Unamfungulia mtu moyo wako, anaingia na kuutesa

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,340
1,377
Sidhani kama ni mimi pekee nimekumbana nalo.

Anakuja mkaka anakutaka urafiki na kwenye mazungumzo unamfeel na baada ya muda unampa ok. Mapenzi yanaanza kuwaka, mapenzi yako yote na ya akiba unampa. Kumbe bila wewe kufahamu umekaribisha jehanam moyoni mwako. Baada ya mwezi unaanza kusikia stori za ajabuajabu juu yake.

Mara eti kaonekana na msichana fulani mahali fulani, unaunganisha na jinsi simu zake zilivyopungua ghafla unaanza kusikia tumbo kama la kuharisha vile. Ukimwuliza ni mahugs na makisses: "baby mbona una wasiwasi na mimi? I cant do stupid things like that!" Unamwamini unanyamaza, si unampenda.

Siku ya siku rafiki yako anakustua: "Nai vipi, wewe na F mmeachana?" Katika kumchunguza rafikiyo anakuambia F sasa yuko na Joyce na keshakwenda kwao kutambulishwa. Unapatwa na kizunguzungu kikali unajisikia kuanguka chini. Unachunguza unagundua ni kweli. Unatamani kumwagia F petroli na kumtia kibiriti. Hilo unashindwa kufanya ila unamtoa kabisa F moyoni mwako for ever and ever! Kwa ujumla hayo ndio mahusiano niliyokumbana nayo kwa miaka 4 sasa, tangu 2012.

Shida ondoka moyoni mwangu, nataka raha.

 
Kwa uzoefu wangu, wanaume wapitaji na wenye nia ya kuchezea mabinti hujifanya wanamapenzi ya hali ya juu mno, tena wanajali utafikiri wamezaliwa Tanga. Wanajua kuwa kwa gear hiyo mabinti hawawezi kuchomoka. Ndio hapo mwanzo wa maumivu.

Muoaji au mwanaume aliye serious hana haja ya ku fake au kukuhadaa anakuja kama alivyo, anachojua yeye ni kutengeneza future na wewe, tatizo nyie wadada hamuwaelewi wala hamvutiwi na wanaume wa aina hiyo.
Mwisho wa yote, inahitaji hekima na busara sana kujua nani mkweli nani muongo, it begins with you.

Pole sana, umeanguka usibaki chini, inuka endelea na safari, chukulia hili tukio kama somo.
 
Daah pole sana, lakini iwe somo kwako na wasichana wengine, kuweni makini na wanaume babaishi acheni maisha ya kuigiza kwny tamthilia, vijana wengi ni waongo wamejaa tamaa za mwili, lakini unakuta kabinti kamo tu, na huku dalili zote za uongo na maigizo yakiwa wazi, lakini hamkomi kabisa, watu wanacheza na maisha yako wala hamstuki, but inasikitisha sana
 
Don't be too serious in relationships kwa sasa, utalia kila siku. Maisha yalivyo magumu halafu uanze kunigandaganda kisa hubby sijui madudu gani.

Ukitaka uwe na Amani take it easy ikitokea mmemove forwad poa ila akizingua unajua tu ndo wale wale.

Pia ifike wakati wadada muanze kutongoza, hii itasaidia kuwa na watu mnaowataka na ambao ni sahihi.
 
Back
Top Bottom