Umoja wa nchi za Ulaya `yaipiga jeki` Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,442
33,335
William%20Mgimwa(1).jpg

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa


Tanzania imepokea msaada wa Sh. bilioni 101 kwa ajili ya kuboresha miradi ya msingi katika mpango wa Millenia wa kukuza na kupunguza umaskini (Mkukuta), kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya (EU).

Akizungumza wakati akipokea hundi ya fedha hizo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema wamepokea fedha hizo ambazo ni kati ya bilioni 654.7 walizoahidiwa na Jumuiya hiyo mwaka 2009.
Alisema tangu kipindi hicho mpaka sasa, tayari serikali imepokea Sh. bilioni 507.7

Baadhi ya maeneo yaliyopewa kipaumbele katika msaada huo ni sekta ya elimu, afya hususani kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto, maji na sekta ya miundombinu.

"Tunahitaji kuwa na kasi ya kuondoa umaskini, na ndiyo maana tunaamua kuzungumza na wenzetu ambao tunashukuru wametusaidia," alisema.

Kadhalika, alisema lengo la serikali ni kuweka mikakati ya kupunguza utegemezi wa misaada kutoka nje. Kadhalika alisema deni la serikali linalotokana na mikopo mbalimbali za nje ni Sh. trilioni 41.



CHANZO: NIPASHE

JE NI KWELI SERIKALI ITAWEZA KUONDOWA UMASIKINI NCHINI TANZANIA? JIBU NI NDOTO ZA MCHANA
 
Back
Top Bottom