Unyama Zanzibar: Kituo cha Redio Chachomwa Moto

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Watu wasiofahamika wateketeza Kwa moto Kituo cha Redio Hits FM usiku wa kuamkia leo, kujeruhi mtangazaji. Meneja wa vipindi Juma Ayoub asema leo.

attachment.php
attachment.php
attachment.php

Watu wasio fahamika wamevamia kituo cha redio cha Hit Fm huko Zanzibar na kumjeruhi mtangazaji wa kituo hicho.

Watu pia walikichoma kituo hicho moto lakini hakijateketea chote.

Bado upelelezi unaendelea kwa taarifa zaidi.

Chanzo: ITV -breaknews
 

Attachments

  • radio.jpg
    radio.jpg
    22.5 KB · Views: 4,048
  • radio2.jpg
    radio2.jpg
    35.5 KB · Views: 4,003
  • radio1.jpg
    radio1.jpg
    10 KB · Views: 3,922
Watu wasio fahamika wamevamia kituo cha redio cha Hit Fm huko Zanzibar na kumjeruhi mtangazaji wa kituo hicho.

Watu pia walikichoma kituo hicho moto lakini hakijateketea chote.

Bado upelelezi unaendelea kwa taarifa zaidi.

Chanzo: ITV -breaknews

Kundi la watu wasiojulikana wenye silaha usiku wa kuamkia leo wameivamia na kuiteketeza kwa moto Studio ya kurushia matangazo ya Kituo cha radio cha kibinafsi cha Hits FM kilichopo eneo la Migombani, Jimbo la Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 
Kulikua na Melody Hawa kila uchaguzi wakitesa wasio ccm
baadae chaguzi nyengine wakaja Janjaweed hawa nao ni special kwa ajili ya kuwabamiza CUF
Mara hii kuna Ma Zombie hawa hujifunika uso kwa soksi na kazi yao pia kuwabamiza CUF sio mara ya kwanza hawa Ma Zombie kuvamia Radio..wakati wa kampeni walifanya haya lakini hata siku moja hawa chukuliwi hatua yoyote...
haya ma zombie yakishakula nyama ya wapinzani kuna siku wataifata ya wale walowatuma ndio theory na principples za ujangili zilivo...
 
Kundi la watu wasiojulikana wenye silaha usiku wa kuamkia leo wameivamia na kuiteketeza kwa moto studio ya kurushia matangazo ya kituo cha radio cha kibinafsi cha Hits FM kilichopo eneo la Migombani, jimbo la Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 
ni maeneo ya migombani,mtangazaji aliyekuwa zamu usiku bw. Ally Abdallah anasema mida ya saa 7 usiku walivamia watu kadhaa studio wakati yeye akiendesha kipindi na wakamuamuru ashuke kitini na kukaa chini,wakamshindilia matambara mdomoni na kumfunika macho kwa kitambaa,wakamtandika kidogo kwa ubapa wa panga na kumwambia awaache wafanye kilichowapeleka,wakamtoa mtangazaji huyo nje kisha wakamwaga petroli na kuchoma moto
chanzo:DW
 
Sio kama hawajulikani wanajulikana, na serikali inawajua, wakati baada ya uchaguzi walivamia kituo kimoja cha radio na kutoa warning kubwa, kwa sababu hicho kituo kilikuwa kinatoa taarifa za uchaguzi.
 
hivi vituo vya sku hizi unakuta mtu ni kada kupindukia kejeli malumbano uswahili kibao kama huku bara hawa kina yahaya wajiangalie
 
Back
Top Bottom