Zitto Kabwe - Uonevu huu viongozi hamuuoni au?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Nimeletewa barua pepe hii kutoka kwa Mwana Mama wa Kitanzania ambaye alipendana na mwanaume raia wa Burundi na hatimaye wakaoana. Baadaye mume wake akafukuzwa nchini. Sijui kama alikuwa na makosa au hapana lakini katika nchi yenye kufuata sheria na haki za binaadamu huwezi kutaraji unyanyasi wa namna hii kufanyika. Nimeombwa kufuatilia suala hili na Mtanzania huyu. Ninalifuatilia ili haki itendeke. Naliweka suala hili hapa ili kuonyesha aina ya uonevu ambao raia wetu hupata bila sisi viongozi kujua au tunajua na kupuuzia.

Kisa chenyewe hiki (kwa maadili sitaweka majina)

Mheshimiwa,naitwa (jina) mzaliwa wa Kigoma ktk Wilaya ya mpya ya Kakonko.Sote pamoja na mume wangu ni wahitimu ktk chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo nilichukua PS$PA na mume wangu

(jina) alichukua sheria.Yapata takriban miaka mitatu tangu apewe PI jambo lililotufanya kutoka Tanzania na kuja kuishi Burundi pasipo maandalizi.Nasikitika kupoteza mwelekeo wangu wa maisha kwa maslahi ya watu binafsi kwani kwa kipindi chote hicho naishi kama mama wa nyumbani wakati nina elimu.

Mheshimiwa,mume wangu alianza kufanyiwa fitina na maafsa uhamiaji na hatimae kupewa PI,sikuwa na jinsi niliamua kumfuata nchini Burundi.Mpaka sasa siwezi kueleza kosa alilotenda mpaka tukaadhibiwa kiasi hicho.Ilikuwa mwezi wa 6 mwaka 2008 nilipomaliza chuo,tulikwenda kwa mara ya kwanza kutembea nchini Burundi tulipofika Mabamba mume wangu aliwekwa chini ya ulinzi kuuliza kosa gani tumetenda tuliambiwa ni amri kutoka juu,tulitii sheria.Cha kushangaza nilianza kukashifiwa na maafsa uhamiaji,”Ulikosa mwanaume wa kukuoa nchini Tanzania mpaka uolewe na Mrundi?”Sijui alichotaka kufanyiwa mume wangu kwani niligombezwa na kuambiwa nirudi nyumbani wnitafahamishwa juu ya kesi yake ila niligoma.Sidhani kama nchi ya Tanzania huadhibu wanaoolewa nje ya nchi,la hasha!Hata hivyo,tunaomba msamaha iwapo kuna lolote baya huenda tulifanya pasipo kukusudia.

Mheshimiwa,natambua kuwa wewe ni mtetezi wa wanyonge na mwana mabadiliko,naomba ufanye jitihada zako afutiwe PI hiyo,si lazima turudi kuishi Tanzania ila tuweze kuwa na uhuru kuja japo kutembea.Naona uchungu kuja nyumbani peke yangu hasa wakati wa matatizo kama msiba.

Samahani kwa kukuchosha,nimejaribu kufupisha

Mwisho

Inawezekana kuna Wanawake wengi sana wa KiTanzania ambao wameolewa na wanaume ambao si raia na wamekutana na manyanyaso ya aina hii. Natamani kuona Taasisi za kutetea Haki za Wanawake zikifika vijijini ili kuona mateso ya aina hii. Kama kuna kosa mtu huyu alifanya ‘due process’ ilipaswa kufuatwa kwa kupelekwa mahakamani, kusomewa mashtaka, kujitetea na kupewa hukumu. Inabidi kufuatilia kesi ya mama huyu mpaka haki ipatikane. Nitawajuza wasomaji wangu juu ya matokeo ya suala hili. Kazi ya kutafuta Haki ya Mama huyu sasa inaanza…

source: Uonevu huu viongozi hamuuoni au? - Wavuti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom