University of Dar es salaam: Mnavyowafanyia wanafunzi wa masters na PhD mnakiua chuo, badilikeni

Mkuu,naelewa msingi wa hoja yako na kero unayopata ila pia kuna mambo mawili unapaswa kujua.Masters na PHD sio sawa na undergraduate degree..Vile usahihisishaji wa THESIS ni mchakato ambao unahitaji ubunifu na upekee katika utekelezaji wake.

Wanafunzi wengi wa masters na hata PHD wa siku hizi hasa wale ambao ni self sponsored huwa wanakuwa na tabia mbaya ya kufikiri kwama Masters na PHD ni kama Undergraduate studies,Wanaungaunga tu madesa na kujaribu kulazimisha thesis zao ziwe accepted bila kuwa critical au indepth.Matokeo yako ndo hao supervisors ambao nao wanakuwa mawenge mawenge.

Mtu mwenye masters anatakiwa aoneshe kiwango cha juu cha uelewa n kumudu eneo husika.Mtu wa PHD anapaswa kuleta mchango mpya wa maarifa katika eneo lake la utaalamu SWALI ni je mtu ambaye mwenyewe hajazama ipasavyo katika eneo husika anaweza kumpima mtu mwingine iwapo amezama katika eneo hilo.JIBU na haiwezekani.

Ndio maana mara zote huwa nawachallenge vijana wanaofanya Degree ya kwanza achague topic ya research ambay anaweza kuendelea nayo katika masters na PHD kwa kutafuta suluhu au maarifa kuhusu jambo ambalo linaweza leta mchango wa maarifa.Hii habari ya kuokoteza topics matokeo yake hata supervisor wako anashindwa jinsi ya kukusaidia.

All in All UDSM wanapaswa wajitazame upya maana haya malalamiko yamekuwa mengi na ni dalili kwamba kuna tatizo mahali.

Hata hivyo napenda kutoa ushauri kwa watu wote wanaofanya Masters na PHD.ni vyema ukawa na coach au mentor ambaye ni ziada ya Supervisor wako wa CHUO ili akusaidie na kukuongoza.SOMA vitabu sana pamoja na kazi za watafiti wengine na hakikisha kama unafanya utafiti basi fanya utafiti kweli usikurupuke maana Masters na PHD kwa uzoefu ni ngazi za elimu ambazo unapoamua kujiendeleza basi una mpango wa kuingia katika taaluma au utafiti ila kama unataka masters kwa ajili ya salary scale nafikir ni lazima utalaumu na kulalamika kuwa supervisor kakubania.

Tuendelee kuwasema UDSM najua watasikia na kujirekebisha.ILA PHD na MAsters za OPEN nafikiri ndo stress free.
 
FB_IMG_1631990952013.jpg
 
Mkuu wachana na huyu, uongo mwingi. Ukisoma andiko lake kila mahala ni uongo tu . Pamoja na kwamba ni kweli Udsm kuna tatizo, ila haya ya huyu ndugu hayana uhalisia. Kwanza hii inayoitwa Academic block pale Udsm sijui ni ipi? Lakini sijui ni wapi alikokutana na hawa waliompa haya aliyoandika hapa. Ni either hakwenda Udsm ama waliompa taarifa hawakuwa wanaudsm. Mzee amepiga master miaka ya 1990 tena nje ila hawezi kujua namna bora ya kumsaidia mtoto wake amalize shule kwa utaratibu sahihi.
Wewe hakika utakuwa mmoja wapo wa linyang' au wa UDISM ma dokta njaa, madokta uchwara njaa kali.
 
Tutazunguka sana lakini ukweli upo wazi mmo.
Supervisor wa Tanzania hana incentive yoyote ya kupambania ili mwanafunzi wake wa Masters afanye vizuri na kumaliza mapema.
Mwanafunzi akimaliza, supervisor analipwa laki na nusu baada ya muda wote huo. Mpumbavu mmoja atasema si ana mshahara? Anao sawa, lakini ki kiduchu.
Nchi nyingi hasa zilizoendelea, supervisor hulipwa vizuri kila mwanafunzi wake anapohitimu. Hiyo ni nje ya mshahara sio masihara kama ya kwetu.
Wakati mwingine huhitajika zaidi ya supervisor mmoja na wagawane hiyo laki moja.

Tuna safari ndefu sana
Kuna siku ililetwa mada humu jamvini kwamba ma Dr na Prof wa bongo wenfi ni masikini na njaa kali maana wanaonejana walivyopauka ila kuna baadhinmlibisha.

Sasa ona mnarejea mulemule mlipopakataa
 
Sina uhakika kama kisa hiki ni cha kweli. Lakini, hata kama ni cha kutunga, ama kimetiwa chumvi, bado malalamiko haya si ya kwanza kuyasikia vyuoni mwetu. Sasa ngoja nijazie kana kwamba ni kisa cha kweli.

Wale majuha mnaoponda mzazi kumsaidia mwanawe hayajawakuta. Ninadhani ni majitu yale yamesoma yakiwa makubwaa kiumri, au yale ambayo yalinyimwa upendo toka kwa wazazi/walezi wao. Yamejaa roho za chuki na husda. Yameteseka na shule sasa yana wivu wakiona wenzao wanapata msaada wa wazazi wao. Haya ndo yale yakiwa matoto, yakivunja kikombe tu,yanapigwa na wazazi mpaka yanavunjwa mkono. Yameharibika mioyo kabisa. Yangependa kuona watu wanateseka kama wao. Aidha, hayana uchungu maana hayajasoma kwa kiwango hicho, yanaona wivu.Au hayana watoto waliofikia ngazi hiyo ama ni yale yasiyojali watoto.

Ipo hivi, siku hizi vijana wanasoma wakiwa wadogo sana kwa kulinganisha na nyie majuha. Halafu, taasisi zetu zina mapungufu mengi ikiwemo haya ya unyanyasaji. Aidha, mfumo wa sheria tunaujua nchini, mtu wa kawaida kupata haki ni mambo mawili, acheleweshwe ama akose kabisa. Majuha hamtonielewa mpaka siku una kabinti kako kapo huko, watu wanataka kukagegeda kupitia mitihani/digrii ndo mtajua kwanini mzazi unapaswa kuwa karibu na mwanao.

Laiti mfumo wetu wa utendaji ungekuwa unajali haki, wala hakuna mtu angehangaika hivi. Haya ni matokeo ya kukosekana kwa maadili na uwajibikaji.

Angalizo
WAKATI TUNAKOSOA UTENDAJI MBOVU VYUONI, TUSISAHAU PIA KUNA KUNDI KUBWA LA WATOTO WETU SIKU HIZI HAWANA NIDHAMU NA SHULE. TABIA AMBAZO SISI WAZAZI NA WALEZI TUNACHANGIA. SI KESI ZOTE NI WALIMU/CHUO PEKEE, ZINGINE ZINACHANGIWA NA WANAFUNZI WENYEWE.
 
Mkuu wachana na huyu, uongo mwingi. Ukisoma andiko lake kila mahala ni uongo tu . Pamoja na kwamba ni kweli Udsm kuna tatizo, ila haya ya huyu ndugu hayana uhalisia. Kwanza hii inayoitwa Academic block pale Udsm sijui ni ipi? Lakini sijui ni wapi alikokutana na hawa waliompa haya aliyoandika hapa. Ni either hakwenda Udsm ama waliompa taarifa hawakuwa wanaudsm. Mzee amepiga master miaka ya 1990 tena nje ila hawezi kujua namna bora ya kumsaidia mtoto wake amalize shule kwa utaratibu sahihi.
Acheni ujanja ujanja UDSM kumeoza afu mnapenda rushwa za ngono
 
Mtoto want amesoma masters mwaka Sasa hata proposal ya masters haijavuka kwa supervisor, kila akimcheki supervisor hakuna email reply Wala wala apokei simu.

Nikafunga safari kwenda naye chuo kuuliza tatizo ni nini? Watu tuliowakuta academic block walichosema unajua Hawa ma senior lecture na hata wengine hawa mnatakiwa mwende nao Polepole la sivyo mkiwashtaki kwa DVC academy akasikia mtoto wako atafudisco maana wanawasiliana.

Tuvumiliane tu tutamjulisha wenyewe supervisor wake. Kwa kuwa nilikuwa na jazba na Kuna wanafunzi walikuwa wanasikia majibizano Yale na baada ya kutoka nje ndipo nikapata ushuhuda wa Nini kinaendelea chuoni.

Kwanza, hakuna mtu anayesimamia wasimamizi wa wanafunzi ambaye anajua kazi hii imekaa kwa supervisor muda gani.

Pili, madaktari wengi wa UDsM wanaamini wao ndio wenye final say na wanawatisha wanafunzi kuwadisco endapo wakionekana kupingana au kulazimisha wahudumiwe

Tatu, tofauti na urasimu wa supervisors urasimu mkubwa zaidi upo kwa external supervisors ambao wamejiwekea muda wa miezi mitatu au sita kufanyia kazi utafiti uliowasihwa kwao.

Nne, hakuna kitengo cha ICT cha kufanya haya mambo kilicho serious

Tano, hakuna mwanasiasa Wala mtoto ambaye mzazi wake ni mtumishi pale anayekwamishwa wala kuchukua muda kurekebishiwa kazi yake kwa sababu wazazi au wahusika hutumia madaraka na Pr zao kuhudumia

Sita, kazi za wanafunzi zinavyowekwa hakuna utaratibu mzuri. Mwanangu alipewa kazi yakupekua box lina mamia ya kazi za watu...no secrettt

Mimi nimesoma nje miaka ya 1990 hakukuwa na urasimu huu, nimeangalia vyuo vingi ikiwemo hata open utaratibu upo streight....nenda suaut na kwingine utaratibu upo wazi. Kwanini UDSM wapo nyuma hivi?

Hawa supervisor na Urasimu wao ndio wanaotegemea kuteuliwa kwenda kuongoza taasisi za umma? Nadhani kigezo Cha utendaji kazi kiwe msingi wa kupandishwa cheo siyo kazi binafsi za supervisor anajaza cv huku aliopaswa kuwahudumia akiwakwamisha kisa yupo busy na kazi zake binafsi. Haujaariwa chuoni kujiendeleza umeajiriwa kusaidia watu.

Masters 4yrs ,Phd 8 yrs unatafiti Nini? Na kibaya zaidi research paper zao hazina hata ubora wa uandishi kama za vyuo vingine useme wana ubora. Kawaida kabisa.

Mzee Rutinwa simamia watu wako wapitishe kazi za wanafunzi waache uungu mtu
Pole sana kwa hii changamoto uliopitia. Machache nayoweza kuandika hapa ni haya:

1. Usijaribu kulinganisha utatatibu wa vyuo vingine ( nje ya nchi) na hapa Tanzania ( hasa UDSM). Kila chuo kinaweza kuwa na changamoto zake, na kwa ujumla wake vyuo vya wenzetu huko kwenye nchi zilizoendelea vitakuwa vimepiga hatua zaidi. Kwahivyo tegemea uwepo wa hizi changamoto hapa kwetu, ingawa naamini bado UDSM ni chuo bora ukilinganisha na vyuo vingi Africa, India na baadhi ya nchi ulimwenguni.

2. Inawezekana wewe hukuwahi kusoma UDSM, ila kwa wale tuliowahi kusoma hapo, tunaelewa namna bora ya kuishi na walimiu wetu. Mimi binafsi nimepata nafasi kusoma UDSM na pia huko Ulaya. Kwa hapa UDSM mwambie kijana wako, akitaka mafanikio ajishushe, asijifanye mjuaji sana. Mwisho wa siku yeye ndiye anayehitaji degree, hao walimu wao tayari wana degree zao, na wengi wao wamezipata vyuo vya Ulaya, Marekani nk. Wewe na kijana wako mkijifanya wajuaji mtaishia kupoteza.

3. Kile ambacho nimejifunza, ni kwamba endapo mwanafunzi hana uwezo mzuri darasani, huwa anakuwa mzigo sana kwa wasimamizi wake, jambo ambalo linakuwa ni kero kwa msimamizi, na huwa anapata wakati mgumu kuisoma kazi/ proposal ya mwanafunzi. Hawa wasimamizi wanakuwa na kazi zingine pia, kwahiyo anapoona mwanafunzi ambaye ni dhaifu, na hana muelekeo huwa anaamua kuendelea na mambo yake mengine. Kwa wale wanafunzi wenye uwezo mzuri, mara nyingi mambo yao yamekua yakiwaendea vizuri, na wamekua wakimaliza kwa wakati.

4. Fanya hivi: Nenda kwa msimamizi wake kwa heshima, usijifanye mjuaji, ongea nae kwa busara. Msikilize anachoweza kusema, pia mwambie kwamba upo tayari kutoa ushirikiano kusaidia kumkazania kijana amalize kwa haraka. Pia mwambie kijana awe anasikiliza kwa makini yake anayoambiwa afanye na msimamizi wake, asiwe mbishi, afanye vile anaelekezwa kufanya hata kama yeye ana mtazamo tofauti. Mtazamo wake ataufanya akisha maliza chuo, kwa sasa afanye kile anaambiwa kufanya.

5. Endelea kutufahamisha maendeleo ya kijana hapa, ili tukupatie msaada zaidi endapo utahitajika.
 
Kama ulitelekezwa na wazazi wako kaa kimya, Kama unadhani siku hizi masters wanasoma wazeee nyambafu yako

Na kama unadhani yupo mzazi analipa milioni nane Hadi ishirini gharama za masterz na mtoto wake akwamishwe na kiumbe mmoja mbinafsi shenzi type.

Tumieni common sense,
Kitendo tu cha wewe kusema umeenda nae as if huyo jamaa ni litoto flani hivi, imetia shaka sana juu ya uwezo wake, muache apambane mwenyewe, maana hata mtaani huku mambo ni hivyo hivyo kwenye maofisi ya umma, yaani unapigwa danadana hadi unataka kulia, socni bora aanze kujua kujipigania mwenyewe.

Kuna ofisi unaweza ukahangaikia kibali hadi chozi likataka kukutoka, hiyo cha mtoto, na miradi ya mamilioni inakwama, ila inabidi ajue sasa kujipigania, mtaani its even worse.
 
Masters 4yrs ,Phd 8 yrs unatafiti Nini? Na kibaya zaidi research paper zao hazina hata ubora wa uandishi kama za vyuo vingine useme wana ubora. Kawaida kabisa.
Najua kuna watu watakuja kutoa povu hapa. Ila hali ni mbaya kwa kweli na inaumiza sana. Imagine unasoma master's degree miaka mitatu mpaka mitano wengine. Ili iwe nini jamani ?

Mbona hata research paper za hizo dissertation hazitusui kwenye top journals mfano Econometrica, International Business Review au zile za natural science ?

UDSM badilikeni.

Acheni upuuzi huu
 
Kitendo tu cha wewe kusema umeenda nae as if huyo jamaa ni litoto flani hivi, imetia shaka sana juu ya uwezo wake, muache apambane mwenyewe, maana hata mtaani huku mambo ni hivyo hivyo kwenye maofisi ya umma, yaani unapigwa danadana hadi unataka kulia, socni bora aanze kujua kujipigania mwenyewe.

Kuna ofisi unaweza ukahangaikia kibali hadi chozi likataka kukutoka, hiyo cha mtoto, na miradi ya mamilioni inakwama, ila inabidi ajue sasa kujipigania, mtaani its even worse.
Kwani mzazi kujali academic affairs za mwanae tena level ya chuo kikuu kuna shida gani ? Akionesha concern kwa masahibu yanayomkuta mwanae ni kosa ?
Acheni mazoea.
Kama mzazi wako hakuwa concerned wakati unasoma chuo ni wewe.
 
Kama ulitelekezwa na wazazi wako kaa kimya, Kama unadhani siku hizi masters wanasoma wazeee nyambafu yako

Na kama unadhani yupo mzazi analipa milioni nane Hadi ishirini gharama za masterz na mtoto wake akwamishwe na kiumbe mmoja mbinafsi shenzi type.

Tumieni common sense,
Safi kabisa.

Hawa wanaandika tu ila hawajui uchungu wa kuzisaka pesa. Siwezi kutoa milioni 16 za master's degree kwa mwanangu afu kila siku sound nikakaa kimya. I'll never do that asilani.

Nimeipenda comment yako anyway. Agiza carton ya yoghurt nakuja kulipia
 
Mkuu unam dhalilisha mwanao,Level Ya Masters hawez tatua matatzo yake ya academic, had wee uingilie sa atakua lin??
Mtoto hakui Kwa Mzazi ndio.. sasa kama Mzazi ana P.H.D na anajua utaratibu kwanini aruhusu mtoto wake akwamishwe..

Ushaambiwa supervisor hapokei simu wala kujibu email.. sasa kama sio uvivu ni nini, kwanini MTU unakuwa Doctor alafu Una poor time management skills??..

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
Kwani mzazi kujali academic affairs za mwanae tena level ya chuo kikuu kuna shida gani ? Akionesha concern kwa masahibu yanayomkuta mwanae ni kosa ?
Acheni mazoea.
Kama mzazi wako hakuwa concerned wakati unasoma chuo ni wewe.
Nilichoandika umekielewa, sihitaji kufafanua, maana jibu la hii hoja yako lipo kwenye hiyo hiyo comment uliyo-quote
 
Hizi elimu za masters sijui PhD sizikubali kabisa
Siku nikirudi darasani basi itakuwa kuna ka course cha ufundi nimeamua kukasoma ambacho najua katanisaidia huko baadae kwenye kujiajiri
Unatoa mil 10+ kwenda kuandika ma essays.
Degree inatosha
(Mtazamo wangu lakini..)
 
Mtoto want amesoma masters mwaka Sasa hata proposal ya masters haijavuka kwa supervisor, kila akimcheki supervisor hakuna email reply Wala wala apokei simu.

Nikafunga safari kwenda naye chuo kuuliza tatizo ni nini? Watu tuliowakuta academic block walichosema unajua Hawa ma senior lecture na hata wengine hawa mnatakiwa mwende nao Polepole la sivyo mkiwashtaki kwa DVC academy akasikia mtoto wako atafudisco maana wanawasiliana.

Tuvumiliane tu tutamjulisha wenyewe supervisor wake. Kwa kuwa nilikuwa na jazba na Kuna wanafunzi walikuwa wanasikia majibizano Yale na baada ya kutoka nje ndipo nikapata ushuhuda wa Nini kinaendelea chuoni.

Kwanza, hakuna mtu anayesimamia wasimamizi wa wanafunzi ambaye anajua kazi hii imekaa kwa supervisor muda gani.

Pili, madaktari wengi wa UDsM wanaamini wao ndio wenye final say na wanawatisha wanafunzi kuwadisco endapo wakionekana kupingana au kulazimisha wahudumiwe

Tatu, tofauti na urasimu wa supervisors urasimu mkubwa zaidi upo kwa external supervisors ambao wamejiwekea muda wa miezi mitatu au sita kufanyia kazi utafiti uliowasihwa kwao.

Nne, hakuna kitengo cha ICT cha kufanya haya mambo kilicho serious

Tano, hakuna mwanasiasa Wala mtoto ambaye mzazi wake ni mtumishi pale anayekwamishwa wala kuchukua muda kurekebishiwa kazi yake kwa sababu wazazi au wahusika hutumia madaraka na Pr zao kuhudumia

Sita, kazi za wanafunzi zinavyowekwa hakuna utaratibu mzuri. Mwanangu alipewa kazi yakupekua box lina mamia ya kazi za watu...no secrettt

Mimi nimesoma nje miaka ya 1990 hakukuwa na urasimu huu, nimeangalia vyuo vingi ikiwemo hata open utaratibu upo streight....nenda suaut na kwingine utaratibu upo wazi. Kwanini UDSM wapo nyuma hivi?

Hawa supervisor na Urasimu wao ndio wanaotegemea kuteuliwa kwenda kuongoza taasisi za umma? Nadhani kigezo Cha utendaji kazi kiwe msingi wa kupandishwa cheo siyo kazi binafsi za supervisor anajaza cv huku aliopaswa kuwahudumia akiwakwamisha kisa yupo busy na kazi zake binafsi. Haujaariwa chuoni kujiendeleza umeajiriwa kusaidia watu.

Masters 4yrs ,Phd 8 yrs unatafiti Nini? Na kibaya zaidi research paper zao hazina hata ubora wa uandishi kama za vyuo vingine useme wana ubora. Kawaida kabisa.

Mzee Rutinwa simamia watu wako wapitishe kazi za wanafunzi waache uungu mtu
Mpeleke akasome Masters ustawi
 
Back
Top Bottom