha Bungeni leo mchana, Mbunge wa Tarime Bw Nyambari Nyangwine ameishangaa serikali kwa kuendelea kuwakumbatia wawekezaji huku ikifahamu kwamba wawekezaji ni wezi. Baada ya Nyangwine kumaliza kuchangia, Mbunge Lucy Owenya alimtaka kuthibitisha kauli yake ambapo mbunge huyo, bila kumumunya maneno, alisisitiza kauli yake kwa kusema kwamba wawekezaji wanaokumbatiwa na serikali ya CCM ni wezi na ndio wamechangia kutufikisha hapa tulipo.

Aidha, akiendelea kuchangia, mbunge huyo wa Tarime aliitaka serikali iwaeleze wananchi ni kwa nini kila siku watanzania wanaambiwa kwamba uchumi unakuwa wakati hawana kitu mifukoni mwao. Ameiomba serikali iache kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwalaghai kwamba uchumi unakuwa wakati kila kukicha maisha yanzidi kuwa magumu.

MAONI YANGU
Kumbe wakati mwingine wabunge wa CCM wakijitoa akili husema ukweli. Naomba wabunge wengine wa CCM wawe na ujasiri wa kuwaambia wananchi ukweli, hata kama kuna baadhi ya makada ambao hawapendi wananchi kuambiwa ukweli.

Source: TBC
:yield:
 
Nyangwine hana njaa kama wengine ndio maana anaweza kutamka hayo aliyoyatamka .

Huyu jamaa safi sana ameweka kila kitu hadharani na lile la wenzetu 10000 kupigwa na jua kutwa nzima kisa ajira 70.Mimi ninaamini kuna siku mungu ccm ataangamia kama miungu mingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom