Unapomleta Diwani wa CUF kuizodoa CHADEMA jukwaani, wenye busara wanakushangaa

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,501
37,793
Leo kwenye kampeni za CCM kumetokea kituko ambacho ni dhahiri sasa kina Polepole wameshajua jinsi ya kuchota akili za Mgombea wao ni kutengeneza matukio hata ya uongo ili kumfurahisha kwa vile wanajua anapenda sifa hata zisizokuwepo.

Leo kabla ya Mh. Magufuli kupanda jukwaani alipandishwa mtu aitwaye OMARY KUMBILAMOTO kutoa kilivhoelezwa na wapambe, "Jinsi CHADEMA ilivyokuwa ikipanga njama kuhujumu miradi ya maendeleo ili ionekane mbele ya wananchi serikali ya awamu ya tano inafeli kuwahudumia wananchi". OMARY KUMBILAMOTO;

1. 2015 alichaguliwa kuwa diwani wa Vingunguti kupitia CUF na siyo CHADEMA na akiwa ametokea CCM kujiunga CUF.

2. Alichaguliwa kuwa naibu Meya kwa mwavuli wa UKAWA kama shukrani kwa muungano wa vyama vilivyopigania katiba mpya yenye maoni halisi ya wananchi.

3. Hakuwahi kuwa Meya wa Ilala kwa tiketi tiketi ya upinzani Bali naibu Meya kama nilivyosema hapo juu.

4. August 2018 alijiuzulu nafasi yake na hatimaye akajivua uanachama wa CUF na baadaye akarejea kwao (CCM) ambako alipewa nafasi ya kugombea tena Udiwani wa Vingunguti na kupita kwa mbeleko wakati wa wimbi la biashara ya manunuzi ya wapinzani. Sababu alizozitoa wakati anajiuzulu ni kwamba amekuwa akipata vitisho toka kwa wenzake kwa sababu ya kuunga mkono Serikali.

5. Alichaguliwa kwa figisu kuwa Meya wa Ilala kwa tiketi ya CCM.

Sasa kwa hayo machache tu:

1. KUMBILAMOTO anapata wapi udhu wa kuisemea CHADEMA mabaya utadhani amewahi kuwa mwanachama mwandamizi hata ngazi ya kata?

2. Kujiita Meya wa upinzani huku akijua aliishia Unaibu Meya akiwa upinzani ni uongo unaotosha kuonesha waliomleta wamefilisika kipropaganda.

3. Tangu ajiunge CCM ni takriban miaka 2 sasa, na hajawahi kusema upuuzi aliolishwa Leo.

4. Wanaopanga propaganda za kitoto kama za leo wanadhani Watanzania bado ni wajinga na wafuata upepo kama wa enzi za Zidumu

Fikra sahihi.

Screenshot_2020-10-12-16-32-49.jpg
 
Kawaida tu.

Jamaa mmoja aliwahi kugombea tu kaudiwani.

Alipokuja PM akajifanya anarudi CCM wale maMC wanampiga kwamba PM eti jamaa aligombea Ubunge upinzani sasa hivi karudi CCM.

Pale wote huwa wanajua wanachokifanya maana wanaopangwa hapo ni wale wafuasi maandalizi uninformed na fuata upepo ambao kwenye kampeni huwa ni kama 90% hivi.
 
Back
Top Bottom