Uongo juu ya Mchawi aliyeanguka Mbezi Lous (UBATA) RPC Mulilo chukua hatua haraka kutetea haki za wanawake

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,666
Je umeshakutana na picha za uchi au vidio za anayeitwa mchawi aliyeanguka mbezi lous UBATA na ukadhani kweli yawezekana ni mchawi kweli ,nakupa ukweli wenyewe.

KWANZA
Kwako waziri Dk. Dorothy Gwajima na RPC Dar msiliache hili la mama huyu kudhalilishwa kisa chuki za mitaani, waliohusika wachukuliwe hatua haraka kulinda hadhi ya wanawake nchini hasa kipindi hiki rais na spika ni wanawake

Imagine mkeo, dada Yako, mamako, shangazi au bibi yako anakwenda kutembea Kwa jirani shosti zake wa siku nyingi anawakuta wanakunywa pombe naye anaagiziwa (kumbe wamepanga kumdhalilisha siku nyingi ) wanampa kinywaji na kumuwekea madawa ya kulevya wanamvua nguo wanampiga picha na video na kuita watu kuwa mchawi kaanguka kwao (huku wakimfahamu kabisa ) roho gani ya unyama kiasi hiki ama kweli wanawake hampendani.

Huyu mama almanusra auwawe na wahuni kabla hawajamfahamu na kugundua ni mke wa mtu anayeheshimika mtaaani , je angeuwawa ingekuwaje ,wahusika wakamatwe haraka ni wauwaji .

Mama huyu hakuwa mchawi ni mama na tukio hilo sio la uchawi kwa mujibu wa wanawake na vijana waliokwenda kumsitili huku wakisema kulikuwa na dalili zote za kupewa madawa ya kulevya Kwa kuwa mmoja wa mama hao kuwa ni adui yake wa muda.

Jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina na wahusika wote wakamatwe haraka kulinda haki za kina mama .

Muhimu, sikuweza kuweka picha hapa wapa videos kulinda maadili na kukwepa kufanya kosa kama waliotekeleza huo uuaji

USSR
 
Sawa mkuu nitumie hiyo VIDEO PM
mm MZIMU WA KOLELO nitascan katika rada zangu nilizofunga toka milimani KOLELO then nitakuja na jibu SAHIHI lisilo na SHAKA kabisa
kama ni mchawi ama lah walimtilia MADAWA YA KUZIONDOA AKILI TIMAMU
 
Imagine mkeo, dada Yako, mamako, shangazi au bibi yako anakwenda kutembea Kwa jirani shosti zake wa siku nyingi anawakuta wanakunywa pombe naye anaagiziwa (kumbe wamepanga kumdhalilisha siku nyingi ) wanampa kinywaji na kumuwekea madawa ya kulevya wanamvua nguo wanampiga picha na video na kuita watu kuwa mchawi kaanguka kwao (huku wakimfahamu kabisa ) roho gani ya unyama kiasi hiki ama kweli wanawake hampendani.
Wakati hayo yanafanyika hukuona busara kuwahi Polisi au kwa uongozi wa Mtaa kutoa taarifa?
 
Back
Top Bottom