UNSC: Azimio uchwara la Marekani kusimamisha vita Gaza lapigwa Munda

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,889
35,901
Imekuwa aibu kwa Marekani na azimio lake uchwara la kusimamisha vita Gaza.

IMG_20240323_112147.jpg

Kwamba halikupigwa veto moja bali duble duble Marekani ijitafakari sana.

Wenye akili zao wanatambua, urafiki na Marekani ni wa kinafiki:

View: https://www.youtube.com/watch?v=i0_CReHGOKM

Mkenya atapinga.
 
Kwahiyo ruksa Israel kuendeleza kichapo?

Azimio lilikuwa uchwara: halimkemei mwisraeli vilivyo wala kumwamuru mwisraeli kusimamisha vita sasa.

Azimio stahiki litapigiwa kura leo ambalo bila shaka mwenye vita vyake huko na mnafiki mkuu ndiye pekee atakayelikataa.
 
Huoni kulizuia hilo azimio ni kurefusha muda wa kuchabangwa Wapalestina?Na unavyofikiri,kuna wa kuwa serious kweli na kumkemea Israel na akatii?
 
Unadhani waliolikataa azimio ni wajinga ila wewe?

Kwa taarifa yako lengo la azimio lilikuwa pause ya Ramadhani vita kuendelea baadaye.

Hakuhitajiki pause, kuna hitajika vita kusimama ikiwezekana milele!
 
Nilidhani uko seriously, kumbe uko hapa kutetea magaidi walichokifanya October 2023 na kuuwawa Kwa Watanzania wenzetu?

Kufa mtu ni kufa haijali kama ni mtanzania au mchina! Kina Ben wako wapi? Ulisema nini wapi? Au ni Yale machozi ya kwetu ya mamba?
 
Unadhani waliolikataa azimio ni wajinga ila wewe?

Kwa taarifa yako lengo la azimio lilikuwa pause ya Ramadhani vita kuendelea baadaye.

Hakuhitajiki pause, kuna hitajika vita kusimama iliwezekana milele!
Kukataa azimio hakuwafanyi kunizidi akili.Kwani Wapalestina hawataki half-time ya vita ili wapate futari bila kukwepa mabomu?Na walipoingia ndani ya Israel kuua na kuteka Waisrael walidhani kitatokea nini kwao hadi leo hii hawataki tena vita milele?
 
Waliolikataa azimio uchwara Hilo siyo wapalestina ndugu.

Akili za kupuyanga Kwa hakika unazo na Kwa hizo wewe nambari 1.
 
Waliolikataa azimio uchwara Hilo siyo wapalestina ndugu.

Akili za kupuyanga Kwa hakika unazo.
Unasoma kwa kutumia akili kweli wewe?Nimeanza na waliolikataa azimio(macho machache na bolsheviks) nikahamia kwa Wapalestina kwenye aya hiyohiyo.Au unasoma huku unapiga dufu?
 
Kufa mtu ni kufa haijali kama ni mtanzania au mchina! Kina Ben wako wapi? Ulisema nini wapi? Au ni Yale machozi ya kwetu ya mamba?
Kwamba Russia ndiyo azimio yake itakuwa serious wakati amekataa kuacha vita na Ukraine? Ukishakuwa na upande wa kushabikia inakuwa tatizo sana.
 
1. HAbari hii haihusiani na vita vya Ukraine ambako kama Israel, Mrusi ni kama kibaka mwizi wa kuku

2. Habari hii inahusu azimio la kusimamisha vita kuwa kwa vile ni uchwara, limepigwa chini.

3. Azimio ni uchwara Kwa sababu linaitisha kusitisha mapigano (calling for ceasefire) badala ya kushinikiza mapigano kusimama (demanding for ceasefire).

4. Ikumbukwe Marekani imependelea kuwa baby seat waisrael hata pale inapokiuka sheria za kimataifa.
 
Hiyo Azimio nyingine inaletwa na nani? Na unajipa uhakika gani kuwa haitakuwa na changamoto ya kupingwa pia na wajumbe?
 
Back
Top Bottom