Update ya mkutano wa wanahabari na Mh. Magufuli

FILOMBE

Member
Mar 2, 2012
27
0
Habari wadau!

Nilisikia kuwa Mh. Waziri wa Ujenzi leo atafanya kikao na Wanahabari pale Idara ya habari maelezo kuanzia saa 3 asubuhi, please naombeni updates kwa mlio karibu
 
Habari wadau!

Nilisikia kuwa Mh. Waziri wa Ujenzi leo atafanya kikao na Wanahabari pale Idara ya habari maelezo kuanzia saa 3 asubuhi, please naombeni updates kwa mlio karibu

Mimi nlifikiri ww umehudhuria huo mkutano....
 
Habari wadau!

Nilisikia kuwa Mh. Waziri wa Ujenzi leo atafanya kikao na Wanahabari pale Idara ya habari maelezo kuanzia saa 3 asubuhi, please naombeni updates kwa mlio karibu

Kama uko kwenye huo mkutano naomba umpatie huu ushauri wangu. Anaweza kuuchukua au kuuacha. The ball is in his court
Huyu Dr. Magufuli kakurupuka. Nilimsikia akisema kwamba nchi nyingine allowable tonnes ni pungufu ya Tanzania. Tanaznia ndiyo tunaruhusu uzito mkubwa ie 56 tonnes. Ok that is fine, lakini ni yale yale ya Spika Makinda kuulizwa kitu kingine yeye anajibu kitu kingine.

Hapa kinachogombaniwa ni msamaha wa 5% kwa uzito uliozidi. Hivyo basi solution hapa ni kwamba kama anaona uzito wa 56 tonnes + 5% tolerance limit ni kubwa na unaharibu barabara zetu anachotakiwa kufanya ni kupunguza allowable 56 tonnes mathalani zikawa 51 tonnes + 5% tolerance limit kwasababu zifuatazo.

Kwanza mizani yetu haiwi CALIBRATED on time and on regular basis, hivyo reading ya mzani wa Kibaha ni tofauti na mizani ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tinde (Shy) na Usagara (MZA). Mimi nilishawahi kusafiri kwa bus from DSM-MZA na nilikaa mbele nikaona hiyo variation ya reading inavyotofatiana kutoka mzani moja na mwingine. (Uzito kwenye mizani unasomeka kwenye taa mbele and anybody can read it).

Pili kwa wale mliowahi kufanya biashara ya mbao. Ukapakia mbao zako mathalani kutoka Urambo, Tabora tonnes ziko sawa kabisa eg 54 tonnes. Mbao unazipeleka DSM. Bahati mbaya ukafika Singida mvua ikanyesha, mbao hizo zikalowa na maji ya mvua. Believe me kama mkifika Dodoma mkapima uzito, mbao hizo hazitakuwa tena na uzito wa 54 tonnes, zinaweza kuongezeka hadi 56.4 tonnes, sasa kama hapo hakuna tolerance limit ya 5% tayari utatakiwa kulipa faini. Na hapa ndiyo unaona UZURI wa kuwa na tolerance limit. Mimi (transpoter) sijaleta mvua. Lakini mvua imenyeshea mbao zangu, zimeongezeka uzito, hivyo hiyo tolerance e limit itanisaidia because it was not my intention kuzidisha uzito in the first place.

Kuna mtu hapo juu amesema kwamba Utafiti wa kisayansi uliofanyika ulionesha kwamba mizani yaTanzania ina Standard errors up to 4%. Sasa kwanini Magufuri adharau utafiti huo wa kisayansi na kufuta hiyo 5% tolerance limit. Uzito unaweza kuonekana umezidi kwasababu ya hiyo variation ya reading ya mizani yetu.

Politicians Wa Tanzania hata awe msomi vipi lakini mamuuzi yao hayafuati ushauri wa Wasomi hapo Dr. Magufuri ametokota!.
 
nimekuja mbio, najua nitapata updates wapi..............!!!:A S 39:
 
Magufuli ni janga popote pale ambako ametia mguu! Busara zero ana kebehi za makusudi akifikiri kuwa ni yeye pekee mwenye akili nyingi za kufikiri! bahati mbaya sidhani kama anaweza chukua ushauri wa wenzake wizarani! PAle alipowaambia wakazi wa Kigamboni kama hawawezi wapige mbizi ndipo nilijua huyu jamaa hana busara hata chembe! Waziri kuhalaralisha kufanya biashara ya vivuko badala ya kuwa huduma za kijamii!

Utakuta pale Ferry magari ya watoto wanaoenda shule yanalipa nauli kama vile ya wafanya biashara wakubwa. Hana utaratibu huyu jamaa na analysis ya impact kwake ilitoroka kichwani mwake alipoukwaa uwaziri!
 
Tatizo la magufuli ni dharau kwa hawa wamiliki wa malori,kuna kitu kiko wazi sana,barabara zetu zinajengwa chini ya kiwango cha kimataifa,barabara hazidumu sababu zinachakachuliwa,yeye kakariri tu kuwa wanaoharibu barabara ni wasafirishaji.

Kama barabara zote zingetengenezwa kwa kiwango kama cha barabara ya morogoro road inayotengenezwa sasa kwa ajili ya mabus ya mwendo kasi wala tusingesumbua na magufuli,isitoshe mabus mengi kwa sasa yanatoka nje kama YOTONG,MARCOPOLLO,SCANIA ETC na yote yanaviwango vya kimataifa,na kama barabara zingekuwa na kiwango cha kimataifa zisingeharibika kama ilivyo sasa.

Unaambiwa magufuli hajawahi kuitisha mkutano na wamiliki wa malori since awe waziri wa ujenzi,sasa matatizo yao atayajuaje kama hataki kukutana nao?
 
Kuna jambo moja ambalo sijui kama waziri wa ujenzi kaliona, kauli zake zilizosababisha mgomo wa wasafirishaji tatizo haliishii hapo, ndiyo maana wakati mwingine tunajiuliza kunapokuwa na kauli zinazokinzana kati ya waziri mmoja na mwingine katika serikali ile ile. Waziri anasema bila hofu kwamba kama madereva wakitaka kugoma wakapaki malori huko kwao na si barabarani. Tuangalie kwa ufupi athari za mgomo huu kwa mawaziri wengine na nchi kwa ujumla. (1) waziri wa fedha ajiandae kupanda mara moja kwa mfumko wa bei wakati mapato ya TRA yakishuka, (2) wananchi kwa ujumla wao wajiandae kupanda kwa bei ya vyakula nchi nzima kutokana na kukosekana kwa mafuta (3) waziri wa mawasiliano ajiandae na mlundikano wa meli zinazongoja kupakuwa bandalini,na meli zitakazopata bahati ya kupakuwa waziri ajiandae kutafuta eneo la kuhifadhi mizigo ambayo itakuwa inapakuliwa lakini haiondolewi bandalini (4) waziri wa afya ajiandae na vifo vya watu vitakavyotokana na ukosefu wa madawa katika hospitali hususani mikoani (5) waziri wa biashara ajiandae na upungufu mkubwa wa bidhaa madukani (6) waziri wa ujenzi naye pia ajiandae na miradi mingi ya ujenzi wa barabara kusimama kwa kukosa mafuta, vifaa vya ujenzoi nk (akumbuke tambo zake za kujenga barabara kilomita 11000 nchi nzima) (7) waziri wa kilimo aandae majibu kwa wakulima watakapokosa mbolea na pembejeo msimu wenyewe ndiyo huu, (8) waziri mkuu ajiandae na hasira ya wananvhi watakapokosa usafiri kwa sababu wenye mabasi wamegoma.

Listi hii ni ndefu na inamgusa karibu kila waziri na mwisho wa siku itamgusa hata Rais mwenyewe mambo yatakapokwenda kombo. Mawaziri wetu wasifanye maamuzi kwa kutafuta sifa binafsi bila kuangalia athari, si kila mahali lazima sheria na ubabe vitumike wakati mwingine busara na hekima inasimama badala ya sheria. Hivi majuzi Rais Kikwete alipowasihi viongozi wa upinzani wakutane badala ya kuandamana nchi nzima alitumia busara na hekima japo watu wengine wanadhani angefuata sheria. Rais Kikwete kwa kutumia busara na hekima alizopewa na Mungu tayari ameepusha vurugu na uvunjifu wa amani ambao ungejitokeza kama maandamano yangefanyika. Namsihi waziri kama alivyofanya Rais akae na wenye malori kutafuta suluhu aachane na mambo ya kuzijua sheria na ubabe usiokuwa na manufaa kwa Watanzania, athari za uamzi wake huo ni kubwa hata kwa mawaziri wenzake.
 
Pili kwa wale mliowahi kufanya biashara ya mbao. Ukapakia mbao zako mathalani kutoka Urambo, Tabora tonnes ziko sawa kabisa eg 54 tonnes. Mbao unazipeleka DSM. Bahati mbaya ukafika Singida mvua ikanyesha, mbao hizo zikalowa na maji ya mvua. Believe me kama mkifika Dodoma mkapima uzito, mbao hizo hazitakuwa tena na uzito wa 54 tonnes, zinaweza kuongezeka hadi 56.4 tonnes, sasa kama hapo hakuna tolerance limit ya 5% tayari utatakiwa kulipa faini. Na hapa ndiyo unaona UZURI wa kuwa na tolerance limit. Mimi (transpoter) sijaleta mvua. Lakini mvua imenyeshea mbao zangu, zimeongezeka uzito, hivyo hiyo tolerance e limit itanisaidia because it was not my intention kuzidisha uzito in the first place.



Umeeleza vizuri mkuu, sikuwa naona umuhimu wa hii 5% tolerance mpaka niliposoma bandiko lako- asante sana
 
Some tyms Magufuli namwelea lkn smtys simsomi kabisaa, yani ananikumbusha ule msemo wa mgema akisifiwa anatia maji pombe yote,
sasa jamaa sifa zimemzidia alianza kujamba sasa ameona ni bora anye kabisaa, tena kama bata!!
 
Magufuli ni MCHUMIA TUMBO.

Nadhani kuna mtu alimdanganya kuwa ana akiki sana na hasa baada ya kuwa Dr. Sasa amebeba dharau kiasi kwamba mdomo wake unahitaji speech governor. Hana tofauti na yule profesa anayesema Watanzania hawana akili isipokuwa yeye.
 
Back
Top Bottom