Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia
Hao vijana wamepoteza maisha ya watu wasio na hatia zaidi ya sana. Wanawavamia watu majumbani mwao wakiwa wamelala, hawajaiba cha mtu halafu wao wanaenda kuwaibia na kuwatoa uhai.

Watu wa aina hii ndiyo unaleta ngonjera zq kijinga ahapa kuwatetea? Au kwakuwa hawajaua ndugu yako hata mmoja?

Nashauri polisi na serikali kwa ujumla, mtu yeyote mwenye walakini ktk mwenendo wake akamatwe na kuuawa. Nchi yetu Tanzania ani nchi ya amani. Hawa Panya-road wauawe wote.
 
Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.
Ninyi si ndiyo mlikuwa mnalalamika Panya road mkawa mnasema mtajichukulia Sheria Mkononi kuwakomeshA? Imekuwaje Tena mnaposaidiwa kazi mnalalamika? Au upo upande huo? Sifurahii kuonewa mtu lakini kama ulivyosema vyombo vyote sita nadhani haviwezi kukosea kumtambua kijana mwalifu vinginevyo iwe ni hujuma!
 
Nakasia tu kuwa police wamemini e risasi had wanyoa viduku watandikwe risasi za Moto yeyote atakae kutwa na kiduku bas wamiminie risasi tu hawan tofauti na panya road

Mostly vijana wanoweka viduku asilimia kubwa ndio panya road

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wote wanaoshinda kwenye vibanda vya kubeti wenye milegezo na wapiga debe wote wapigwe risasi.

Hongereni sana polisi kwa maamuzi haya mazuri
 
Kuna mtoto mmoja wa kiongozi mkubwa namaanisha mzazi wake yuko kwenye utatu Mtakatifu.
Ni mtukutu sana na lisumbufu, angekuwa Uswahilini naye angepigwa risasi kwa tabia zile.
Je, huyo mtoto ni panya road na anahusika na uporaji? Ukweli ni kuwa polisi hawaruhusiwa kuuwa, lakini je panya road wanaruhusiwa kukata watu mapanga, kupora, na kuua? Hawa panya road na majambawazi wakiachiwa amani haitakuwepo mtaani. Najua ni jambo kubwa kwa mzazi kuuliwa mtoto wake, lakini inafika mahali inabidi tuukabili ukweli. Ita kuuwawa "panya road" na majambawazi mengine ajali kazini. Kama hawataki polisi wawakamate waachane na ujambazi utaona kama [olisi atawafuata na kuwaua.
 
Habari!
Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.

Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.

Sasa polisi wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wanavuta bangi kisha kuwaua kinyama. Misiba ni mingi mitaani, inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.

Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.

Rais Samia utakuwa na mwisho mbaya. Police wamegeuza Kitonga Dar kuwa machinjio ya binadamu. Hata familia zenu zina vijana wa hovyo, wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road. Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.

NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu, ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, huzuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda uswahilini Tandika na Buza ni huzuni.
Ila ww akili zako za kitoto sana........Kama unajua kuna msako kwa Nini ukakae vijiweni na ujingani.

Siku wakuvamie wakubake wakuibie tuone kama utakuja hapa kusema hayo unayosema
 
Huyu hajawahi kukutana na hawa jamaa chobingo wakaanza mtia mapanga bila kosa na kumsaula mali zake. Anakuja kujifanya mwanaharakati. Huyu kama vipi na yeye auliwe na polisi unaweza kuta anashiriki uhalifu huu wa panya road why anakerekwa kusikia unatokomezwa?!
Kwa sasa ukiona mtu anamtetea panya road basi ujue ni eidha na yeye ni mmoja wa hao panya road, au ana ndugu yake, mtoto wake, rafiki yake ambae ni panya road.
Mtu wa kawaida kabisa unaefahamu unyama unaofanywa na hawa mbwa hauwezi kamwe kuja kuwatetea humu mitandaoni kama wanavyofanya baadhi ya hawa wahusika wenzao.

Natamani polisi iwe inapita humu JF kuwafuatilia na kuwachunguza vizuri hawa wanaowatetea hao vijana makatili.
 
HILI LA KUUA PANYA ROaD SIO SAHIHI.. kila mtu asikilizwe na ahukumiwe na sheria mahakamani. Mtu akifa unaweza kumpa hatia yeyote hata kama aliuliwa kwa makosa...
Ile tume ya kuangalia Jeshi letu ifanye kazi kwa haraka..
Yaa i watu wanatetea uvunjwaji wa sheria kisa tu yanayowakuta ni watoto wa maskini! Hivi tukisema mtu akifanya kosa auawe bila kufuata sheria wangapi watauawa. Mfano hao watoto wa ushuani wakichukua gari za baba zao na kwenda nazo kwenye sherehe za birthday za ulevi kisha kutokana na kuendesha gari wakiwa wamelewa wakisababisha ajali nao wauawe papo hapo au wazazi wao watakuwa wa kwanza kutaka sheria ifuatwe? Au watoto wao humo ndani wakibaka housegirl mbona wanajitahidi kuyamaliza kimya kimya? Je nao wauawe bila kuhukumiwa mahakamani?

Ni vyema tutatue matatizo ya jinai mbalimbali kwa kufuata sheria.
 
Wewe kama kijana unajua vizuri operation linaloendelea sasa ni kuwasaga 'panya road' halafu wewe bado unakaa maeneo hatarishi usiku mkubwa eti unavuta bang.

Polisi haiwezi kutofautisha kibaka na mvuta bangi endapo utakutwa usiku sehemu isiyoeleweka na ukaamriwa ujisalimishe kisha ukatoka nduki lazima risasi zikuhusu mkuu.

Siungi mkono mauaji ya aina yoyote yale ila kipindi hiki cha operation maalum tujihadhari sana na kuzurura usiku pasipo sababu inayoeleweka.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo kijana akikimbia tu,apigwe risasi??
 
Back
Top Bottom