Unafiki wa baadhi ya Maaskofu wa Tanzania

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Kwa kutambua umuhimu wa haki za kibinadamu katika misingi ya kiimani, waasisi wa taifa letu waliamua kuwapa wananchi religious freedom katika mstabali wa maisha yao.

Kwa sasa tunachokiona kutoka kwa viongozi wa kidini ni madai ya kutaka absolute religious privilege katika serikali kana kwamba serikali ina dini wakati ni secular state.

Nimeshangazwa na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la tarehe 18 Machi 2015 lenye kichwa cha habari kinachosema, ''Askofu Niwemugizi amjibu Migiro''.

Kusoma habari hiyo gonga
HAPA

Huu ni upofu au unafiki wa kiwango cha juu kutoka kwa Askofu Seveline Niwemugizi kwa sababu kile alichokuwa anamjibu Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro ni marudio ya yale yalisemwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo siku mbili zilizopita.

Mpaka sasa hakuna mchungaji au Askofu aliyejitokeza hadharani na kupambana na hoja za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, badala yake baadhi ya viongozi wa dini kama Askofu Seveline Niwemugizi are picking on easy target just to feel better, popular and seen as tough or cool in our society.

Hakuna mpaka sasa kiongozi wa dini mwenye ubavu wa kujitokeza na kujibu hoja za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo badala yake viongozi wa dini kama kama Askofu Seveline Niwemugizi wanatafuta easy target.

Maneno ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambayo ni makali, yamevunja vunja na kulitupilia mbali hitimisho la barua za kichungaji ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na ile ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ya kuwataka waumini kujiandikisha na kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayondekezwa.

Kuna wale baadhi ya watu waliojaliwa fikra finyu na wasiofahamu umuhimu na uwepo wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika kanisa, watayapuuza maneno yake lakini waliyojaliwa fikra pevu lazima wayafanyie kazi katika msingi wa fikra pevu ndiyo maana viongozi wa dini kama Askofu Seveline Niwemugizi wanajificha na hoja zao kwenye vivuli vya maneno ya wanasiasa.

Msingi mkuu wa uwepo wa kanisa ni kuwaunganisha waumini katika msingi wa imani na siyo kuwatenganisha waumini katika msingi wa siasa.

Mapenzi ni kama kipofu!

Baadhi ya viongozi wetu wa kiimani wamezipenda siasa mpaka hawaoni misingi wa uwepo wa kanisa.

Mwingereza aitwaye Lord Acton aliwahi kusema, Power corrupts, and absolute power corrupts absolutely.

Baadhi ya viongozi wetu wa dini kwa sasa wamekuwa na nguvu kubwa katika mstakabali wa nchi kupitia imani mpaka wanataka kuanza kuwaamulia kwa nguvu wananchi wote nini cha kutenda katika maisha yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kukubaliana na mawazo kama haya, kesho kuna viongozi wa dini wengine watasema wanataka Watanzania wote wawe wakristo au Waislamu kwa sababu kuwaacha wakiwa na imani nyingine ni kuwafanya wapotee wakati wao kama viongozi wenye ''maono'' wako kimya.

Kukubaliana na mawazo kama haya, kesho kuna baadhi ya viongozi wa dini watakuja na kusema lazima Rais wa nchi awe fulani kwa sababu hawawezi kuwaona kondoo wa bwana wanapotezwa nchini.

Maneno ya Mwadhama Polycarp Pengo yameziba ufa wa kiimani unaosababishwa na viongozi wa dini ambao ni wanafiki ili kesho taifa lisije likashindwa hata kujenga ukuta wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Haya maneno ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo yamebeba ujumbe wote;

"Kuwaambia sisi kama maaskofu tunasema mwende mkapige kura ya hapana na kwa nini tuwafanye hivyo waamini wetu? Tuwafanye watoto wadogo ambao ni lazima kuwaambia mwende mkapige kura ya hapana, hili ni jambo ambalo linadhalilisha uhuru wa wana wa Mungu ndani ya waamini wetu, hatuna uwezo wala hatuna haki ya kuwaambia mwende mkapige kura lakini kura hiyo iwe ya hapana, na kwa nini iwe hivyo? Je, waumini wetu ni watoto wadogo wasioweza kufikiri na kutafakari wao wenyewe kiasi kwamba tuwaambie nendeni mkapige kura ya hapana, tumeipata wapi haki hiyo? Hilo ni swali muhimu sana.

Tukio la mwisho ni kwamba linagawa taifa letu kati ya wakristo na wasiokuwa wakristo matokeo yake tunaweza kuyafikiria sisi wenyewe. Vile vile linagawa wakristo kutoka kwa serikali yao jambo ambalo kwa kweli haliwezekani, ndani ya serilali yetu ya Tanzania katika uongozi wake wako waamini wetu wakatoliki na wapo waamini wakristo wasio wakatoliki, kusimama na kuwaambia kanisa linasimama dhidi ya serikali, kuwaambia ninyi pia tunasimama kinyume chenu, sasa sijui hao viongozi wakristo wafanye nini? Waasisi imani yao wasimame upande wa serikali au watoke serikalini wasimame upande wa imani yao? Wachague lipi kati ya hayo?
 
Kanisa ni janga tangu enzi za ukoloni, Nyerere akaja kupigilia msumari wa mwisho
 
MKUU andiko lako ni ukweli mtupu, hoja za Dr. Migiro ni marudio ya alichosema Pengo, cha ajabu eti Askofu kamjibu migiro baada ya kadinal...
 
itabaki palepale ninyi ccm mmepata wapi ujasiri wa kuwasemea wananchi eti wapigie katiba ya hovyo kura ya ndiyo?
Ndugu;
Hoja kama hii ni kina kirefu kifikra kwa watu wa aina ya fikra kama zako.

Huhitaji kuchangia kama unafahamu uwezo wako kifkra.

Hata kusoma tu inahesabika kama ni moja ya kutoa mchango kifikra.

Jambo la msingi kabisa linalosababisha matatizo hapa duniani leo ni kwamba wajinga wanajiamini sana wakati wenye maalifa wamejaa shaka-Bertland Russell
 
MKUU andiko lako ni ukweli mtupu, hoja za Dr. Migiro ni marudio ya alichosema Pengo, cha ajabu eti Askofu kamjibu migiro baada ya kadinal...

Ameua ndege wawili kwa jiwe moja kama kweli hoja za Migiro ni marudio ya alichosema Pengo. Hakuna cha ajabu hapo wote wamepata majibu,
 
Ndugu;
Hoja kama hii ni kina kirefu kifikra kwa watu wa aina ya fikra kama zako.

Huhitaji kuchangia kama unafahamu uwezo wako kifkra.

Hata kusoma tu inahesabika kama ni moja ya kutoa mchango kifikra.

Jambo la msingi kabisa linalosababisha matatizo hapa duniani leo ni kwamba wajinga wanajiamini sana wakati wenye maalifa wamejaa shaka-Bertland Russell

Fikra gani ulizonazo zaidi ya propaganda tu?
 
Inawezekana pengo akawa sahihi kwa namna moja ama nyingine. Je ccm na viongozi wa serikali wanapata wapi ujasiri watanzania wapigie kura ya ndio katiba hii ya mafisadi kina chenge?
 
Hahahahaaaaaa ama kweli tembea na mke wa mtu sawa ila mtu akitembea na mkeo ni kosa, ndicho ninacho kiona, wanaopiga kampeni wananchi wapige kura ya ndio wako swa ila wanaosema hapana wapotoshaji. Hii ndio Tanzania
teh teh, mkuu huu ndo unafiki wa mtoa mada! Sipati picha kama tec wangeunga mkono hii katiba ya chenge sijui lumumba wangetoka na hili andishi ama!
 
MKUU andiko lako ni ukweli mtupu, hoja za Dr. Migiro ni marudio ya alichosema Pengo, cha ajabu eti Askofu kamjibu migiro baada ya kadinal...

Tatizo lako hujui kwamba tamko rasmi la Kanisa Katoliki utolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu
ama Makamu wake na likiwa na sahihi za Maaskofu wote. Kwa hiyo haya unayo tuletea hapa ni maoni binafsi ya Mtanzania anayeitwa Polycap Pengo.
 
Kwa kutambua umuhimu wa haki za kibinadamu katika misingi ya kiimani, waasisi wa taifa letu waliamua kuwapa wananchi religious freedom katika mstabali wa maisha yao.

Kwa sasa tunachokiona kutoka kwa viongozi wa kidini ni madai ya kutaka absolute religious privilege katika serikali kana kwamba serikali ina dini wakati ni secular state.

Nimeshangazwa na habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania la tarehe 18 Machi 2015 lenye kichwa cha habari kinachosema, ''Askofu Niwemugizi amjibu Migiro''.

Kusoma habari hiyo gonga
HAPA

Huu ni upofu au unafiki wa kiwango cha juu kutoka kwa Askofu Seveline Niwemugizi kwa sababu kile alichokuwa anamjibu Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro ni marudio ya yale yalisemwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo siku mbili zilizopita.

Mpaka sasa hakuna mchungaji au Askofu aliyejitokeza hadharani na kupambana na hoja za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, badala yake baadhi ya viongozi wa dini kama Askofu Seveline Niwemugizi are picking on easy target just to feel better, popular and seen as tough or cool in our society.

Hakuna mpaka sasa kiongozi wa dini mwenye ubavu wa kujitokeza na kujibu hoja za Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo badala yake viongozi wa dini kama kama Askofu Seveline Niwemugizi wanatafuta easy target.

Maneno ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ambayo ni makali, yamevunja vunja na
kulitupilia mbali hitimisho la barua za kichungaji ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na ile ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ya kuwataka waumini kujiandikisha na kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayondekezwa.

Kuna wale baadhi ya watu waliojaliwa fikra finyu na wasiofahamu umuhimu na uwepo wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika kanisa, watayapuuza maneno yake lakini waliyojaliwa fikra pevu lazima wayafanyie kazi katika msingi wa fikra pevu ndiyo maana viongozi wa dini kama Askofu Seveline Niwemugizi wanajificha na hoja zao kwenye vivuli vya maneno ya wanasiasa.

Msingi mkuu wa uwepo wa kanisa ni kuwaunganisha waumini katika msingi wa imani na siyo kuwatenganisha waumini katika msingi wa siasa.

Mapenzi ni kama kipofu!

Baadhi ya viongozi wetu wa kiimani wamezipenda siasa mpaka hawaoni misingi wa uwepo wa kanisa.

Mwingereza aitwaye Lord Acton aliwahi kusema, Power corrupts, and absolute power corrupts absolutely.

Baadhi ya viongozi wetu wa dini kwa sasa wamekuwa na nguvu kubwa katika mstakabali wa nchi kupitia imani mpaka wanataka kuanza kuwaamulia kwa nguvu wananchi wote nini cha kutenda katika maisha yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kukubaliana na mawazo kama haya, kesho kuna viongozi wa dini wengine watasema wanataka Watanzania wote wawe wakristo au Waislamu kwa sababu kuwaacha wakiwa na imani nyingine ni kuwafanya wapotee wakati wao kama viongozi wenye ''maono'' wako kimya.

Haya maneno ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo yamebeba ujumbe wote;
'''Msingi mkuu wa kanisa ni kuwaunganisha waumini katika imani na si kuwatenga katika misingi ya kisiasa''

Maneno hayo ungemwambia waziri William Lukuvi aliyekwenda kanisani kuwatenganisha si waumini wa wa dini moja, bali waumini wa kikristo na Waislam katika msingi wa siasa, mchana kweupe(video zipo tele JF)

Hapa wewe ndiye mnafiki mkubwa, usiweza kumkemea waziri anayechochea vurugu bali maaskofu wanaosema

Pili, TEC na CCT walishatoa waraka uliosaniwa na maskofu 30(kama namba ni sahihi) akiwemo Polycap Pengo

Hivyo, Pengo anapowakana wenzake ni mnafiki kwanza kabla ya wanafiki unaosema

Kwavile anacheza ngoma na mirindimo ya William Lukuvi, leo ni shujaa wenu

Pengo alipokemea rushwa na maadili mabovu ya serikali, mlikaa kimya mkisema dini zitenganishwe na siasa.
Leo ni shujaa wenu.

Usichokielewa ni kuwa mwakilishi wa wakatoliki alikuwepo katika mkutano.

Hivyo kanisa liliwakilishwa tena Pengo akijua.

Hayo aliyoyasema hayana tofauti na zile kauli za Pengo kuwa nchi iwe na serikali 2.

Wakati anaamua nchi iwe na muundo gani, wanafiki mlikuwa kimya bila kukemea jinsi anavyoamulia watu.

Leo mnarudia kusema kile kile alichowahi kukitenda.

Hivyo, jisafishe kwanza kwa unafiki wa kumwacha Lukuvi aharibu taifa, ukitaka njoo hapa tujadiliane ya wengine
 
Kanisa ni janga tangu enzi za ukoloni, Nyerere akaja kupigilia msumari wa mwisho
Ndugu;
Ninaamini kanisa kama kanisa siyo janga, bali baadhi ya viongozi wa kanisa ndiyo majanga kwa mstakabali wa taifa.
 
Back
Top Bottom