Unalalamika then unasema bajeti itapita 100% nini maana yake?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
JF wadau

kuna jambo bado silielewi juu ya wabunge walio DODOMA ktk kipindi cha bajeti,utasikia mbunge anasema naunga mkono bajeti kwa 100%,lakini mwisho wa siku mbunge huyohuyo analalama kuwa jimbo langu ni masikini,halmashauri ni kubwa pesa ni ndogo,maji ya tuwasa hayatoshi,kata ni nyingi lakini mwisho wa siku unasikia naunga mkono hoja sasa nini maana yake?
 
wana JF nahitaji msaada mkubwa sana kwani naona ueklewa wangu kwenye hili jambo linalofanywa na wabunge huko Dodoma na hasa jioni hii nimemshuhudia mbunge wa Kishapu,mh Nchambi,amelalamika sana tena kwa uchungu mkubwa sana na amebainisha matatizo yote yaliyoko jimboni kwake na baadae akazungumzia matatizo ya mikoa inayolima pamba,na kiukweli matatizo yaliyoko jimbo la kishapu ambayo ni wilaya ya Kishapu ni matatizo nadhani yanaongoza nchi nzima,kula kuna matatizo ,makubwa sana ya afya,elimu,ukame na miundo mbinu,naongea kwa uhakika sana maana naifahamu wilaya ya Kishapu in details,lakini mwisho wa siku ameunga mkono hoja kwa 100% Je maana yake ni nini?mimi sijaelewa kabisa na wabunge wengi wa Nyinyiemu wanasimama wanalalamika kisha wanaunga mkono hoja,je hii ina maanisha nini?ni kwa faida yanani?
Kwa wale wanaolijua jimbo la kishapu naomba mnisaidie kwa stahili hii kishapu itajikwamua?kumbuka huko ndiko ambako zimeliwa billion sita za maendeleo katika halmashauri ya Kishapu.kwa wale mnaotoka huko na mnaolijua jimbo hili please comment something about MP huyu.
 
Back
Top Bottom