Unachukua hatua gani unapokutana na taarifa potofu mtandaoni?

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
1709123622903.jpeg

Kupata habari ndani na nje ya mtandao imekuwa sehemu ya maisha yetu, ni kawaida kwenye mitandao ya ijamii na kwenye makundi sogozi ya WhatsApp, Facebook na Telegram kukutana na habari za uongo au zinazotia mashaka.

Je, huwa unachua hatua gani unapokutana na habari za uongo au zinazokupa mashaka mtaani au mtandaoni?

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.

Soma:
- Hatua za kuchukua unapohisi Taarifa ni Potofu
 
Nyie huwa mnazengua. Habari za upotoshaji zimejaa humu mpaka karaha kabisa, na huwa zikiripotiwa huwa na hamfanyi chochote.

Mfano, kumeandikwa hapa na Daktari wenu kuwa Mtu Mweusi sio Binadamu kamili.

Kuna ukweli gani au msingi gani wa kisayansi unaosema Mtu mweusi sio binadamu kamili kama sio upotoshaji wa makusudi?

Sio hivyo tu, madhara yake kisakilojia kwa vijana ni hasi.

Vijana wanaanza kukosa self esteem, ndio mnaona wanaanza kujichubua n.k

Niseme tu, huwa mnajikoga tu humu...
 
Cha kwanza lazima utafute habari yenye ukweli ili ujiridhishe kutoka eneo unalodhani taarifa hiyo imetokea, kwa lugha pendwa (balancing story)
 
Nafikiri swali liwe Jukwaa la Jamiiforums huwa linachukua hatua gani pale linapotumika kuwa Jukwaa la kudekeza habari na Taarifa za Uongo.

Kitaeleweka
 
Back
Top Bottom