Updates: Simba SC vs Yanga SC Uwanja wa Taifa

Mimi jaguar ni yanga damu,bravo and congrats to you simba,you deserve this massive victory,(kupanda kwa simba kushuka kwa yanga and vice versa)^-1.

Thanks Jaguar. Hata hivyo ujue kuwa raha ya Simba na Yanga ipo pale timu zote zinapokuwa strong. Hivyo tunataraji kuwa baada ya kichapo cha leo Yanga watajipanga ili tuendelee na utani wetu kwa idadi ya magoli yenye heshma kama 2-0, 3-0, 1-0 etc. Siyo 5-0, 6-0.
Vinginevyo utani utakosa maana au utahama na kuwa kati ya Simba na Azam.
 
Duh! Kipigo hiki cha aibu sana. Sijui hivi vipigo ( 6-0, 5-0) tutavilipiza lini.

Ila nitajua kuwa nyinyi Simba wa ukweli kama mtatoa kipigo hicho kwa hao Wasudan (Al-Ahly S.) kwani mpaka sasa hamna lolote mmesaidiwa na kamgogoro kanakoikumba timu yetu, vinginevyo mgepata kichapo cha mbwa mwizi (kauli za mtani).
 
Balatanda,yahoo naomba matokeo ya simba na Yanga..kama kuna mwingine anaweza kunijuza....
 
Balatanda,yahoo naomba matokeo ya simba na Yanga..kama kuna mwingine anaweza kunijuza....
Are you serious????....

Kuna tofauti kubwa sana kati ya Bala na Yahoo.....

Bala Is Always Here............ na huwaga sina Ushabiki Maandazi,daima nakubali kushindwa na natoa Pongezi panapostahili.....Na tayari nimefanya hivyo(angalia post na. 217).

Dah!!!.....

Hii ni FEDHEHA sasa.....

Watani hamna hata HURUMA kwa Mgonjwa?........Vibaya hivyo....

Btw....Tunastahili aina yoyote ya KIPIGO kutoka kwa SIMBA...

Hongereni sana Watani kwa ushindi huu mnono ambao utachagiza upokeaji wa Kombe la Ubingwa wa EPL.....

Kweli nimeamini(mwaka 2011/2012) aungurumapo Simba mcheza nani?........Tunajipanga nasi mwakani.....

Kila la heri katika CAF CL........

Tusinyimane mualiko na kadi ya sherehe ya UBINGWA jamani...

Bala.
 
Leo watani wameingia cha kike, bao 5 sio kubahatisha simba wanatisha, wamethubutu, wameweza na sasa wanasonga mbele kwenye mashindano ya kimataifa.
 
Niliambiwa kuwa mechi imeuzwa mapema kumkomoa Nchunga. Fitina nyingine HATARI sana
 
Ingawa nimefurahi Simba kumchapa Yanga, lakini 5-0 is too humiliating. Nasikitika kwa ajili ya rafiki yangu Balantanda na Jackbeaur.
Jipeni moyo wakuu, hayo ndio mambo ya uwanjani.
 
Miaka ile ya sabini (1976?), Yanga alipotundikwa 6-0, kulikuwa na mgogoro kwenye club ambao ulipelekea kuzaliwa kwa Pan African. Viongozi wa Yanga hawajawahi kujifunza athari za migogoro? Hii ni aibu kubwa sana kwa club. Japo siombei, club akisambaratika baada ya mechi hii, nitakuwa mmoja kati ya ambao hawatashangaa.
Usisingizie mgogoro, ni kiwango tu kipo chini. Kuna mgogoro gani utaushinda ule wa Yanga Asili na Yanga Kampuni? Mbona hamkufungwa 5 ?
 
Kati ya mashabiki wa Yanga ninaowahurumia ni Yahoo, CPU, kuna mwingine anatumia Id ya Polisi na yule jamaa wa kwenye you tube anayesema, Niyonzima kadi nyekundu, Canavaro kadi nyekundu, huu ni uzalendo, huu ni uzalendo kweli, poleni sana watani na hongera kwa washabiki wote wa Mnyama.
 
Back
Top Bottom