Update....mnapeana?!

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,821
59,424
Habari yenu wandugu.

Hivi ni wangapi kati yenu baada ya muda kupita tangu kuanza mahusiano/kuingia kwenye ndoa zenu mmewahi kukaa chini ma wenzi wenu na kuwauliza mahusiano yenu yanaendelea vipi/yanaelekea/wanataka yaelekee wapi?!Mnaulizana kama kila mmoja anayafurahia na ameridhika na yanavyoendelea?!Unaongea na mwenzio kujua kama nae anafurahia kama unavyofurahia wewe?!Kama bado mpo kwenye ukurasa mmoja kama ilivyokua awali?!

Au ndio mkishakubaliana/oana basi kunakua hamna umuhimu wa kupeana ‘UPDATE‘ kwenye swala zima la hisia zenu?!Usidanganyike na “I love you too“....na mengineyo yanayorudisha majibu ya “.....na mimi pia.“ Haya ni majibu ambayo hayahitaji hisia ziwepo kuyapata. Mtu anaweza akaonyesha furaha japo hanayo...mapenzi yamepungua kibaba wewe hujui wakati ungejua ungefanya juhudi za kuyarudisha.Mwenzako mawazo ya ‘upenzi tu‘ yameshamtoka yanatamani/taka ndoa wewe ndo kwanza unaonyesha msisitizo ni kiasi gani huna hamu nayo....mwenzako kashakuchoka na ‘uchumba‘ anatamani kuuvua ila wewe ndo kwanza kila siku waongelea mbwembwe za harusi anashindwa kukwambia.Msisubirie kushushuana kanisani kwa jibu la ‘HAPANA SIKUBALI‘...ndoani mwenzio ‘HATA HAJUI HISIA ZAKE ZIKO WAPI‘ au kuagwa na mpenzi maana alichotaka mwanzo sicho anachotaka sasa hivi na wewe bado hujabadilika.Meaning mwendo wenu hauwiani....kila mmoja anatembea kwa speed yake mpaka mmepotezana au mmoja kabaki nyuma sana.

Kumbukeni kwamba mawasiliano ni muhimu kwenye mahusiano....na mawasiliano yenyewe ndo haya.

Siku njema!
 
inaonyesha may be its true kuwa computer scientist ndio best lovers lol

sababu updates ni sehemu ya kazi yao lol
 
Huo muda utoke wapi?? ikitokea shida ndo tunaulizana lakini kama mambo yako sawia maisha yanakwendaWatu wengine hawataki kuambiwa "We need to talk"
Mnasubiria mpaka nyufa zigeuke milango ehhhh!Nwy hamna haja ya kutishana na “we need to talk“..ni maongezi ya kawaida unaunganisha na mengine mkiwa mmetulia!
 
Huo muda utoke wapi?? ikitokea shida ndo tunaulizana lakini kama mambo yako sawia maisha yanakwenda

Watu wengine hawataki kuambiwa "We need to talk"

na hata 2kipata huo muda bado tutaambiwa mambo shwari hakuna tatizo, ni wachache sana watatoa ushirikiano, wacha tusubirie tu tumbwili likitokea ndio tuweke mambo sawa hayo mengine hatutapeana majibu dhabiti.
 
You can review it by going somewhere mbali kidogo na nyumbani (kama pesa ya kufanya hivyo ipo)....Huko mnaweza kuongea taratibu bila ya kuwa na ile ''state ya we need to talk''. Mara nyingi binadamu anaweza kufunguka yale yaliyomo moyoni mwake kirahisi zaidi akiwa ''ame - relax'' kuliko akiwa kwenye tension.

Mambo ya ''we need to talk'' hayachelewi kupelekea statements kama ''I don't see this relationship taking us anywhere''....!!
 
from my experience

ukimuuliza mwenzuio kuna tatizo gani,
utaanza kumfanya ayatafute matatizo hata kama hayapo..
utamjengea mawazo ya to look for faults...
hata kama sio tatizo kubwa,litagaeka kubwa...

so kama husemi,na huonyeshi kivitendo kuna tatizo
bora na wewe kujifanya hakuna tatizo mpaka lije kwa uwazi
updates kwani ndoa ya mkataba????/
 
nimekupata, bado nacctizia kwenye ushirikianio, mwenzangu ataonyesha huo ushirikiano sasa? i mean kuwa muwazi.
 
Huo muda utoke wapi?? ikitokea shida ndo tunaulizana lakini kama mambo yako sawia maisha yanakwenda

Watu wengine hawataki kuambiwa "We need to talk"

halafu hili la we need to talk umeling'ang'ania sana
litakuharibia mahusiano..

mazungumzo mazuri ni yale ambayo hayakupangwa,tena sometimes ni ya mzaha mzaha
hivi au utani utani hivi l...hapo hapo unamchomekea mtu pointii muhimu
 
from my experience

ukimuuliza mwenzuio kuna tatizo gani,
utaanza kumfanya ayatafute matatizo hata kama hayapo..
utamjengea mawazo ya to look for faults...
hata kama sio tatizo kubwa,litagaeka kubwa...

so kama husemi,na huonyeshi kivitendo kuna tatizo
bora na wewe kujifanya hakuna tatizo mpaka lije kwa uwazi

updates kwani ndoa ya mkataba????/

thnx Boss....nadhani nilishindwa kueelzea vzr, hiyo ndio ilikuwa point yangu haswaa.
 
nimekupata, bado nacctizia kwenye ushirikianio, mwenzangu ataonyesha huo ushirikiano sasa? i mean kuwa muwazi.

Kwanza wewe laazizi wangu una kesi na mimi......''so we need to talk''. Tehetehetehetehe!
 
Mnasubiria mpaka nyufa zigeuke milango ehhhh!Nwy hamna haja ya kutishana na “we need to talk“..ni maongezi ya kawaida unaunganisha na mengine mkiwa mmetulia!
ndugu tena ikitokea mwenzako alikubali kuwa na wewe kwa sababu zake binafsi na akazikosa anakuwa anatumia nyufa effectivelly hadi kuachana kabisa, so issue ya kukutana na mke/mume kila wkend/ month end mahsusi kuzungumzia maendeleo ya mahusiano ni suala la msingi sana
 
Back
Top Bottom