Unaifahamu vipi CocaCola?

Huu ni uzushi tu.

Sasa kama ni wawili tu wanaojua, hawa wa hapa nyerere road wanatumia compounds zip kuipata coca??? Na wakati hawajui??? Au inashushwa na ndege na kujazwa ktk vyupa???
Ni unga wake ndio unaosambazwa wao wanachanganya na kikiminika tu ili kupata kinywaji
 
Yule muhindi wa Sunkist alikufa na Siri yake
Mikate haina ubora tena
Sasa Hao wa coca hawafagi?
 
Waku, suala la usiri wa formula ya coca cola sio conspiracy theory, ni suala halisi kabisa.


Katika ulimwengu wa 'ushushu wa kibiashara' kuna terminology maarufu inaitwa "Trade Secret"..

Trade secret - ni mbinu au namna ya ufanyaji jambo au mchakato au kifaa au formula au taarifa za siri zinazotumiwa na kampuni husika katika uendeshaji wake biashara au utengenezaji wa bidhaa zake na kuiweka kampuni hiyo katika nafasi nzuri ya kuwashinda washindani kibiashara.

Sasa mojawapo ya 'trade secret' zinazolindwa zaidi ulimwenguni ni viungo (ingredients) zinazotumika kuchanganywa kwenye kinywaji cha Coco Cola na kukifanya kuwa na ladha tofauti na vinywaji vingine vyote duniani. Viungo hivi vya siri vinavyo changanywa kwenye coca cola vinajulikana kama '7X'.

Sasa kampuni mama yenyewe ya coca cola huko marekani wao wanatengeza 'concentrate' yenye viungo hivi na kuwauzia 'bottlers' wenye vibali kutoka kwao kila pembe ya dunia ambao wao wanachanganya 'concentrate' hiyo na maji (carbonated water) na kuongeza kiwango cha sukari na kusindika kisha kuuza kwa walaji..

Ndio kusema kwa mfano, Bonite Bottlers ya Bw. Reginald Mengi wao wananunua concentrate kutoka makao makuu marekani na kuchanganya na maji na sukari na kuuza kwa walaji.
Mfumo huko hivyo Dunia nzima kila unapoiona coca cola.

Wapo 'majasusi' wa kibiashara kwa kushirikiana na wanasayansi wamefanikiwa kucrack hii ingredient lakini bado kitendawili kinabaki kuhusu viwango na namna ya uchanganyaji wa viuongo hivyo.

Ni wafanyakazi wachache sana (wengi husema watu wawili tu) kwa muda husika ndio hupewa siri ya ingredient ya '7X' inayotumika kutengeneza concentrate inayoipa coca cola ladha yake ambayo ni tofauti kabisa na vinywaji vingine vyote na siri hii inabakiwa kuwa moja ya 'Trade secret' inayolindwa zaidi.

The Bold.


Cc: minji, Nifah, kbosho, Adolph Hitler Jr
Safi sana Bro. ...maelezo yako yamenishawishi...coz dunia ya leo isingeshindikana kuzitambua hzo ingredients..na wanazijua ila jinsi ya kutumia ili kupata az a original coca cola ndo tatizo
 
Back
Top Bottom