Umewahi Kujiuliza kwanini MIKATE Haiandikwi Expiring DATE?

Siku utakapoharisha ndiyo Utajulishwa Expiring date Ya Huo Mkate Itakuwa Lini Sawa?
 
Hallo Wana JF.

Nimeona sio vibaya tukajadili hili suala.
Mara Nyingi nikiwapo nyumbani, kabla ya kifungua kinywa, ukimtuma DADA/MSAIDIZI
dukani kwa ajili ya kununua Mkate Mara nyingi huwa wanambambika Mikate ya Juzi.
Na Mara nyingine humpatia hata ile ambayo Imekauka kama Biscuits na mingine inakuwa ishaota Ukungu wa FUNGUS.
Ukirudisha ndio Mwenye Duka naye anajifanya kushangaa kuwa hakuona pia.

Naona ifikie hatua sasa Mikate nayo iwe Na MFG DATE and EXP DATE kama ilivyo kwa bidhaa nyingine,
la sivyo tutakuwa tunalishana Sumu huku mitaani.

Sijui ni Mamlaka ipi hapa inayohusika ili lawama zielekezwe kwao(TBS or TFDA).

Naomba tuelimishane kuhusu hili kama nawe umeshakuwa mhanga wa hili.

Thanks.

dada /msaidizi_vimeniboa sana, kwnn usiweke dhana ya wewe/mkeo/mwanao_hakuna haja ya kujua life style yako wakat ukieleza jambo au kujielezea ulivyo
 
Kweli hii ni hatari. Japo hapo ninaponunua mikate huisha mapema sana na ukichelewa hupati lakini hili limenistua sana. Nimejaribu kucheki mkate hapa nyumbani hauna tarehe ya kutengenezwa wala tarehe ya kuisha kutumika. Ni mikate gani yenye kuandikwa hizo tarehe?
 
Kwani mingine ni ya wapi? bekari ni sehemu ambapo mikate hutengenezwa, ukishasema mkate maana yake umetengezwa bekari sasa unaposema wanunue ya bekari unakua husomeki, labda hujui maana ya bekari!!

Ingawa ni vyema umemuelewesha lakini najua wajua hakuwa na maana hiyooooo....
 
Hallo Wana JF.

Nimeona sio vibaya tukajadili hili suala.
Mara Nyingi nikiwapo nyumbani, kabla ya kifungua kinywa, ukimtuma DADA/MSAIDIZI
dukani kwa ajili ya kununua Mkate Mara nyingi huwa wanambambika Mikate ya Juzi.
Na Mara nyingine humpatia hata ile ambayo Imekauka kama Biscuits na mingine inakuwa ishaota Ukungu wa FUNGUS.
Ukirudisha ndio Mwenye Duka naye anajifanya kushangaa kuwa hakuona pia.

Naona ifikie hatua sasa Mikate nayo iwe Na MFG DATE and EXP DATE kama ilivyo kwa bidhaa nyingine,
la sivyo tutakuwa tunalishana Sumu huku mitaani.

Sijui ni Mamlaka ipi hapa inayohusika ili lawama zielekezwe kwao(TBS or TFDA).

Naomba tuelimishane kuhusu hili kama nawe umeshakuwa mhanga wa hili.

Thanks.

Pole nchi yetu ngumu sana
 
Usiamini sana hizo tarehe maana zinachakachulika na wenye maduka wanazipachika tu. Kingine kibaya ktk hili ni namna ya uhifadhi usiozingatia kanuni za afya. Niliacha kutumia mikate miaka mingi sababu nilikuta fungus ktk baadhi ya slesi na tarehe zenu hizo zikiwa mbichi kabisa.
 
Habari mkuu.nakushauri ununue mkate jion kwenye bakery maana bakery nyingi jion wanatoa mikate fresh kutoka motoni.hii ya grocery na shops Sio mizuri.ikumbukwe kuwa mkate mzuri unakaa siku 2.wazalishaji wengi wanaweka calcium ili at least ukae siku 5.
 
Kweli hii ni hatari. Japo hapo ninaponunua mikate huisha mapema sana na ukichelewa hupati lakini hili limenistua sana. Nimejaribu kucheki mkate hapa nyumbani hauna tarehe ya kutengenezwa wala tarehe ya kuisha kutumika. Ni mikate gani yenye kuandikwa hizo tarehe?

Ni kweli Kabisa. Mikate Mingi Sana haiandikwi Tarehe. Na hii inapelekea Mikate Mingi kukaa Dukani hadi zaid ya wiki ikitusubiria Sisi walaji tuende kununua. Mingine inakuwa kama Crisps. Kinachoniudhi unakuwa hujapata kitu ambacho kinaendana na thaman ya Pesa yako.

Sasa basi: labda tu, tupige Campaign kuwa watu tununue Mikate Bakery Mida ya Jion. La sivyo wengi tutaumia sana.
 
ikiwekwa expire date watapata hasara kwani toka uanze kula hiyo mikate mpaka leo ushapata madhara gani?
 
kuna bakery 1o hapa nchini zilizosajiliwa zote zaidi ya 1ooo ni bubu ndugu yangu.endelea tu kujilia za uswahili.hakuna kitu kama hicho.mkate salama in manufacture na expire dates.
 
Mi kuna baadhi ya mikate huwa nakuta imeandikwa lakin asimia kubwa huwa hawaandiki
 
Mikate ina use by ila kwa hapa hawaweki
3f265cfc58e60123dc7a90f80ea1afb5.jpg
 
Endelea kula tu viongoz wanafungua kinywa na cap china na burger
Cappucino nadhan cjakosea namna ya kuiandika.mkuu bongo wananchi tunaishi maisha ya boarding sikiliza wimbo wa jay na ft dully skyes utaona watz tunaishije
 
Sisi tunayotumia imeandikwa kabisa. Tarehe ya kupikwa, then wameandika itumike ndani ya siku tatu tokea ipikwe
 
Mikate ina expire date.. Labda kama munanunua mandazi au mikate ya kihuni ila yote imeandikwa...
Kabla hujaufungua kile kidude cheupe walichofungia kiAngalie vizuri utakuta pale expire date
 
Back
Top Bottom