Update Kesi ya wananchi kuhusu bandari mahakama kuu Mbeya

Njia zipo nyingi, hii ni ya kwanza, ikifeli itaangaliwa ya pili, ilimradi kuhakikisha haki ya rasilimali za Tanganyika inapatikana.
John Heche kazuiliwa mjadala uliotakiwa kuwa Star TV, ndo uonee uhalisia ulivyo, huyo Jaji atapewa karipio 1 tyuuh atafutilia mbali hilo shauri
 
#Updates
Mheshimiwa Jaji Ndunguru ameingia Mahakamani 5:00 .

Karani wa Mahakama amewaita Walalamikaji na wamekaa kwenye Kizimba chao.

MAWAKILI Wanajitambulisha;

1. Kwaajili ya Wajibu Maombi (Serikali)

Adv. Hangi Chana (principal state attorney)

Adv. Ayoub Sanga -state attorney

2. Kwaajili ya Walalamikaji;

Adv. Boniface MWABUKUSI - Wakili kiongozi

Adv. Philip Mwakilima

Adv. Livino Ngalimitumba

CHANA SA: Mhe Jaji, Sisi upande wa Wajibu Maombi tulipokea Nyaraka za Shauri hili siku ya tarehe 26.06.2023.

CHANA SA: anaendelea.... Marekebisho sehemu yoyote ukiona SA namaanisha wakili wa serikali.

Mhe Jaji kwakuwa shauri hili limefunguliwa kikatiba chini ya Ibara ya 108 (2) ya Katiba, ambapo sheria inahitaji shauri la namna hii kuendeshwa kama shauri la kawaida,

Ni kwa sababu haijaletwa chini ya sheria ya BRDEA na hivyo shauri hili linatakiwa liendeshwe chini ya Sheria ya Civil Procedure husuani Order VIII Rule 1 ya CPC ambayo inataka Majibu tuyalete ndani ya Siku 21 tangu tarehe ambayo tumekabidhiwa Hati ya Madai.

CHANA SA: Kwa msingi huo, tarehe ya Mwisho ya kuleta majibu yetu ni tarehe 17.07.2023 kwakuwa tulipokea hati hizo tarehe 26.06.2023.

Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji, bado tunazo siku za kuandaa majibu yetu na tutayaleta.

Ni hayo tu. Na mwenzangu SA hana la kuongeza.

Jaji anamkaribisha wakili Mwabukusi.

WAKILI MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, kama alivyosema mwenzangu Wakili Mwandamizi Chang'a, kimsingi sisi hatupingani na hoja zao.

Lakini Mheshimiwa Jaji, wakati tunasubiri majibu yao; tunaomba kuitaarifa Mahakama kwamba tumeshasajili Maombi Madogo chini ya Hati ya Dharura, na hivyo tunasubiri maelekezo ya mahakama yako tukufu.

Wakili Mwabukusi: Mhe Jaji kwa kuzingatia aina ya shauri lililoko chini ya Mahakama hii tukufu, na kwa kuzingatia kwamba Wajibu maombi wanahitaji muda wa kujibu maombi yetu na kuyaleta mahakamani,

Hivyo Chini ya Order XLIII (2) Proviso na Kifungu cha 68 (e) ya CPC, CAP 33 R.E 2019, Mheshimiwa tunaiomba Mahakama hii tukufu ione kwamba kuna umuhimu wa kutoa "Conservatory Orders" kwamba Hali ibaki jinsi ilivyo mpaka pale shauri litakapokuja kutajwa tena baada ya Wajibu maombi kuleta majibu yao, na Mahakama kupata fursa ya kuona na kuyapokea maombi yaliyopo mbele yake au kutoa Amri zozote.

Wakili MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, hii ni kuleta maana kwamba, kisifanyike kitu ambacho kitafanya Maombi/Shauri lililoko Mahakamani kuonekana halina Mashiko au kuharibu jambo hilo kiasi cha kutotengenezeka.

Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Anasimama wakili wa serikali.

SA: Mheshimiwa Jaji, licha ya Mawakili wa Waleta Maombi wamekubaliana na ombi letu,

Kimsingi ameleta maombi haya kwa Order XLIII (2) na Kifungu 68 Ambayo inalenga kuleta maombi kwa mdomo bila formal applications.

SA: Mheshimiwa Jaji, licha ya Mawakili wa Waleta Maombi wamekubaliana na ombi letu,

Kimsingi ameleta maombi haya kwa Order XLIII (2) na Kifungu 68 Ambayo inalenga kuleta maombi kwa mdomo bila formal applications.

SA: Hata hivyo Mheshimiwa Jaji, kifungu hicho alichokitaja kinaweka wazi kwamba hilo ni suala la mamlaka ya Mahakama (discretionary powers) na kwamba kinaeleza zaidi kwamba inaombwa kwa namna ya mdomo pale ambapo Wadaawa wanakuwa wameridhia kwamba maombi yafanyike kwa mdomo, sisi upande wetu wa Wajibu Maombi hatujakubaliana.

SA: Hata hivyo Mheshimiwa Jaji, kifungu hicho alichokitaja kinaweka wazi kwamba hilo ni suala la mamlaka ya Mahakama (discretionary powers) na kwamba kinaeleza zaidi kwamba inaombwa kwa namna ya mdomo pale ambapo Wadaawa wanakuwa wameridhia kwamba maombi yafanyike kwa mdomo, sisi upande wetu wa Wajibu Maombi hatujakubaliana.

SA: Mheshimiwa pia sheria inaelekeza mahakama kutazama mazingira ya jambo husika, tunaiachia mahakama, pia nyaraka ambazo wenzetu wanasema wamesajili kimsingi hadi sasa haijapokelewa mahakamani na sisi hatujapewa.

SA : Mhe Jaji pia vigezo vilivyowekwa kwenye kesi ya ATILIO MBOWE ni muhimu vikidhi.

SA: Wameleta shauri ambalo wamesema Serikali na Bunge wameshafanya maamuzi, na hawajasema yanatarajiwa kufanyika. Maombi haya ya kutaka mambo yabaki kama yalivyo, amri hizo zitawasaidia nini?

Mhe Jaji sisi tunafikiri maombi yao yasikubaliwe kwa mdomo, tusifanyie kazi kwenye "speculations" kwamba watu hawa watafanya hivi na vile.

Tunasisitiza maombi yao yasikubaliane yatupiliwe mbali.

Anasimama wakili Mwabukusi kwa ajili ya REJOINDER

WAKILI MWABUKUSI: Mheshimiwa Jaji, Msomi Sanga ametafsiri vibaya (misconstrued) kifungu cha Proviso, ameshindwa kutambua kwamba Conditions zilizowekwa zinajitegemea.

Wakili Mwabukusi: Mheshimiwa Jaji Wakili Sanga amefanya mawasilisho yake kwa kitu kipya, hakujibu hoja zetu. Hivyo tunaomba Mahakama hii tukufu iweze kupuuza (disregard) hoja zake.

Wakili MWABUKUSI: Mhe Jaji, Wakili Sanga amesema tumefanya "a mere statement from the Bar." Na huu ndio msingi wa Kifungu tulichotumia kuomba maombi yetu kwamba mazingira ya namna hii yanamruhusu Wakili kutoa maombi directly from the Bar.

Naomba kumkaribisha Wakili Mwakilima kuongeza kidogo.

WAKILI MWAKILIMA: Mhe Jaji, Wakili Sanga ametaja kesi ya ATLIO v. MBOWE. Kesi hiyo haiwezi kusaidia Mahakama kutatua jambo hili kwani katika kesi hiyo ilihusu ugomvi wa Mpangaji na Mwenyenyumba.

Shauri letu hapa ni la Wananchi kuhusu upotevu mkubwa na kupotezea kabisa rasilimali za nchi.

Anamaliza Mwakilima.

MHE JAJI NDUGURU: Wajibu Maombi mnafikiri majibu yenu mnaweza kuleta lini? Mkizingatia nature ya shauri imeletwa chini ya Hati ya dharura na sisi (Majaji) tumejipanga angalau tarehe 17 au 18 tuanze kusikiliza kesi hii.

SA: Sisi tutakuwa tayari kuleta majibu yetu ifikapo tarehe 14.07.2023.

MWABUKUSI: Na sisi tuanze kuhesabiwa tarehe 15 na tupo tayari kuleta majibu yetu hadi ifikapo tarehe 19.07.2023.

Mheshimiwa Jaji anaandika Uamuzi mdogo wa kutoa maelekezo na ratiba (schedule) ya namna ya kufikisha nyaraka Mahakamani

JAJI NDUNGURU;

Kuhusu maombi yaliyoletwa, Mahakama inaona kwamba Maombi hayo kama yalivyo semwa yanasajiliwa Mahakamani, basi inafaa yafanyiwe kazi katika namna yake pale yatakapokuwa tayari Mahakamani.

AMRI:

1. Shauri linaahirishwa.

2. Shauri litaanza kusikilizwa tarehe 20.07.2023 kwa Mfululizo.
Tulizoea sana kusikiliza akin
1. kibatala
2. John Mallya
3. Etc
 
Hii kitu ni vita halisi mitaani, kwenye social medias na sasa mahakamani kati ya WA - TANGANYIKA vs WA - ZANZIBARI..

Tunajua hawa Wazanzibari wanaongozwa na kamanda wao Samia Suluhu Hassan mpangaji aliyeko katika ikulu ya Tanganyika...

Lakini uhakika ni mmoja, Tanganyika tutashinda hii vita bila shaka..!!!
 
Hoja kuu za wananchi kuhusu vipengele vya mkataba vinavyoiuza Tanganyika vifanyiwe kazi
 
Nimeandika nikafuta, nikaandika tena nikafuta kama mara tatu hivi. Samia Samia Samia Samia Samia Samia Samia Samia Samia!!!!!!!!!!!!!!!!!!?.
 
Hii kitu ni vita halisi mitaani, kwenye social medias na sasa mahakamani kati ya WA - TANGANYIKA vs WA - ZANZIBARI..

Tunajua hawa Wazanzibari wanaongozwa na kamanda wao Samia Suluhu Hassan mpangaji aliyeko katika ikulu ya Tanganyika...

Lakini uhakika ni mmoja, Tanganyika tutashinda hii vita bila shaka..!!!
Amen Amen Amen. Enyi wazanzibar, kauzeni Zanzibar yenu. Watanganyika tumekataa kuuzwa kwa Tanganyika yetu.
 
Kesi hii ya bandari ni mali ya wananchi , wananchi wajaa mahakamani



Kesi ya kikatiba kupinga vifungu hatarishi uhuru wa taifa, rasilimali na usalama wa taifa vilivyopitishwa kupitia mkataba waliosaini serikali na Azimio la Bunge kupitisha mikataba hiyo batili.
 
Wakili Mwabukusi na wakili Mwakilima wasema haya baada ya kesi kuhairishwa




Waziri mkuu, waziri wa uchukuzi, wabunge hawajui walichopitisha kama mkataba hivyo sisi mawakili tunawasaidia viongozi kuelewa uzito wa makosa makubwa waliyopitisha bungeni


Spika, Waziri wa miundo-mbinu, katibu wa Bunge, katibu mkuu miundo-mbinu wanatakiwa wajipime wenywe na kujiuzulu hili ni la kuwajibika kwa walipa kodi kwa kuchezea hisia za waTanzania huku wakihatarisha mali za Tanganyika bure kwa wawekezaji wa nje na hili la kuwajibika halihitaji Mahakama ...

Waliokabidhi mali ya Tanganyika na DP World kukubaliaba kukimbilia Uingereza ni kwa sababu English law haitambui sheria za Tanzania za natural resources ya 2017
 
Alphonce Lusako mmoja wa raia aliyefungua kesi, anena haya katika viunga vya Mahakama Kuu Mbeya

 
1688401897640.png

Wadau ambao wanatetea mali za Tanganyika wakiwa ktk viunga vya mahakama kuu kanda ya Mbeya
Busokelo TV
 
Angalau inatia moyo.
Hivi kuna utaratibu wowote wa ku ''support'' jambo hili?
 
Kesi hii ya bandari ni mali ya wananchi , wananchi wajaa mahakamani



Kesi ya kikatiba kupinga vifungu hatarishi uhuru wa taifa, rasilimali na usalama wa taifa vilivyopitishwa kupitia mkataba waliosaini serikali na Azimio la Bunge kupitisha mikataba hiyo batili.
Jamaa wangeweka wazi iyo michango inatumwa wapi. Wa Tz watafanya miamala chap chap, hii ni swala kubwa sana.
 
Hili shauri lingefunguliwa kwenye mahakama ya Afrika Mashariki kwa sababu Mahakama ni mhimili mmoja wa Serikali hiyo hiyo iliyotetewa na mhimili mwingine yaani Bunge. Hawa watalindana tu!.
 
HAPA HAMNA KUPOTEZA. HII PEKEE NI USHINDI MAANA NI SAWA MTU ALIYEBANWA NA MLANGO ANAZIDI KUPIGA KELELE ILI ANUSURIKE ASIFE. HATA KAMA ATAZIDIWA NA WALIOMBANA NA AKAFA. HISTORIA ITABAKI KUWA HAKUNYAMAZA, ALIPIGANIA UHAI WAKE. HATA UKIFUKUZWA NA SIMBA, KIMBIA HATA KAMA ATAKUKAMATA LAKINI ULIWEKA JUHUDI ZA KUJIOKOA. HIVI SIO KWELI ALIYEPOST HIVI, NANUKUU"Hivi watu wana muda wa kupotezaa eeh?? Huyo Jaji na mahakama yake akipigiwa cm 1 tyuuh anafuta case na shauri zake zote.

Watumie njia nyinginee, hii wanajichosha buree tyuuh,.
 
Back
Top Bottom