Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Mimi wa kwangu nikimuona sasa hivi najiuliza hivi macho yangu yalikuwa na matatzo gani nilikuwa ninaona nini kwake
Secondary's Crush Sophia Mungu anakuona.
Alijua kabisa mimi ni domo zege ila akawa anajifanya haoni richa ya kumwandikia sana noticies za Biology na michoro kama yote. Nimeandika sana vinemo katikati ya daftari lake la Bios ila anauchuna tu. Nilimpenda sana nikapenda mwandiko wake nikapenda hadi mtaa aliokua anaishi. Kuna wakati nilikua Natamani sana niisukune nyumba yetu hadi mtaani kwao niwe namuona....Nilimchukia baba kwakutokununua kiwanja mtaani kwa Sofia

2019 alinitafuta baada ya miaka mingi kupotezana ila sikua nampenda hata robo .
Hapo kwenye ubovu ndio tunaungan na nyinyi yaani nikikutana nae najiulizaga nilivurugwa na nini kwake?
 
Aliniandikia Hadi barua

"nikiwa mkubwa nitavaa suruali za kubana ili unipende"
kipindi hiko suruali za kike tarumbeta ndio zinaingia ingia

Nafahamu huwezi kukosa humu niko na picha zako tulizopiga na mapengo yako Uko pembeni yangu unafurahiiiiii baada ya kukutoa out na kukununulia pipi 😅.....
 
Primary nilipenda binti Fulani anaitwa Angel she was very cute wakati huo ila now namuona wa kawaida sana alinitesa haswa huyu Crush na wakati huo mimi pia napendwa sana sana na Beatrice halafu siña muda nae, Kufika la Sita wote tukahama mikoa nimekuja kukutana na Angel wakati ana graduate chuo kikuu siku ya Graduation na Game akanipa bila Hiana niliforce game kwa vile utotoni kule hakukuwa na mishe za kula mzigo,Alitaka Kufall nkamuambia hapana Ntamtesa ya utoto yameisha nilikula mzigo siku tatu nonstop after all tumebaki as friends tu
 
Jamani nikiwa primary yule kijana alikuwa siwezi kufika shule asubuhi bila kwenda kumsalimia.Duu after primary kila mtu kivyake tumekuja kuunda grp la primary after 20yrs plus mtu wakwanza kumwulizia was him .

Nilisikitika nilivyoambiwa amepata stroke yupo tu kitandani sijawahi kudhubutu kwenda kumwona ila niliulizia anapokaa nikaambiwa nikawa napita nimwone siku moja nilimwona anafanya mazoezi barabarani huku amesaidiwa nilisimama sikuweza kusema chochote anyway nimeolewa nampenda mme wangu.Maisha nikitendawili
 
Richie W. aka Richie Richie ( huyu tulipendana wote hadi tunamaliza lasaba B ila wote tulikuwa tunanata hakuna aliyetaka kumsemesha mwenzake. Tukawa tukasalimiana tuu na kupeana tabasamu basi). Sekondari tulipangiwa shule jirani tukawa tunaonana njiani saa ya kutoka au asubuhi kuingia shule.... alipopangiwa Minaki tukapotezana mazima hadi leo. Nilifatilia post za A level shule yao nikajua kapangiwa Minaki.... crush ya primary ikaishia hapo.)

Nkundwe ....( huyu hakujua kama nilimzimikia ila sababu alikuwa handsome waschana wengi walikuwa wanamsonga.... sikumbuki vizuri kama alihama tukiwa lasaba B au baada ya hapo alihamia ughaibuni.

Baada ya hapo nikawa mkaksi hadi nilipoingia chuo ndo nikaanza mahanjam 😋.
 
Jamani nikiwa primary yule kijana alikuwa siwezi kufika shule asubuhi bila kwenda kumsalimia.Duu after primary kila mtu kivyake tumekuja kuunda grp la primary after 20yrs plus mtu wakwanza kumwulizia was him .Nilisikiyika nilivyoambiwa amepata stroke yupo tu kitamdani sijawahi kudhubutu kwenda kumwona ila niliulizia anapokaa nikaambiwa nikawa napita nimwone siku moja nilimwona anafanya mazoezi barabarani huku anasaidiwa nilisimama sikuweza kusema chochote anyway nimeolewa nampenda mme wangu.Maisha nikitendawili

Life is full of mysteries and uncertainties....
 
Asikwambie mtu, yule crush wa utotoni hasa mara nyingi inakua shule ya msingi ni mapenzi ambayo yanavuruga sana hasa ukizingatia mara nyingi mtu mabae unampenda anakua hana ata habari au aanajua unampenda ila hana habari na wewe yuko busy na yeye na crush wake.
Nakumbuka nilipokua darasa wa tano ndo nilikua na crush huyo then kwao alikua kuna duka, bas kama siku sijaenda shule na sijamuina ni lazima nitoke nikamuone hata kama sikua na nia ya kununua kitu, bahati mabaya ilikua ni kijijini kwao hadi ufike unapita kwenye mapoli ila ilikua niko radhi, nakumbuka kuna siku nyingine nakwenda dukani usiku ili nimuone lakini nikitifika unakuta hayuko dukani unakuta mama yake au ndugu zake wengine, ila hata nikisia sauti yake tu huko ndani basi nakua na furaha.
sikuwahi kumueleza kua nampenda mana nilikosa lakusema nilipokua karibu yake, now ameolewa na hatuna mawasiliano ila mpaka sasa sijawai kuona ile hali tena . hakika yale yalikua true unconditional love.
Uzuri ma crush wangu wote nao walikuwa wananipenda ila tunaogopana tu 😻
 
Nimekumbuka kuwa tabia niliyo nayo kwa sasa kuhusu mtazamo wa mahusiano kumbe ni tangu zamani, nakumbuka sikuwahi kuwa na crush primary. Najikubali msimamo wangu tangu utotoni.
Daahh Mimi niliwahi kuwaga na crush let me declare the truth .. katika maisha yangu sijawahi kupenda kwa kiwango kile tena Kama jinsi nilivyo wahi kumpenda yule binti Nyie mapenzi before ya kubakwa na majukumu + maumivu ya walimwengu Ni matamu sana acheni tu
 
Back
Top Bottom